Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miaka kumi ya pata potea Son, Spurs

SON Pict

Muktasari:

  • Kane aliondoka Spurs tayari miaka ikiwa imesonga, aliondoka na uwezo wa kufunga lakini sio ule wa miaka mitano nyuma yake. Kwenda kwake Bayern haikuwa kwa sababu ya pesa.

LONDON, ENGLAND: WAINGEREZA walikuwa wanaumia sana kuona Harry Kane akiwa anatimiza miaka 30, halafu katika kabati lake hana medali ya ubingwa unaoeleweka. Bosi wa Spurs, Daniel Levy alipindua kisogo kila wakati timu kubwa zilipogonga hodi mlangoni kwake kutaka huduma yake.

Kane aliondoka Spurs tayari miaka ikiwa imesonga, aliondoka na uwezo wa kufunga lakini sio ule wa miaka mitano nyuma yake. Kwenda kwake Bayern haikuwa kwa sababu ya pesa.

Spurs alikuwa akipokea mshahara mwingi na kuwa katika orodha ya wachezaji wanaovuna zaidi EPL. Pia pesa yake ilikuwa inakatwa kodi kidogo kwa sababu pale ni nyumbani.

Mashabiki wa soka wa England walitamani sana kuona akiondoka kwenda timu ambayo itamwezesha kuchukua ubingwa aidha wa Ligi  Kuu au michuano ya kimataifa na Bayern ilionekana kuwa ni timu sahihi yakwenda kwa wakati huo.

Msimu uliopita ndoto hiyo ilitimia na akapata alichokuwa anakiota. Ingekuwa aibu ya karne kwa kiwango chake cha kuwa mfungaji bora wa EPL mara tatu kumaliza maisha yake ya soka bila ya taji lolote.

Juzi kati, Son Heung-min naye aliaga. Moja ya vipaji vikubwa kuwahi kucheza EPL. Mara zote Daniel Levy alipotumiwa Email ya ofa kwa ajili ya kumuuza, alipinga kufanya hivyo.

Timu kubwa nyingi zilienda magharibi na mashariki kwa ajili ya kuipata huduma yake hakuna walichoambulia. Spurs ilifanikiwa kuruka viunzi na kubakia naye kwa miaka 10.

Hadithi yake huenda ikawa ni tofauti na ilivyo kwa Kane, yeye anaondoka Spurs na timu  anayotarajiwa kujiunga nayo ni Los Angeles FC.

Ni rasmi katika miaka yake 33, ya kuishi duniani, anakubalika kwa soka lake la ushindani. Lakini katika kabati lake kwenye jumba lake la kifahari kule Seoul, Korea Kusini kuna medali moja tu ya ubingwa ambayo ni ile ya Europa League waliyopata msimu uliopita.

Zaidi ya hapo Son hajawahi kubeba taji lolote jingine la ngazi ya klabu na tayari ameshatupa taulo kukubali kwamba hawezi kuendelea tena, ni miaka 10 ya pata potea, waandishi wa vitabu wa Korea Kusini watapata tabu kuwasimulia watoto watakaozaliwa 2050 juu ya jinsi gani Son alikuwa bora na alisumbua sana barani Ulaya lakini hadi anaachana na bara hilo kwenda Marekani alikuwa na taji moja tu. Son ambaye alihitajika na Man United, Chelsea na hata timu kubwa kule Hispania, hadithi yake inaenda kusomwa ndani ya kurasa zisizo na maandishi ya kuchekesha mengi.

Ilikuwa ni miaka 10 ya pata potea jijini London.