Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Napoli yajitosa kwa Jadon Sancho

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Sancho ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo, Aston Villa amekuwa akihusishwa na vigogo wengi Ulaya wanaoonekana kuhitaji saini yake hasa wakivutiwa zaidi baada ya kuona atapatikana bure mwisho wa msimu.

KWA mujibu wa ripoti, Napoli ya Italia imefanya mawasiliano ya awali na wakala wa Jadon Sancho kuhusu uwezekano wa kumsajili winga huyo wa Manchester United ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Sancho ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo, Aston Villa amekuwa akihusishwa na vigogo wengi Ulaya wanaoonekana kuhitaji saini yake hasa wakivutiwa zaidi baada ya kuona atapatikana bure mwisho wa msimu.

Mara kadhaa imekuwa ikielezwa Sancho pia anaweza akarudi Borussia Dortmund ambayo pia imeonyesha nia ya kumsajili ingawa changamoto kubwa ni mshahara wake.

Dortmund haipo tayari kumpa staa huyo mshahara unaozidi Euro 200,000 jambo ambalo Sancho anaonekana kutolihitaji kwani mshahara wake wa sasa unafikia Euro 400,000 kwa wiki na anahitaji timu itakayoweza kumlipa walau Euro 200,000 kwa wiki.

Akiwa na Villa msimu huu, amecheza mechi 35 za michuano yote, amefunga bao moja na asisti tatu.


Mohamed Salah

RIPOTI zinaeleza mshambuliaji nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, 33, huenda asitimkie  Saudi Arabia dirisha lijalo.

Taarifa zinadai Salah anaweza kukataa ofa kutoka Saudia na badala yake kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki inayodaiwa kuweka pesa ndefu ili kumshawishi.

Salah ametangaza ataondoka Liverpool mwisho wa msimu huu ikiwa ni baada ya kuhudumu kwa kipindi kisichopungua miaka 10 katika kikosi hicho.


Nicolas Jackson

CHELSEA inaamini inaweza kupata hadi Pauni 60 milioni ikimuuza mshambuliaji wao, Nicolas Jackson, 24, aliye kwa mkopo Bayern Munich.

Jackson ambaye hajapata nafasi kubwa ya kucheza msimu huu, inadaiwa hataki kurudi Chelsea na badala yake amemwambia wakala wake amtafutie timu nyingine ndani au nje ya England.

Inaelezwa Bayern haina mpango wa kuendelea kusalia na staa huyu kutokana na kiwango ambacho amekionyesha.


El Hadji Malick Diouf

MANCHESTER United inamfuatilia kwa karibu beki wa kushoto wa West Ham, El Hadji Malick Diouf, 21, ambaye inahitaji kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Lengo la Man United ni kuongeza ushindani katika nafasi ya beki wa kushoto na Luke Shaw, 30, amekuwa chaguo namba moja. Diouf anaonekana kulivutia zaidi benchi la ufundi la Man United ambalo linaamini atatumika kwa muda mrefu.


James Trafford

TOTTENHAM inatarajiwa kumuuza kipa wao wa kimataifa wa Italia, Guglielmo Vicario, 29, Inter Milan dirisha lijalo la majira ya kiangazi na katika orodha ya makipa wanaoweza wakaziba pengo lake ni James Trafford, 23, kutoka Manchester City na Bart Verbruggen, 23, wa Brighton.

Hata hivyo, makipa hao wote hawataki kufanya uamuzi wowote hadi watakapoona hatma ya Spurs kwa msimu huu ikiwa itasalia katika Ligi Kuu au itashuka.


Alisson Becker

JUVENTUS imeonyesha nia ya kumsajili kipa wa Liverpool, Alisson Becker, 33, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Alisson ana mwaka mmoja tu uliobaki katika mkataba wake, hali inayoifanya Liverpool kufikiria kumuuza kuepuka kumpoteza bure badaye.

Kipa huyo kwa sasa ndio tegemeo Liverpool lakini Juventus inaamini ikimpata itakuwa imemaliza kabisa shida ya eneo la lango lao ambapo wamekuwa wakiruhusu sana mabao.


Azzedine Ounahi

ASTON Villa inachunguza uwezekano wa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Morocco, Azzedine Ounahi, 26, kutoka Girona.

Maskauti wa Villa wamemtazama staa huyu mara kadhaa na wameonekana kuvutiwa naye kiasi cha kupendekeza asajiliwe.

Inaelezwa Girona ipo tayari kumuuza lakini itahitaji zaidi ya Pauni 40 milioni ili kufanya hivyo. Mkataba wake unamalizika mwaka 2030.


Archie Brown

NOTTIGHAM Forest ipo karibu kutoa kiasi cha pesa kinachohitajika ili kuipata saini ya beki wa kushoto wa Fenerbahce, Archie Brown mwenye umri wa m, 23.

Moja kati ya mambo ambayo yameishawishi sana Forest kutaka kumsajili fundi huyu ni uwezo wake mkubwa wa kupandisha mashambulizi mbali ya majukumu yake mama ya kukaba. Mkataba wa sasa wa Archie unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.