Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikel Arteta hataki mchezo EPL

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Arsenal iliendelea na rekodi yake ya ushindi wa asilimia 100 katika kutetea taji lake Jumamosi usiku, baada ya mabao ya Bruno Guimaraes na Bukayo Saka kuipa timu hiyo pointi tatu.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amekosoa vikali uamuzi wa mwamuzi John Brooks wa kuipa Sunderland penalti katika ushindi wa mabao 2-0 wa Arsenal dhidi ya Black Cats, akisema uamuzi huo ulikuwa “haukubaliki” katika kiwango hicho cha soka.

Arsenal iliendelea na rekodi yake ya ushindi wa asilimia 100 katika kutetea taji lake Jumamosi usiku, baada ya mabao ya Bruno Guimaraes na Bukayo Saka kuipa timu hiyo pointi tatu.

Hata hivyo, mambo yangeweza kuwa tofauti kabisa baada ya Sunderland kupewa penalti wakati mchezo ukiwa bado 0-0.

Brooks aliamuru penalti baada ya kubaini kuwa Ezri Konsa alimvuta Dan Ballard hadi chini wakati wa mpira wa kona. Uamuzi huo ulipitiwa na VAR, lakini ukaendelea kusimama.

ART 01

Kwa bahati ya Arsenal, kipa David Raya alifanya kazi kubwa kwa kuupangua mpira wa Enzo Le Fee, akidandia upande wake wa kushoto na kuzuia Sunderland kupata bao la kuongoza.

Baada ya mchezo, Arteta hakuficha hasira zake kuhusu uamuzi huo.

“Ni ushindi mkubwa, lakini mambo yangeweza kuwa tofauti kabisa,” amesema Arteta katika mahojiano na TNT Sports.

Alipoulizwa alimaanisha nini, Arteta alijibu kwa kifupi: “Unajua kwa namna gani, kwa namna ambavyo wangeweza kubadili mchezo. Unajua ni nani.”

Baada ya mwandishi kumtaja uamuzi wa penalti, Arteta alifunguka zaidi.

“Ndio, ndio. Nimekasirika sana. Hii haikubaliki katika kiwango hiki. Haikubaliki. Hii inaweza kubadili mwelekeo wa msimu, ubingwa. Hii haikubaliki,” amesema.

Arteta ameongezakuwa alitazama tukio hilo mara kadhaa ili kujiridhisha kabla ya kutoa msimamo wake.

ART 02

“Nimelitazama mara 10 kuhakikisha, kwa sababu nililiona moja kwa moja na nikasema haiwezekani katika kiwango hiki kwamba hii inaweza kuwa penalti. Ni kama mtu anafanya judo, huo ndio ulikuwa mchezo wenyewe, na hauwezi kutokea,” amesema.

“Kwa mtazamo wangu, na kwa mtazamo wa mtu yeyote aliyewahi kucheza soka, hiyo si penalti. Katika hali yoyote, kwenye mchezo wowote, katika mazingira yoyote au ligi yoyote.”

Arteta amesema pia angezungumza na mwamuzi Brooks baada ya mahojiano hayo ili kumweleza wazi hisia zake kuhusu uamuzi huo.