Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikasa, vihoja mbio za kubebana wenza

Muktasari:

  • Mashindano hayo ya mbio za mume akiwa amembemba mke wake kupitia njia yenye vikwazo vingi, mchanga, kokoto, bwawa la maji na matope yatafanyika Julai 4 na 5.

Kila mwaka mji mdogo wa Sonkajaervi uliopo Finland humiminika mamia ya watu, hasa kutoka nchi jirani kuhudhuria mashindano ya dunia ya aina yake yanayofanyika kila mwaka.

Mashindano hayo ya mbio za mume akiwa amembemba mke wake kupitia njia yenye vikwazo vingi, mchanga, kokoto, bwawa la maji na matope yatafanyika Julai 4 na 5.

Katika miaka ya nyuma mbio hizo zilikuwa za masafa marefu zaidi na kujumuisha kupanda milima, kuruka naye viunzi vifupi na hata kuogelea katika bwawa akiwa mgongoni.

Mashindano hayo ya dunia ambayo yalianza Finland tangu 1992 ni yenye historia ya kuvutia ya zaidi ya karne mbili na siku hizi hufanyika katika nchi nyingi za Ulaya, Marekani ya Kaskazini na Kusini na katika nchi kadhaa za Asia.

Katika Bara la Afrika mashindano hayo yameanza hivi karibuni kufanyika Afrika Kusini. Lakini kumbukumbu zinaonyesha Wagiriki wa mji wa Olimpia walikuwa na mchezo huo zaidi ya karne mbili zilizopita kama kipimo cha kijana anayeweza kutorosha msichana na kwenda mpaka atakapo akiwa naye mgongoni.

Katika mashindano hayo ya dunia ya mita 250 huyo mke anayebebwa anatakiwa awe na uzito wa angalau kilo 49 na akiwa chini ya hapo, basi ili kuongezeka uzito atapaswa abebe mfuko  begani wenye mchanga au kokoto ili kuongeza uzito wake.

Mashindano hayo katika baadhi ya nchi hasa Estonia huwa ya mume kutakiwa kumbeba mkewe akiwa kichwa chini miguu juu.

Miongoni mwa masharti kwa washiriki ni kutoa vielelezo, hasa cheti cha ndoa kuwa huyo unayekwenda naye katika mashindano ya mume kumbeba mkewe mgongoni ni mke wake wa ndoa.

Kama mzee mwenye mke mnene na mzito sana anataka kushiriki mbio hizo ili kuonyesha hadharani mahaba yake kwa mkewe huyo ni shauri yake. Lakini baadhi ya nchi zimeamua kulegeza masharti, kama ya kuruhusu mwanamume kumchukua mwanamke jirani au hata kahaba kushiriki naye kama mke mwenza wa muda.

Zawadi halisi ya mshindi ni kupewa bia yenye uzito sawasawa na mke, lakini baadhi ya nchi zimekuja na zawadi za ziada za fedha na vitu mbalimbali.

Masafa rasmi ya mbio hizo ni mita 253.5 na katika baadhi ya nchi mwanamume anaweza kutafuta mwanamke yeyote yule kama mwenza wake katika mbio hizo.

Mchezo huu umekuwa na vioja kama ilivyo kwa michezo mengine. Miongoni mwa vioja vilivyotia fora ni cha kijana mmoja wa Estonia kumchezea rafu rafiki yake wa karibu wa kiume aliyemuazima mpenzi wake kuingia naye katika mashindano.

Baada ya mashindano yule dada aliyebebwa mgongoni aliamua kubaki na huyo aliyembeba kama mpenzi wake. Alipoulizwa ilikuwaje hata akafikia uamuzi huo alisema: “Namna alivyonibeba kulinifanya kuhisi huyo ndiye mpenzi sahihi kwangu. Huyo niliyekuwa naye hajawahi kunibeba hata siku moja.”

Hii ilisababisha katika mashindano ya mwaka jana kutolewa angalizo la kuwataka wanawake walioazimwa kushiriki mbio hizo wasigeuze kibao na kubadili wapenzi kwani wao ni wenza wa muda tu kwa ajili ya mbio hizo.

Haikuchukua muda wakafunga ndoa na yule kijana aliyeporwa mpenzi wake alihudhuria harusi na kusema ni vyema amesalitiwa kabla ya kufunga ndoa na aliwatakia kila la heri na kilichobaki ni kutafuta mwanamke atayekuwa mwenye mapenzi ya kweli kwake. 

Katika mashindano yaliyofanyika Machi 5, mwaka jana katika mji wa Surrey, Uingereza jamaa mmoja alikuja na mpya. Alijiandikisha kushiriki katika mashindano na mbwa wa kike akisema ndiye mkewe wa muda mrefu.

Waandaaji walikataa na alipobisha na kutishia kufungua mashitaka kwa kufanyiwa ubaguzi, Joel Hicks aliruhusiwa kuingia katika mashindano kwa kumbeba mkewe (mbwa) mgongoni.

Lakini kwa kuwa mbwa alikuwa na uzito mdogo ilibidi afungishwe kizigo cha mchanga ili uzito ufikie kilo 50. Wengi wa watamaji walimshangilia, lakini alimaliza wa mwisho katika mbio hizo  huku mbwa wake akibweka kila walipopitwa na wapinzani wao katika mbio hizo ziizokuwa za masafa ya mita 380.

Mbio hizo za kubebana mgongoni zilichukua sura mpya katika nchi ya Nepal mwaka huu kwa kuanzishwa mashindano ya mke kumbeba mumewe wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wananaake Duniani, Machi 8.

Lengo ni kutaka kudhihirisha uwezo wa mwanamke katika harakati za kampeni ya usawa wa kijinsia kwa kuonyesha naye ana uwezo wa kumbeba mume na kwenda naye pamoja katika safari yenye shuruba.