Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msikie Arteta kuhusu EPL 2025/26

Muktasari:

  • Arsenal ilimaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita, pointi 10 nyuma ya mabingwa Liverpool huku nafasi hiyo ya pili ikikaliwa na timu hiyo ya London kwa misimu mitatu mfululizo.

LONDON, ENGLAND: MIKEL Arteta anaamini kutakuwa na timu hadi nane zitakazochuana na Arsenal kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao na kusisitiza, patachimbika.

Arsenal ilimaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita, pointi 10 nyuma ya mabingwa Liverpool huku nafasi hiyo ya pili ikikaliwa na timu hiyo ya London kwa misimu mitatu mfululizo.

Kocha Arteta kwa miaka mitano aliyokuwa kwenye kikosi cha Arsenal, mafanikio yake makubwa ni taji moja tu la Kombe la FA, hivyo anafahamu wazi presha inayomkabili kwenye kuipa timu hiyo taji la Ligi Kuu England, ambalo mara ya mwisho timu hiyo ilibeba mwaka 2004 ilipokuwa chini ya Arsene Wenger, ilipocheza kwa msimu wote bila ya kupoteza mechi yoyote kwenye ligi.

Lakini, kwa mujibu wa kocha huyo Mhispaniola msimu ujao utakuwa mgumu kwelikweli kwenye mbio za ubingwa na pengine itakuwa mara ya kwanza kutokea hivyo.

Liverpool, Manchester City na Chelsea zilimaliza ndani ya Top Four msimu uliopita, wakati Newcastle, Aston Villa na Nottingham Forest zilishindwa kidogo tu.

Mabingwa wa Europa League, Tottenham na Manchester United – zilizomaliza kwenye nafasi ya 17 na 15 mtawalia – zitakuja kivingine msimu ujao baada ya kufanya usajili kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Arteta anaamini Arsenal itakuwamo kwenye ushindani wa ubingwa, hasa baada ya kutumia karibu Pauni 200 milioni kwenye usajili wa dirisha hili, akisema: “Utakwenda kuwa mwaka wa ushindani mkali sana. Kila mwaka vitu vinabadilika. Kutakuwa na timu sita, saba au nane kwenye ligi ambazo kila moja ina uwezo wa kushinda ubingwa na ikumbukwe, bingwa ni mmoja tu."

Arsenal inafanya usajili wa kunasa mastaa wa kuipa ubingwa miamba hiyo ya Emirates kuanzia kwenye Ligi Kuu England hadi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo msimu uliopita ilikomea kwenye hatua ya nusu fainali ilipotupwa nje na Paris Saint-Germain na Arteta alisema: “Tutawezaje kufanya zaidi? Tunajua tupo kwenye hatua za kukaribia hilo na tuna michuano mikubwa miwili tunahitaji kupiga hatua kubwa zaidi.”


MECHI ZA KWANZA LIGI KUU ENGLAND MSIMU WA 2025-26

Ijumaa, Agosti 15, 2025

Liverpool vs Bournemouth (Saa 4:00usiku)


Jumamosi, Agosti 16, 2025

Aston Villa vs Newcastle (Saa 8:30mchana)

Brighton vs Fulham (Saa 11:00 jioni)

Sunderland vs West Ham (Saa 11:00 jioni)

Tottenham vs Burnley (Saa 11:00 jioni)

Wolves vs Man City (Saa 1:30 usiku)


Jumapili, Agosti 17, 2025

Chelsea vs Crystal Palace (Saa 10:00 alasiri)

Nottm Forest vs Brentford (Saa 10:00 alasiri)

Man United vs Arsenal (Saa 12:30 jioni)

Leeds United vs Everton (Saa 4:00 usiku)