Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkongwe Brazil aangukiwa ukuta na kufa

KIFO Pict

Muktasari:

  • Tassio alitambuliwa kuwa mmoja wa watu wawili waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea juzi mchana katika eneo la milimani la Santa Teresa mjini Rio de Janeiro, ambalo lilikumbwa na upepo wenye kasi ya hadi kilomita 120 kwa saa.

RIO DE JANEIRO, BRAZIL: MCHEZAJI wa zamani wa timu mbalimbali Ulaya aliyewahi kukipiga Europa League, Tassio Maia dos Santos, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 41 baada ya ukuta kuanguka kutokana na upepo mkali wa dhoruba iliyosababisha vifo vya watu watano nchini Brazil.

Tassio alitambuliwa kuwa mmoja wa watu wawili waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea juzi mchana katika eneo la milimani la Santa Teresa mjini Rio de Janeiro, ambalo lilikumbwa na upepo wenye kasi ya hadi kilomita 120 kwa saa.

Mbali na kucheza Europa League na kuifungia bao CSKA Sofia dhidi ya Vitesse Arnhem, Tassio alifahamika zaidi kipindi chake akiwa mchezaji wa Botafogo, ambapo klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Brazil ilithibitisha kifo chake kupitia taarifa iliyoambatana na picha yake akiwa amevaa jezi ya timu hiyo.

KIF 01

"Kwa masikitiko makubwa, Botafogo inaomboleza kifo cha aliyekuwa mchezaji wetu, Tassio Maia dos Santos, aliyeivaa jezi yetu mwaka 2015, akiwa na umri wa miaka 41. Tassio amefariki baada ya kuangukiwa na ukuta ulioporomoka kutokana na dhoruba kali iliyokumba Rio de Janeiro. Apumzike kwa amani," ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Katika maisha yake ya soka yaliyodumu kuanzia 2002 hadi alipostaafu 2019, Tassio alichezea timu 27. Mbali na kucheza katika nchini Brazil, aliwahi pia kuichezea CSKA Sofia ya Bulgaria na Deportivo Saprissa ya Costa Rica, ambako alifunga mabao matano katika mechi 19.

Ajali iliyomuua ilitokea katika eneo ambalo alikuwa akifanya kazi kwenye jumba la kihistoria lenye mandhari ya kuvutia ya Mlima Sugarloaf na sanamu maarufu la Christ the Redeemer, ambalo hutumika pia kwa shughuli za harusi.

KIF 02

Mtu aliyefariki pamoja naye alikuwa rafiki yake wa karibu na pia mfanyakazi mwenzake. Video zilizoonyeshwa na televisheni nchini Brazil zilionyesha ukuta mkubwa ukianguka na kufunika gari lililokuwa limeegeshwa eneo hilo.

Baada ya taarifa za kifo chake kusambaa, watu wengi walituma salamu za pole kwa familia yake.

Makumi ya miti yaliangushwa na upepo, huku maelfu ya watu wakikwama baada ya huduma zote tatu za reli ya metro mjini Rio de Janeiro kusimamishwa. Mbali na Tassio na mwenzake, mvuvi mmoja alifariki baada ya boti kuzama, huku watu wengine wawili wakipoteza maisha katika Jimbo la Sao Paulo baada ya kuangukiwa na miti iliyong'oka kutokana na upepo mkali.