Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi za funga kazi AFCON 2025

AFCON Pict

Muktasari:

  • Diaz alifunga bao pekee lililowavushwa wenyeji wa michuano hiyo ya 35 tangu ilipoasisiwa mwaka 1957 wakati wakiichapa Tanzania katika mechi ambayo mwamuzi Boubou Traore akigeuka gumzo kwa kuinyima penalti ya wazi Stars baada ya Idd Seleman ‘Nado’ kuangushwa katika eneo la hatari na Morocco, lakini aliamua ‘kumeza’ filimbi.

RABAT, MOROCCO: WAKATI Brahim Diaz wa Morocco akiandika rekodi ya kufunga katika mechi nne mfululizo za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 jana na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kunyakua tuzo ya Mfungaji Bora wa michuano hiyo kwa msimu huu, leo katika hatua ya 16 Bora zinapigwa mechi za funga kazi.

Diaz alifunga bao pekee lililowavushwa wenyeji wa michuano hiyo ya 35 tangu ilipoasisiwa mwaka 1957 wakati wakiichapa Tanzania katika mechi ambayo mwamuzi Boubou Traore akigeuka gumzo kwa kuinyima penalti ya wazi Stars baada ya Idd Seleman ‘Nado’ kuangushwa katika eneo la hatari na Morocco, lakini aliamua ‘kumeza’ filimbi.

Bao hilo limemfanya Diaz kufikisha mabao manne akiongoza orodha wa wafungaji wa michuano hiyo (kabla ya mechi za jana), akifuatiwa na wachezaji wengine watatu wenye mabao matatu akiwamo Lassine Sinayoko wa Mali, Ayoub El Kaabi wa Morocco na Riyad Maharez wa Algeria ambaye atakuwa uwanjani usiku wa leo kukabiliana na DR Congo.

AFC 01

Kabla ya mechi mbili za jana jumla ya mabao 97 yalifungwa kupitia mechi 40 ikiwa ni maana ya wastani wa kila mechi kuzalisha mabao 2.42, huku Diaz akifunika kwa kufunga katika mechi nne mfululizo, zikiwamo tatu za makundi na hiyo ya juzi ya 16 Bora wakati Morocco ikitinga robo fainali na ikitarajiwa kuvaana na Cameroon.

Wakati hayo yakiwa hivyo, leo zinapigwa mechi mbili za kuhitimisha hatua ya 16 Bora ambapo mapema saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Moulay Hassan, mjini Rabat mabingwa wa mwaka 2019 Algeria wataumana na DR Congo, kabla ya saa 4:00 usiku kwenye Uwanja wa Marrakech watetezi Ivory Coast watamalizana na Burkina Faso.

Mechi hizo mbili zinatajwa kama ngumu zaidi katika hatua hiyo kutokana na vikosi na upinzani wa timu zinazovaana kwani kwa pambano la Algeria ya Riyad Mahrez na DR Congo litakuwa ni la sita kwa timu hizo tangu 1988, kwani zimeshakutana mara mbili katika hatua tofauti za fainali za AFCON na nyingine tatu za kirafiki.

AFC 02

Katika mechi hizo tano za awali ni mara mbili tu ndio zimetoa mshindi zote zikiwa ni Algeria ikiwamo ya kirafiki iliyopigwa Juni 9, 2022 na wababe hao kushinda kwa mabao 3-0, lakini ilishinda pia mechi ya makundi ya AFCON 1988 kwa bao 1-0 kuonyesha kuwa ni mechi ngumu kutabirika na itakayojipanga itapenya kwenda robo fainali.

Makocha wa timu zote, Sebastien Desabre wa DR Congo na Vladimir Petkovic wa Algeria kila mmoja amekiri hilo ni pambano gumu, lakini dakika 90 au 120 ndizo zitakazoamua kwa vile ni lazima mshindi apatikane kwenda robo.

Algeria itaendelea kumtegemea Mahrez, Ibrahim Maza na kipa Luca Zidane wakati DR Congo yenye straika wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele ina majembe ya maana akiwamo, Theo Bongonda, Gael Kakuta, Meschak Elia, Cedrick Bakambu na wengine kusaka robo fainali zitakazoanza kupigwa Ijumaa dhidi ya mshindi kati ya Nigeria au Msumbiji lililopigwa jana usiku.

Pambano jingine la mwisho la 16 Bora litapigwa saa 4:00 usiku likizikutanisha nchi majirani Ivory Coast na Burkina Faso ya Stephane Aziz KI.

AFC 03

Hili litakuwa ni pambano la 14 kwa timu hizo baada ya awali kukutana mara 13 katika michuano mbalimbali, huku rekodi zikiwabeba watetezi, Ivory Coast ambao wameshinda mara nane, huku wapinzani wakitakata mara mbili na mechi nyingine tatu zikiisha kwa sare.

Mara mbili za mwisho zilipokutana ilikuwa ni katika mechi za kuwania Fainali za CHAN 2024 ambapo kila moja ilishinda nyumbani kwa mabao 2-0 na kuamuliwa kwa penalti ambazo ziliibeba Burkina Faso, lakini kwa rekodi zilivyo ni wazi kina Aziz KI watakuwa na kazi kubwa kukabiliana na watetezi hao Tembo wa Ivory Coast.

Mshindi wa mechi hiyo ndiye atakayecheza na mshindi kati ya Misri na Benin iliyopigwa usiku wa jana katika pambano la Jumamosi, likiwa pia ni funga kazi ya mechi za robo fainali.