Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United inavyopitia kwenye tanuru la moto

Muktasari:

  • Kuna sababu za kupunguza lawama kuhusu kipigo dhidi ya City kutokana na dabi hiyo kuchezwa siku tatu baada ya ushindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sabah, Alhamisi, huku kikosi cha Enzo Maresca kikiwa na mapumziko ya saa 48 zaidi baada ya kuifumua Porto.

MANCHESTER, ENGLAND;Je, Manchester United ni mbaya kiasi kama awali Ligi Kuu England (EPL)? Manchester United ipo nafasi ya 13 katika Ligi Kuu England (EPL), ikiwa imekusanya pointi nne katika mechi nne za kwanza; ilifungwa 2-0 na Hull, ikaifunga Ipswich 5-2, ikatoka sare ya 2-2 ugenini dhidi ya Everton na kufungwa 1-0 na Manchester City, Jumapili iliyopita.

Kuna sababu za kupunguza lawama kuhusu kipigo dhidi ya City kutokana na dabi hiyo kuchezwa siku tatu baada ya ushindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sabah, Alhamisi, huku kikosi cha Enzo Maresca kikiwa na mapumziko ya saa 48 zaidi baada ya kuifumua Porto.

Hivyo, je, United, ambayo Jumatano ilikuwa wenyeji wa Brighton katika Carabao kabla ya kwenda Fulham kucheza EPL Jumapili wiki hii ni mbaya kiasi hicho kama msimamo unavyoonyesha?

CARRICK NI SOLSKAJAER MPYA?

Baada ya Ole Gunnar Solskjaer kuteuliwa kuwa kocha wa muda Desemba 2018 kutokana na kipindi cha misukosuko cha Jose Mourinho, alishinda mechi 14 kati ya 19 na akapewa kazi ya kudumu mwezi Machi 2019. Kilichofuata ilikuwa anguko la ghafla akishinda mechi mbili kati ya 10 na United kumaliza katika nafasi ya sita ambayo Solskjae aliikuta alipowasili.

Carrick alifufua hali ya klabu akiwa kocha wa muda msimu uliopita baada ya anguko na kufukuzwa kwa Ruben Amorim, na akaiongoza United hadi nafasi ya tatu. Hata hivyo, baada ya kupewa majukumu ya kudumu matokeo yameanza kuwa mabaya.

Kwa sababu tu Solskjaer alikuwa na timu isiyotulia na hakuwahi kuwa salama kwenye nafasi yake ya kazi (akifukuzwa Novemba 2021), haimaanishi kwamba aliyekuwa mchezaji mwenzake na msaidizi wake atapitia uzoefu kama huo.

Lakini, Carrick yupo umbali wa matokeo mangapi zaidi mabaya kabla Jason Wilcox hajaanza kulaumiwa kwa kumteua haraka mchezaji mwingine maarufu wa zamani wa United? Dalili kwamba mkurugenzi wa soka huenda alikuwa na shaka kuhusu Carrick inaweza kuwa katika muda mfupi wa mkataba aliopewaambao unaendelea hadi 2028.

LEGELEGE INAYOTIA HOFU

Phil Foden alipotolewa kwa kadi nyekundu baada ya dakika 23 katika Uwanja wa Old Trafford, Jumapili iliyopita, United ilikuwa na faida ya mchezaji mmoja dhidi ya Man City. Lakini ,kikosi cha Carrick kilibaki kimetulia bila kufanya lolote la maana, huku kiungo cha kati cha Kobbie Mainoo na Youri Tielemans kikishindwa kutawala mchezo na kutengeneza nafasi kwa washambuliaji wanne Bruno Fernandes, Bryan Mbeumo, Matheus Cunha na Marcus Rashford.

Kwa mara ya kwanza katika mechi 12 za nyumbani za EPL chini ya Carrick, United ilitengeneza mabao yanayotegemewa (xG) chini ya 1.0 (0.95), jambo ambalo linapaswa kuwa wasiwasi zaidi kwa Carrick kuliko uamuzi wa VAR uliokuwa karibu na kuchekesha ulioruhusu bao la ushindi la Erling Haaland (Enzo Fernandez, kama Pro Ref ilivyokiri baadaye, alikuwa ameingilia mchezo).

Tatizo hilo hilo lilionekana katika kipigo cha mchezo wa kwanza dhidi ya Hull, ambapo Andrey Santos alicheza na Tielemans kulikuwa na tishio karibu sifuri la kufunga na kikosi cha Carrick kilionekana kuwa legevu.

