Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikal Bridges alivyopiga dili la mabilioni Knicks

NBA Pict

Muktasari:

  • Kwa mtu ambaye hajui mpira wa kikapu taarifa hii inaweza kuonekana ya kawaida, lakini kwa muktadha wa mchezo mkataba huo unaonyesha uwekezaji mkubwa ambao Knicks imeufanya kwa Bridges. 

CALIFORNIA, MAREKANI: TIMU ya kikapu ya New York Knicks imefanikiwa kumsaini mmoja wa wachezaji wake muhimu, Mikal Bridges, kwa kumuomngeza mkataba wa miaka minne wenye thamani ya Dola 150 milioni (takriban Sh390 bilioni).

Kwa mtu ambaye hajui mpira wa kikapu taarifa hii inaweza kuonekana ya kawaida, lakini kwa muktadha wa mchezo mkataba huo unaonyesha uwekezaji mkubwa ambao Knicks imeufanya kwa Bridges. 

Huyo ni mchezaji ambaye si tu anajua kufunga, bali ni aina ya wachezaji wanaotoa michango mikubwa uwanjani kwa kazi ambazo unaweza usizione mara moja kama vile kuwazuia wapinzani na kucheza kila mechi bila kukosa mchezo.

NB 01

ALICHOFANYA BRIDGES

Katika msimu wake wa kwanza akiwa na Knicks, Bridges alikuwa na wastani wa kufunga pointi 17.6 kwa kila mechi akiwa pia na ribaundi 3.2 (kuokota mipira iliyogonga mwamba wa nyavu) na asisti 3.7.

Hizi siyo tu takwimu kubwa kwa mchezaji wa kiwango chake, lakini mchango wake mkubwa ulikuwa upande wa ulinzi na uimara wa kuwapo uwanjani kila siku.

Bridges hajawahi kukosa mchezo hata mmoja tangu aanze kucheza NBA 2018. Ameshacheza michezo 556 mfululizo hadi sasa jambo linalomfanya aitwe mwamba wa NBA, yaani mtu ambaye ni mgumu kama chuma kwa sababu haumii wala haachwi nje.

Kwa kawaida wachezaji wa NBA hukosa mechi nyingi kutokana na majeraha au sababu zingine, lakini Bridges ni tofauti.


KUONGEZA NGUVU

Mkataba huu mpya utamuweka Bridges New York hadi msimu wa 2029-30, japokuwa ana nafasi ya kuchagua kujiondoa kabla. Alichofanya kinavutia zaidi kwa sababu angeweza kusubiri hadi mkataba wake wa sasa uishe msimu ujao na kupata fedha zaidi, lakini alikubali kiasi kidogo ili kusaidia timu iwe na nafasi ya kuongeza wachezaji wengine muhimu.

Hii inaonyesha ni jinsi gani anapenda kuwa sehemu ya mipango ya muda mrefu ya Knicks.

Uongozi wa timu hiyo ulitumia machaguo matano ya mzunguko wa kwanza wa wachezaji chipukizi kumpata kutoka Brooklyn Nets.

Ni uamuzi mkubwa ambao hauwezi kufanywa bila kuwa na imani ya dhati na uwezo wa mchezaji.

NB 02

UBORA WAKE

Wakati wa michezo ya mtoano (playoffs) mwaka huu, Bridges alifanya kazi kubwa ya kuwazuia wachezaji hatari wa Boston Celtics ambao walikuwa mabingwa wa NBA msimu uliopita. Katika mechi ya nusu fainali ya Mashariki, Bridges alifanya kazi nzuri ya kuwazuia Celtics jambo lililoisaidia Knicks kuingia fainali ya Kanda ya Mashariki kwa mara ya kwanza tangu 2000.

Bridges amekuwa na uzoefu mkubwa, kwani aliwahi kuipeleka Phoenix Suns katika fainali ya NBA 2021 na mwaka uliofuata alikaribia kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ulinzi. Hali hiyo ilimfanya kuwa mchezaji wa thamani kubwa hadi Brooklyn ilipomtoa kwa ajili ya kumpata Kevin Durant.

NB 03

MJENZI WA TIMU YA NDOTO

Mpango wa Knicks sasa unaonekana kueleweka kuunda timu imara inayoweza kupambania ubingwa.

Bridges ameungana tena na rafiki zake wa zamani kutoka Chuo Kikuu cha Villanova yaani Jalen Brunson na Josh Hart.

Ushirikiano wao uwanjani umeonekana kuzaa matunda mapema na sasa wakiwa chini ya kocha mpya Mike Brown matumaini ni makubwa.