Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jinsi Simba, Sowah walivyopotezeana muda kiaina

JICHO Pict


SINGIDA Big Stars wamemrudisha nyota wao, Jonathan Sowah ambaye alienda zake Simba kwa kishindo katika dirisha kubwa la mwaka jana. Kilichomtokea Sowah ni kitu ambacho sijawahi kukiona katika mpira wetu kwa hizi timu kubwa.


Nimewahi kuona mchezaji mkubwa kama yeye akienda timu kubwa kisha akashindwa kuonyesha makali yake. Hilo limewahi kutokea mara kadhaa na tunalikubali. Uhamisho wa mchezaji ni sawa tu na mchezaji anayetokea benchi uwanjani.


Vyote hivi viwili ni bahati nasibu. Unaweza kutokea benchi ukaingia uwanjani kipindi cha pili na usifanye maajabu yoyote yale. Ni kama ambavyo unaweza kuhamia timu nyingine huku mashabiki na mabosi wa timu yako mpya wakiwa na matarajio makubwa na wewe lakini usifanye kitu.

SOWA 01

Kesi ya Sowah imekuwa ya ajabu. Kabla hajatuonyesha cheche zake uwanjani akaingia katika mgogoro wa muda mrefu na mabosi wa timu yake. Nasikia pia aliingia mgogoro hadi na benchi lake la ufundi.

Timu ilikuwa Dodoma akarudishwa Dar es salaam aanze kucheza timu ya vijana. Kuanzia hapo mashabiki wa Simba hawakumuona tena uwanjani. Ina maana Sowah aliichezea Simba miezi mitatu tu ya mwanzo. Hatukumuona tena Sowah uwanjani.

Sijui kama wanachama wana haki ya kujua mambo yaliyomtokea Sowah kwa mujibu wa katiba yao. Sijui. Hata hivyo wengi waliishia kuwa kama sisi tusio wanachama wa Simba. Wote tupo gizani kuhusu Sowah.

SOWA 02

Tulichoambiwa ni kwamba mchezaji ana utovu wa nidhamu. Upi? Hatufahamu zaidi. Labda katika mabadiliko ya katiba mpya ya klabu hizi kuwe na vipengele ambavyo vinawalazimisha wanachama kujua mambo kama haya kwa undani kupitia mkutano mkuu.

Vyovyote ilivyo, Sowah na Simba wamejua namna ya kupotezeana muda. Wameuchezea muda haswa. Sowah amekubali kipaji chake kikae benchi muda mrefu. Nasikia aligoma kuomba msamaha klabuni.

Simba nao walishikilia hapo hapo. Walikubali kubakia na mshambuliaji mmoja tu, Suleiman Mwalimu. Hawakujali sana kwamba Sowah angeweza kuwasaidia kule mbele. Sijawahi kuona wakubwa wakiwa na msimamo mkali dhidi ya mshambuliaji nyota klabuni.

SOWA 03

Mara kadhaa wachezaji bora wamewahi kufanya makosa mengi ya utovu wa nidhamu klabuni lakini wamekuwa wakisamehewa kwa urahisi tu.

Wakati mwingine inatokea kwa mashabiki na wanachama kuweka shinikizo kwa viongozi kumsamehe mchezaji staa aliyefanya makosa ya utovu wa nidhamu klabuni.

Kwa Sowah haikuwa hivyo labda kwa sababu alikuwa hajawashika vizuri mashabiki wa timu hiyo. Hakuwa amefunga mabao ya kutosha kabla ya kuanza kwa matatizo yake ya utovu wa nidhamu.

SOWA 04

Lakini kitu kingine ambacho kilisababisha mashabiki wakae kimya ni ukweli kwamba timu yao imeanza kurudi. Ilikuwa inafanya vizuri uwanjani licha ya kutokuwepo kwa Sowah. Akina Libasse Gueye na wengineo waliiweka timu katika ramani nzuri ya ushindani tofauti na mwanzo wa msimu.

Maswali mawili ya kujiuliza baada ya Sowah kurudi zake Singida Big Stars. Kwanza kabisa kwanini watani wa Simba, Yanga hawakuamua kumchukua Sowah wakati huu wanasaka mshambuliaji wa kuziba pengo la Prince Dube?

Lazima kuna kitu ambacho Injinia Hersi Said na watu wake wanafahamu kuhusu Sowah. Mara mbili wamepotezea nafasi ya kumchukua na kumpeleka Jangwani.

SOWA 05

Mara ya kwanza ni ile ambayo watu wote walikuwa wanadhani Sowah angeenda Jangwani baada ya kufunga mabao mengi kwa muda mfupi alipowasili Singida.

Ilijulikana kwamba Sowah alikuwa rafiki wa karibu wa Hersi na mwenyewe alidai kwamba Hersi ni kama baba yake. kwa mshangao wa wengi licha ya kufunga mabao lukuki ndani ya muda mfupi Yanga walipotezea kumchukua na ghafla akaibukia Simba.

Mara ya pili ni hii hapa. Simba wamechana mkataba wake lakini Yanga wamempotezea tena. Inaonekana Yanga kuna kitu wanakifahamu kuhusu Sowah. Lazima kuna kitu wanakifahamu na hawataki kusema.

SOWA 02

Swali la pili lililojitokeza ni namna ambavyo Singida wanaweza kumtumia Sowah. Kama akirudia makali yake akiwa na Singida itakuwa wazi kwamba timu pekee ambayo inamjulia Sowah hapa nchini ni Singida tu.

Kwamba hata kama Yanga hawakumchukua kwa matatizo ya nidhamu, au Simba wameamua kuachana naye kwa sababu ya matatizo ya nidhamu, inakuaje Singida wanamudu kuishi naye? Au wanamvumilia?

Ni hadithi ile ile ya zamani ya Mario Balotelli na kocha, Roberto Mancini. Makocha wengi walishindwa kuishi na Balotelli lakini ikaja kujulikana kwamba kocha pekee anayemudu tabia zake mbovu ni Mancini pekee.

SOWA 02

Tukiachana na hilo, hatimaye Simba wana nafasi nzuri ya kumpata mshambuliaji mwingine ambaye atakuja kuziba nafasi ya Sowah.

Huwa hatuwezi kusema pengo la Sowah kwa sababu mchezaji ambaye ametumia muda mwingine akiwa sebuleni kwake hatuwezi kusema ameacha pengo.

Huyu tunasema ameacha nafasi. Na kwa Sowah mwenyewe ningependa anionyeshe 'kiburi'. Yaani afunge mabao mengi uwanjani msimu ujao ili kuamsha hasira za Wanasimba ambao walikuwa katika upande wa uongozi wakati wa sakata lake hili.