Mitego ya EPL wiki hii: Nani atapona, nani atazama
Muktasari:
- Kabla ya mapumziko ya wiki tatu ya mechi za kimataifa, macho yataelekezwa kwenye viwanja mbalimbali huku baadhi ya vigogo wakisaka ushindi wa kujinasua na timu nyingine zikilenga kuendeleza mwanzo wao mzuri.
LONDON, ENGLAND: Ligi Kuu England msimu wa 2026/27 inaingia wiki ya tano huku michezo kadhaa ikitarajiwa kutoa majibu muhimu kuhusu mwenendo wa timu mbalimbali.
Kabla ya mapumziko ya wiki tatu ya mechi za kimataifa, macho yataelekezwa kwenye viwanja mbalimbali huku baadhi ya vigogo wakisaka ushindi wa kujinasua na timu nyingine zikilenga kuendeleza mwanzo wao mzuri.
Haya ndiyo maswali 5 makubwa yanayobeba uzito mechi hizo
Man United itafufuka dhidi ya Fulham?
Manchester United inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na presha baada ya kuanza msimu kwa kupata pointi nne pekee katika michezo minne.
Kocha Michael Carrick alikiri baada ya kipigo cha 1-0 dhidi ya Manchester City kwamba timu yake haijapata pointi nyingi kama ilivyotarajiwa.
United pia ilipata pigo jingine katikati ya wiki baada ya kupoteza 3-2 dhidi ya Brighton & Hove Albion kwenye EFL Cup, licha ya kuongoza 2-0.
Sasa safari ya Craven Cottage dhidi ya Fulham inakuwa muhimu zaidi. Sare itamaanisha United imefikia pointi tano baada ya mechi tano, idadi ambayo ni rekodi mbaya zaidi ya klabu hiyo katika hatua hiyo tangu Sir Alex Ferguson alipostaafu mwaka 2013.
Kipigo kitaifanya hali kuwa ngumu zaidi. Hata hivyo, msimu bado ni mchanga na United ina muda mrefu wa kubadilisha mambo.
Chelsea na shida ya ulinzi
Chelsea imeanza msimu kwa kuruhusu mabao mengi, ikiwa imefungwa mara tisa katika mechi nne za Ligi Kuu na kuruhusu angalau mabao mawili katika kila mchezo.
Kocha Xabi Alonso amekiri kuwa makosa hayo ya kiulinzi yamekuwa yakijirudia na kwamba itachukua muda kuyarekebisha.
Tatizo jingine ni kwamba mpinzani wao, Brentford, ni timu inayojua kutumia nafasi kwenye mashambulizi ya kushtukiza.
Alonso anaweza kutazama uzoefu wake akiwa Bayer Leverkusen, ambako timu yake iliruhusu mabao 49 katika msimu wake wa kwanza Bundesliga, kabla ya kupunguza idadi hiyo hadi 24 msimu uliofuata.
Hivyo, swali kubwa ni kama Chelsea inaweza kuanza kuonyesha nidhamu zaidi katika ulinzi wakati itakapokuwa ikivaana na Brentford ambaye imeshafunga mabao saba kwenye michezo minne.
Vita ya Spurs kutafuta bao Huu ni miongoni mwa michezo mikubwa ya wikendi.
Tottenham Hotspur na Aston Villa zote zimeanza msimu bila ushindi na zinashikilia nafasi za chini kwenye msimamo, hali ambayo haikutarajiwa kutokana na matarajio yao ya kucheza michuano ya Ulaya.
Mabadiliko makubwa ya vikosi wakati wa dirisha la usajili yanaonekana kuhitaji muda kwa timu hizo kuzoeana.
Kwa Roberto De Zerbi wa Spurs na Unai Emery wa Villa, ushindi katika mchezo huu unaweza kuwapa nafasi ya kuingia kwenye mapumziko ya kimataifa wakiwa na matumaini mapya.
Lakini kipigo kinaweza kuongeza presha kabla ya mapumziko hayo ya wiki tatu, ingawa Spurs inakabiliwa na uhaba wa mabao ikiwa haijafunga bao lolote kwenye michezo minne iliyocheza.
Man City inaendeleza kasi
Manchester City inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na rekodi ya asilimia 100 baada ya kuifunga Manchester United kwenye Dabi ya Manchester.
Ushindi huo wa Old Trafford, uliopatikana licha ya City kucheza ikiwa pungufu kwa mchezaji, umeongeza morali kwenye kikosi cha Pep Guardiola.
Sasa inakutana na Sunderland ambayo inaweza kuwa imechoka kutokana na kushiriki michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya miaka 50.
Sunderland ilimaliza nafasi ya saba msimu uliopita, lakini kucheza mechi mbili kwa wiki ni changamoto kubwa kwa kikosi ambacho hakikuwa kimepanga mapema kushiriki mashindano hayo.
Pia Sunderland bado haijashinda ugenini msimu huu, ikiwa imefungwa na Ipswich na kutoka sare dhidi ya Brentford.
Bournemouth na Liverpool moto mzito
Mchezo wa Bournemouth dhidi ya Liverpool unaweza kuwa mmoja wa mechi zenye kasi kubwa wikendi hii.
Bournemouth ilionyesha uimara wa ulinzi kwa kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Fulham, jambo ambalo lilimfurahisha kocha Andoni Iraola, hasa kutokana na mechi nyingi za fujo alizokuwa akikumbana nazo wakati wa mwanzo wa utawala wake klabuni hapo.
Lakini sasa Bournemouth ipo chini ya Marco Rose na imefungwa mabao mawili katika mechi tatu kati ya nne.
Liverpool nayo inatarajiwa kuwa tishio kubwa mbele ya lango, huku Bournemouth ikiwa imefunga katika kila mchezo wa Ligi Kuu msimu huu.
Mitindo ya timu hizo yenye presha kubwa, kasi na mashambulizi ya moja kwa moja inaweza kufanya mchezo huu kuwa wa kuvutia na wenye mabao mengi.
Brighton inaweza kuipasua Arsenal?
Brighton imeanza msimu kwa kuvutia, ikiwa ndiyo timu iliyofunga mabao mengi zaidi hadi sasa, ikiwa na 13.
Timu hiyo pia imekuwa na idadi kubwa zaidi ya kupokonya mpira juu kwenye eneo la mpinzani, ikiwa imefanya high turnovers 41.
Hiyo inaonyesha Brighton haitakuwa tayari kukaa nyuma dhidi ya Arsenal.
Lakini Arsenal yenyewe imeonyesha uimara mkubwa wa ulinzi, ikiwa imekabiliwa na nafasi zenye thamani ya mabao 2.7 pekee kwa mujibu wa kipimo cha xG katika mechi zake za Ligi Kuu hadi sasa.
Brighton italazimika kutumia presha na ubunifu wake kuvunja ulinzi huo.
Leeds na mwanzo mzuri
Leeds imeanza msimu kwa kiwango kinachowapa mashabiki wake sababu ya kuota nafasi za juu.
Ina pointi nane baada ya mechi nne, mwanzo wake bora tangu msimu wa 2001/02 chini ya David O'Leary.
Ushindi wa 4-1 dhidi ya Newcastle ulikuwa moja ya matokeo yaliyowapa nguvu zaidi.
Lakini Crystal Palace inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na matatizo yake ya ulinzi.
Palace imeruhusu mabao 11, imekabiliwa na xG 8.15 na wapinzani wake wamefikia mpira mara nyingi ndani ya eneo lake la hatari.
Leeds ikishinda, itazidi kujisogeza kwenye mjadala wa nafasi za kucheza Ulaya.