Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UEFA kumbakiza Bruno Old Trafford

Muktasari:

  • Man United inahitaji pointi mbili tu katika michezo yao minne iliyosalia ya ligi ili kumaliza katika nafasi tano za juu za kufuzu Ligi ya Mabingwa.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United United inaamini kufuzu kwao kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kutatosha kumshawishi nyota wao Bruno Fernandes kuendelea kubaki katika viunga vya Old Trafford na kuondoa uwezekano wa kuondoka mwisho wa msimu huu.

Man United inahitaji pointi mbili tu katika michezo yao minne iliyosalia ya ligi ili kumaliza katika nafasi tano za juu za kufuzu Ligi ya Mabingwa.

Fernandes, 31, ana mkataba na Man United hadi mwaka 2027 ukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Hata hivyo, mkataba wake una kipengele kinachomruhusu kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa Pauni 57 milioni na Man United haitokuwa na uwezo wa kumzuia.

Katika kuhakikisha suala hilo halitokei, vigogo wa juu wa mashetani hao wekundu wanaamini kufuzu kwao Uefa kutamvutia zaidi Bruno kuendelea kubakia na asifikiria mpango mwingine.

Nyota huyo ameweka wazi anataka kuiona Man United ikiendana na malengo yake ya kushinda mataji makubwa Ulaya.

Kuelekea msimu ujao, Man United inadaiwa kutaka kusuka zaidi kikosi chao hususan eneo la kiungo na imewaweka katika rada tayari mastaa kama Elliot Anderson, Carlos Baleba, Aurelien Tchouaméni, Federico Valverde na Adam Wharton.

Fernandes alijiunga na Man United mwaka 2020 akitokea Sporting CP kwa ada ya takribani Pauni 47 milioni na tangu wakati huo amekuwa mmoja wa usajili bora wa klabu hiyo.

Licha ya changamoto zilizoikumba Man United katika nyakati za karibuni, Fernandes ameendelea kuwa mchezaji wa kiwango cha juu na sasa yuko karibu kuvunja rekodi ya pasi za mabao katika msimu mmoja wa Ligi Kuu England ambayo kwa sasa ni 20 na yeye anaonekana kuwa anaweza kuivuka.