Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Michael Olise mbioni Real Madrid

OLISE Pict

Muktasari:

  • Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa Olise amekuwa akizungumza na wachezaji wa Real Madrid waliopo kwenye kikosi cha Ufaransa, akiwemo Kylian Mbappé na Aurélien Tchouaméni, ili kupata taarifa zaidi kuhusu klabu hiyo.

MADRID, HISPANIA: NYOTA wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ufaransa, Michael Olise, ameripotiwa kuwa na hamu kubwa ya kujiunga na Real Madrid katika dirisha hili la usajili.

Kwa mujibu wa gazeti la L'Equipe, Olise mwenye umri wa miaka 24 amewaambia wenzake wa timu ya taifa ya Ufaransa wakati wa Kombe la Dunia kuwa ndoto yake ni kuwachezea mabingwa hao wa Hispania.

Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa Olise amekuwa akizungumza na wachezaji wa Real Madrid waliopo kwenye kikosi cha Ufaransa, akiwemo Kylian Mbappé na Aurélien Tchouaméni, ili kupata taarifa zaidi kuhusu klabu hiyo.

OLI 01

Olise alijiunga na Bayern Munich mwaka 2024 kwa ada ya pauni milioni 50 na bado ana miaka mitatu katika mkataba wake, hivyo Real Madrid italazimika kulipa fedha nyingi ikiwa itataka kumsajili.

Mlinzi wa Bayern Munich, Dayot Upamecano, anaripotiwa kumshawishi Olise kubaki nchini Ujerumani.

Olise amekuwa katika kiwango bora msimu huu baada ya kufunga mabao 16 na kutoa pasi 27 za mabao katika mechi 39 za ligi. Pia anaongoza kwa kutoa pasi za mwisho za mabao (assist) tano kwenye Kombe la Dunia.

OLI 02

Awali Liverpool ilihusishwa na nia ya kutoa ofa kubwa ya pauni milioni 173 kwa ajili ya Olise kama mbadala wa Mohamed Salah, lakini Bayern Munich ilisisitiza kuwa haikuwa tayari kumuuza.

Aidha, jina la Olise liliwahi kutajwa wakati wa uchaguzi wa urais wa Real Madrid, ambapo ilidaiwa klabu hiyo ilikuwa tayari kutoa pauni milioni 130 iwapo rais Florentino Pérez angeendelea kuongoza. Hata hivyo, hadi sasa hakuna mazungumzo rasmi yaliyoanza kati ya Real Madrid na Bayern Munich kuhusu uhamisho huo.