Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mke amchoma Icardi, afungiwa miaka 73

Muktasari:

  • Nyota huyo wa zamani wa PSG na Inter Milan, ambaye enzi zake alikuwa mashine ya kufunga mabao alijikuta matatizoni baada ya video iliyowekwa mtandaoni na mpenzi wake mpya, China Suarez, kuifanya Wizara ya Uchukuzi ya Argentina kuifuatilia na hivyo kufikia uamuzi huo.

BUENOS AIRES, ARGENTINA: Mshambuliaji wa zamani wa Argentina, Mauro Icardi, amepewa adhabu ya kushangaza ya kufungiwa kuendesha gari kwa miaka 73 baada ya kufanya hivyo bila leseni halali.

Nyota huyo wa zamani wa PSG na Inter Milan, ambaye enzi zake alikuwa mashine ya kufunga mabao alijikuta matatizoni baada ya video iliyowekwa mtandaoni na mpenzi wake mpya, China Suarez, kuifanya Wizara ya Uchukuzi ya Argentina kuifuatilia na hivyo kufikia uamuzi huo.

Video hiyo ilimuonyesha akiwa amening’inia kupitia dirishani mwa gari lililokuwa likiendeshwa na Icardi, nje kidogo ya Buenos Aires, ambapo wizara ilianzisha uchunguzi uliobaini kuwa leseni ya udereva ya mshambuliaji huyo ilikuwa imekwisha muda wake.

Wizara hiyo baadaye ilitoa taarifa kupitia mtandao wa X ikisema: “Tumebaini leseni ya udereva ya Icardi ilikuwa imekwisha muda wake. Kwa sababu hiyo, tumeamuru kusimamishwa kwake kwa muda... mchezaji huyo atahitaji kufanyiwa tathmini ili kubaini kama anastahili kuendesha gari. Usalama barabarani hauruhusu ubaguzi.” Hata hivyo baadaye wizara hiyo ilithibitisha kuwa Icardi amefungiwa kuendesha gari hadi mwisho wa karne hii ikimaanisha kwamba kwa miaka 73 hatagusa usukani wa gari lolote.

Mshindi huyo mara mbili wa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu cha Serie A alitoa kauli kali akijibu adhabu hiyo, akiandika: “Fikirieni kurekebisha barabara ili kuboresha mwenendo wa magari badala ya kupoteza muda kuandika kwenye Twitter....” Mshambuliaji huyo sasa yupo kwenye mzozo wa kisheria dhidi ya wizara hiyo, akipinga kusimamishwa kwa leseni yake kwa matumaini ya kuondolewa adhabu hiyo. Kama sehemu ya adhabu hiyo, Icardi pia amefutiwa leseni yake ya udereva ya Italia, licha ya kuwa ilikuwa halali hadi mwaka 2029.

Mshambuliaji huyo alitumia tena mitandao ya kijamii kueleza kutoridhishwa kwake, akiandika: “Nataka kujua mmewezaje kufuta leseni yangu ya udereva ya Italia.” Mshambuliaji huyo siyo mgeni wa mabishano nje ya uwanja, kwani amewahi kuhusishwa na moja ya kashfa kubwa zaidi katika soka. Mwaka 2013, baada ya kujiunga na Inter Milan, Muargentina mwenzake Maxi Lopez alimkaribisha mara kwa mara nyumbani kwake kukutana na familia yake na kutumia muda pamoja. Kadiri muda ulivyokwenda, Icardi alianza kuwa na ukaribu wa siri na mke wa Lopez wakati huo, Wanda Nara.

Lopez na Nara hatimaye walitengana mwishoni mwa mwaka 2013 na, kwa kushangaza, mwaka mmoja baadaye Nara alifunga ndoa na Icardi. Nara na Icardi walikanusha mara kwa mara kwamba uhusiano wao ulianza kabla ya Nara kuachana rasmi na Lopez.

Hata hivyo, usaliti huo ulidhaniwa ulimfanya mshambuliaji huyo kutocheza katika timu ya taifa ya Argentina kwa sehemu kubwa ya miaka yake ya mwanzo kutokana na uchunguzi na shinikizo alilokumbana nalo.

Nara na Icardi walitengana kwa mzozo mkubwa mwanzoni mwa mwaka jana, na Icardi akaanza uhusiano na mpenzi wake mpya, China Suarez, lakini bado yuko kwenye mchakato wa kisheria na Nara kuhusu makubaliano ya talaka. Kwa sasa Icardi hana timu baada ya Galatasaray kuachana naye.