BEKI MPYA KUSHOTO AANZA KUNG’ATA

Inabidi ujiulize kwa nini nia ya kusajili beki wa kushoto iliyodumu kipindi chote cha dirisha la usajili la majira ya kiangazi, iliyomhusisha Lewis Hall wa Newcastle United kama lengo namba moja, Myles Lewis-Skelly wa Arsenal na David Raum wa RB Leipzig, haikufanikiwa.

Kutambua kwamba nafasi fulani inahitaji kuimarishwa, kisha kushindwa kufanya hivyo kunaonekana kama uzembe na huenda hakukumfurahisha Carrick. Badala yake, viungo watatu walisajiliwa kina Tielemans, Santos na Carlos Baleba. Kwa kuwa Mainoo na Manuel Ugarte (ambaye ana majeraha ya muda mrefu) wapo kwenye kikosi, kuna hoja kwamba usajili wa viungo watatu ulikuwa mmoja zaidi ya uliohitajika katika eneo hilo.

Badala yake, fedha za, kwa mfano, Santos (Pauni 48milioni pamoja na Pauni2 milioni) zingeweza kuwekezwa kwenye beki wa kushoto.

Mechi nne tu ndani ya msimu, uwezekano wa kufanya uamuzi mbaya katika hilo umeanza kuonekana. Luke Shaw, beki wa kushoto chaguo la kwanza ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha katika kipindi bora cha taaluma yake, hakuwepo katika mchezo dhidi ya City kutokana na jeraha, na Carrick alilazimika kumtumia Patrick Dorgu kama suluhisho la muda.

Katika mchezo kama huo msimu uliopita, Mdenmark huyo alicheza kama mshambuliaji wa pembeni upande wa kushoto na alifunga bao. Lakini Jumapili iliyopita, Josko Gvardiol alipompasia Haaland kutoka upande wa kulia wa United na mshambuliaji huyo kufunga kwenye nguzo ya mbali, Dorgu ndiye aliyekuwa akimkabili Mkroratia huyo badala ya kuwa katika eneo lake la ulinzi upande wa kushoto ili kumzuia mshambuliaji wa City. Pia, ni kichwa kibaya cha Dorgu kilichowapa City mpira na kuwawezesha kuanzisha shambulizi hilo.


WALIOTUA WANA KAZI NZITO

Kwa uwekezaji wa Pauni 148 milioni, United iliwasajili Santos, Tielemans (Pauni 35 milioni) na Carlos Baleba (Pauni 65 milioni). Matokeo hadi sasa? Santos ameanza mchezo mmoja (ule wa kipigo dhidi ya Hull), huku Tielemans akiwa haonekani kabisa licha ya kuanza katika mechi zote nne za ligi. Kisha unamfikia Baleba, usajili uliokuwa gumzo zaidi ambaye bado hajacheza hata dakika moja kutokana na jeraha.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon hatarajiwi kurejea hadi baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa. Katika kipindi hiki cha mwanzo cha msimu hakuna kati ya mambo haya ambayo yangekuwa na umuhimu mkubwa kama matokeo yangekuwa mazuri zaidi.

Katika mahojiano kwenye kambi ya mazoezi ya United ya kabla ya msimu huko County Kildare mwezi Agosti, Tielemans alikiri kwamba hakuna klabu nyingine iliyokuwa na nia ya kuamsha kipengele cha mkataba wake cha kuachiliwa kwa Pauni 35m akiwa Aston Villa.

Wakati United ikijaribu kuufufua msimu wake, nahodha huyo wa Ubelgiji anahitaji kujitoa zaidi kama mchezaji na kiongozi.

NI WAKATI WA SESKO KUANZA?

Straika Benjamin Sesko alirejea kutoka kwenye jeraha wakati msimu ulipoanza na amecheza kama mchezaji wa akiba katika mechi zote za ligi za United msimu huu, huku kuanza mchezo wa nyumbani dhidi ya Sabah ambao alifunga bao katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mslovenia huyo pia alifunga katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya Everton jambo linalomfanya kuwa mfungaji wa tatu kwa pamoja wa United kwenye ligi, nyuma ya Bruno Fernandes (mabao matatu) na Bryan Mbeumo (mawili).

Matheus Cunha na Marcus Rashford hawajafunga bao lolote kwenye ligi katika mechi nne na tatu walizoanza mtawalia, na uwezo wa Sesko wa kucheza moja kwa moja kama mshambuliaji asili namba tisa unaweza kuwa chaguo linalostahili kujaribiwa kuanzia mwanzo katika mchezo dhidi ya Fulham.