Mlango wazi kwa Endrick nchini Brazil
Muktasari:
- Mchezaji huyo alipoamua kubadili msimamo kutokana na kukosa muda wa kucheza katika kikosi cha Real Madrid, moja ya hoja zake kuu mbali na kupata nafasi ya kucheza ilikuwa angalau kuwa katika ushindani wa kuingia kwenye kikosi cha Kombe la Dunia 2026.
LYON, UFARANSA: SUPASTAA wa kimataifa wa Brazil, Endrick, amekuwa gumzo nchini Ufaransa baada ya kiwango chake bora akiwa na Lyon katika Ligi Kuu nchini humo, ambayo anaichezea kwa mkopo akitokea Real Madrid.
Mchezaji huyo alipoamua kubadili msimamo kutokana na kukosa muda wa kucheza katika kikosi cha Real Madrid, moja ya hoja zake kuu mbali na kupata nafasi ya kucheza ilikuwa angalau kuwa katika ushindani wa kuingia kwenye kikosi cha Kombe la Dunia 2026.
Ni kocha wa Brazil wa sasa, Carlo Ancelotti ambaye anamfahamu vizuri tangu msimu wake wa mwisho Real Madrid aliyemshauri kubadili uamuzi ili apate nafasi ya kuchezea nchi yake na kuongeza uwezekano wa kuitwa Kombe la Dunia.
Endrick amefikia lengo la kufanya vizuri Lyon, na takwimu zake zinathibitisha hilo kwani katika michezo minane tayari amefunga mabao matano na kutoa asisti nne. Tangu Endrick aondoke Madrid, straika Kylian Mbappe amefunga mabao tisa na kutoa asisti moja katika michezo tisa, huku Vinicius Jr akiwa na mabao saba na asisti tatu katika michezo 12.
Hivyo, Endrick amehusika katika matukio 10 ya mabao kama mastaa hao wenzake wa zamani, lakini katika michezo michache zaidi. Na sasa kuna sababu nyingine inayompa Endrick nafasi zaidi Brazil, kwani habari mbaya za jeraha la mchezaji mwenzake wa zamani wa Real Madrid huenda zikafungua mlango mwingine kwake kuelekea Kombe la Dunia. Winga Rodrygo Goes amepata jeraha la ligamenti na atakuwa nje ya uwanja kwa kati ya miezi 10 hadi 12 na huyo ndiye aliyekuwa akipambania naye namba kwa Ancelotti kuingia katika kikosi cha Kombe la Dunia. Mashabiki wengi wanaamini Endrick ana kila kitu cha kuwa mchezaji huyo atakayeitwa kwani kwa sasa hakuna mshambuliaji namba tisa aliyehakikishiwa nafasi katika kikosi wala winga.
Katika nafasi mshambuliaji ambayo pia Endrick hucheza Richarlison ambaye mara nyingi huitwa na Ancelotti, Joao Pedro na Cunha.