Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MKEKA TAYARI: Magwiji watoa utabiri mapema EPL

Muktasari:

  • Msimu mpya wa Ligi Kuu England ulianza wikiendi iliyopita na mabingwa watetezi Liverpool walianza vyema kwa ushindi.

LONDON, ENGLAND: GARY Neville na Jamie Carragher wametoa utabiri wao wa mambo ya Ligi Kuu England yatakavyokuwa msimu huu wa 2025-26 huku wakipingana kwenye maeneo kadhaa.

Msimu mpya wa Ligi Kuu England ulianza wikiendi iliyopita na mabingwa watetezi Liverpool walianza vyema kwa ushindi.

Washindani wengine kwenye mbio za ubingwa, Arsenal na Manchester City nazo zilinyakua pointi tatu kwenye mechi zao za kwanza, huku Chelsea ilibanwa na Crystal Palace kwa kutoka sare ya 0-0 licha ya kusajili kwa pesa nyingi dirisha lililopita.

Na matokeo hayo yamebadili mawazo ya wawili hao, Carragher na Neville, wakati walipotoa utabiri wa kile ambacho kinaweza kutokea miezi 10 ijayo kwenye mchakamchaka wa Ligi Kuu England.

Katika utabiri wake, Neville ambaye ni gwiji wa Manchester United, amesema Arsenal itachukua ubingwa.

Alisema: “Siwezi kuitenganisha Arsenal, Manchester City na Liverpool. Nadhani na yenyewe ina nafasi sawa ya kushinda ubingwa. Arsenal imekuwa kwenye kiwango bora kwa misimu mitatu ikishika namba mbili. Nahisi sasa wamefikia kwenye kiwango cha kukaa pale juu.

“Liverpool, mabeki wao wa pembeni wapo vizuri. Wanajipambanua sana, bila ya shaka watakwenda kuwa kivutio kuwatazama. Watafunga mabao mengi.

“Man City nayo imekuwa na uti wa mgongo imara. Wataendelea kuwa timu kama iliyokuwa miaka mitatu iliyopita. Na kwenye fowadi, Arsenal itakuwa pazuri kwa kuwa na Viktor Gyokeres pale mbele.”

Carragher hakukubaliana naye, akidai Liverpool ndiyo itakayonyakua ubingwa. Alisema: “Nilichokiona kwenye Ngao ya Jamii, sikukidhania kingetokea usiku wa Ijumaa. Nina hakika kocha alizungumza na wachezaji wake kwenye pre-season hasa baada ya ile mechi dhidi ya AC Milan, Ngao ya Jamii na mechi nyingine kubwa zilizokuwa zinanipa wasiwasi.

“Lakini, kama Liverpool itaboresha tofauti hizo watakuwa moto. Siku chache zilizopita, nilipata hisia ya kudhani Arsenal itakwenda kuwa mshindani mkuu wa Liverpool. Lakini, nilivyowaona walivyocheza dhidi ya Man United, Arsenal imebaki kuwa ileile ya msimu uliopita. Nilivutiwa na Man City na nadhani ni wao ndio watakaokuwa washindani wa Liverpool.”

Ukiweka kando ishu ya ubingwa, kuna vita kali ya kuwania tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Carragher anaziona Man City, Arsenal na Chelsea zitamaliza msimu kwenye Top Four, wakati Neville ametabiri Man United itashindana na Man City na Liverpool kwenye kusaka tiketi ya Ulaya.

Carragher alisema Man United inaweza kuwa sapraizi kubwa kwenye kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya, wakati Neville kwa upande wake, anadhani timu ya sapraizi itakuwa Nottingham Forest. Kwa upande mwingine wa msimamo wa ligi, magwiji hao wote wamekubaliana, Wolves na Burnley zitashuka daraja na kucheza Championship, huku Carragher timu yake ya tatu itakayoshuka akiitaja Sunderland na Neville ameitaja Leeds United.

Lakini, magwiji hao wa Ligi Kuu England kwa pamoja wamemtaja Erling Haaland ndiye atakayekuwa kinara wa mabao msimu huu, huku Carragher akiamini Florian Wirtz utakuwa usajili bora wakati Neville utabiri wake ni Viktor Gyokeres ambaye atakuwa usajili bora.

Na wote hao wamewataja wachezaji Estevao na Adrien Truffert wa Bournemouth watang'ara sana msimu huu. Mwisho kabisa, Carragher anaamini kocha wa Crystal Palace, Oliver Glasner ndiye atakayevutia kumwaangalia, wakati Neville alisema Ruben Amorim, ndiye kocha atakayevutia kumtazama msimu huu.


UTABIRI WA CARRAGHER, NEVILLE KWENYE LIGI MSIMU WA 2025/26


-UBINGWA

Carragher: Liverpool

Neville: Arsenal


-TOP FOUR

Carragher: Man City, Arsenal, Chelsea

Neville: Man City, Liverpool, Man United


-NAMBA TANO

Carragher: Newcastle

Neville: Chelsea


-NAMBA SITA

Carragher: Tottenham

Neville: Newcastle


-SAPRAIZI YA ULAYA

Carragher: Man United

Neville: Nottingham Forest


-KUSHUKA DARAJA

Carragher: Wolves, Sunderland, Burnley

Neville: Leeds, Burnley, Wolves


-MFUNGAJI BORA

Carragher: Haaland

Neville: Haaland


-USAJILI BORA

Carragher: Wirtz (Liverpool)

Neville: Gyokeres (Arsenal)


-MAKOCHA KIVUTIO

Carragher: Glasner (Palace)

Neville: Amorim (Man United)