Mkongwe arudi Serie A, apewa Parma
Muktasari:
- Gilardino, mwenye umri wa miaka 44, ambaye aliisaidia Italia kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2006 akiwa mchezaji, amepewa nafasi hiyo baada ya klabu hiyo kumtimua kocha wake wa awali.
PARMA, Italia: Kocha Alberto Gilardino amerudi katika Ligi Kuu Italia, Serie A, baada ya kuteuliwa kuwa kocha mpya wa Parma, akipewa mkataba hadi mwisho wa msimu huu.
Gilardino, mwenye umri wa miaka 44, ambaye aliisaidia Italia kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2006 akiwa mchezaji, amepewa nafasi hiyo baada ya klabu hiyo kumtimua kocha wake wa awali.
Parma imesema mkataba huo una kipengele kinachoiwezesha kuongeza muda wa miaka mingine miwili.
Changamoto ya kwanza kwa Gilardino itakuwa kubwa kwani mchezo wake wa kwanza utakuwa dhidi ya mabingwa wa Serie A, Inter Milan, Oktoba 10 baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.
Parma imeanza vibaya msimu huu ikiwa imeshinda mchezo mmoja pekee kati ya mitano ya mwanzo ya Serie A.
Ushindi huo uliupata dhidi ya Genoa katika mchezo wa mwisho wa kocha Cuesta, lakini umejikusanyia pointi nne pekee hadi sasa.
Gilardino amewahi kuzifundisha Genoa na Pisa katika Serie A. Alifutwa kazi na Pisa mwezi Februari baada ya kupata ushindi mmoja tu katika mechi 23 za Serie A.
Uteuzi wake umekuwa mabadiliko ya tatu ya benchi la ufundi katika Serie A msimu huu.
Kabla yake, Paolo Vanoli alichukua nafasi ya Fabio Grosso huko Fiorentina, wakati Raffaele Palladino aliteuliwa kuchukua nafasi ya Domenico Tedesco huko Bologna.