Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkongwe asisitiza... Casemiro, Ugarte wanasepa Man United

WANASEPA Pict

Muktasari:

  • Casemiro ataondoka Old Trafford mwishoni mwa msimuu, huku United wakitaka kupunguza gharama za mishahara ya klabu, kwani nyota huyo wa Brazil amekuwa mchezaji anayelipwa zaidi United katika nyakati za hivi karibuni, akiwa na mkataba wa karibu Pauni 400,000 kwa wiki.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imetakiwa kutumia fedha nyingi kutafuta mbadala wa kiungo Casemiro na Manuel Ugarte ambao wanaondoka mwisho wa msimu huu, jambo ambalo linaweza kuiathiri timu hiyo iwapo itasubiri hadi msimu umalizike ndipo ianze majadiliano na mastaa wakubwa wanaoweza kuziba mapengo yao.

Casemiro ataondoka Old Trafford mwishoni mwa msimuu, huku United wakitaka kupunguza gharama za mishahara ya klabu, kwani nyota huyo wa Brazil amekuwa mchezaji anayelipwa zaidi United katika nyakati za hivi karibuni, akiwa na mkataba wa karibu Pauni 400,000 kwa wiki.

Lakini, gwiji wa United, Bryan Robson amesisitiza kuwa itaigharimu klabu hiyo fedha nyingi zaidi kupata mtu wa kuziba nafasi ya kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid sambamba na Ugarte ambaye wakala wake, Jorge Mendes ameshawasiliana na Juventus akitaka kumpeleka huko.

WANA 01

Timu hiyo imetengeneza orodha ya majina yanayowajumuisha Elliot Anderson, Carlos Baleba, Adam Wharton na mastaa wawili wa Real Madrid, Aurelien Tchouameni na Federico Valverde ili kwenda kuziba mapengo yatakayoachwa, na Robson anajua hakuna hata mmoja kati yao atakayepatikana kwa bei nafuu.

Nahodha huyo wa zamani wa England na United aliiambia Betfred: “Yeye (Casemiro) anaelewa mchezo vizuri. Ana nguvu katika mipambano, na ni mpenyezaji mzuri wa mpira. Mchezo wake kwa ujumla ni mzuri sana. Nafikiri tutalazimika kulipa fedha nyingi kuziba pengo lake kwa sababu amefanya kazi nzuri sana kwetu."

“Uwiano wa timu unaonekana mzuri kwa sasa, lakini tutalazimika kufanya kazi wakati wa kiangazi na tusisubiri mpaka msimu umalizike ili kumaliza kazi maana wachezaji hao ni ghali na watakuwa ghali zaidi tukisubiri,” amesema mchezaji huyo wa zamani huku akisisitiza kwamba kikosi chao hakina uwezekano wa kumbakiza Ugarte ambaye tayari keshazungumzia kutaka kuondoka Old Trafford.

Wakati Casemiro akielekea kuondoka, Robson analizungumzia umuhimu wa United kumbakiza nahodha Bruno Fernandes, ambapo amesema  kuwa mchango wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno ndani ya klabu hiyo ni mkubwa ni kwa tumaini lao kubwa msimu ujao wa michuano ya kimataifa Ulaya iwapo watafuzu.

WANA 02

“Ukiangalia takwimu zake ni za ajabu, lakini pia ni kijana mzuri. Ni mtu mzuri ndani ya klabu. Kila wakati anatabasamu, anafanya kazi kwa bidii mazoezini na hilo linaonekana uwanjani. Jambo lingine kwake ni kwamba kiwango chake cha utimamu wa mwili ni cha juu sana na haumii mara kwa mara. Ni mchezaji bora sana.”

Kwa upande mwingine, Ugarte aliyejiunga na United kutoka PSG 2024 akiwa amecheza mechi 69, msimu huu umekuwa mbaya zaidi kwake akicheza mara 24 katika mashindano yote, huku saba tu kati ya hayo yakiwa tangu Michael Carrick achukue jukumu mapema mwaka huu.

Kupungua huko kwa dakika za kucheza kumeibua maswali makubwa kuhusu nafasi yake ya muda mrefu katika kikosi, hasa wakati United wanaendelea kubadilika kimkakati.

Kwa mujibu wa La Gazzetta dello Sport, wakala wa Ugarte, Mendes ameanza kutafuta uwezekano wa kumuondoka dirisha la usajili la kiangazi ikiamini kwamba anamtafutia nafasi ya kutua AC Milan au Juventus, huku Napoli pia wakitajwa kuwa na nia kumsajili.