Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi tano za moto EPL 2026/27

Muktasari:

  • Baada ya ratiba kutoka, Opta imefanya tathmini kwa kuzingatia namba ikichambua ugumu wa mechi ikieleza ni timu gani zina mwanzo rahisi na zipi zenye ugumu zaidi mara tu msimu mpya utakapozinduliwa miezi miwili ijayo.

LONDON, ENGLAND: JUZI, ratiba ya Ligi Kuu England kwa msimu wa 2026-27 ilitangazwa ambapo mechji zinatarajiwa kuanza Agosti 22, mwaka huu, huku vita ya kuwania ubingwa ikianza kuonekana mapema hata kabla ya mchezo wa kwanza.

Baada ya ratiba kutoka, Opta imefanya tathmini kwa kuzingatia namba ikichambua ugumu wa mechi ikieleza ni timu gani zina mwanzo rahisi na zipi zenye ugumu zaidi mara tu msimu mpya utakapozinduliwa miezi miwili ijayo.

Mashabiki wa klabu tatu zilizopanda daraja ambazo ni Coventry City, Ipswich Town na Hull City wanaweza kuanza kutafakari itakuwaje.  Msimu wa 2026-27 utaanza kwa mchezo kati ya mabingwa wa Ligi Kuu England, Arsenal dhidi Coventry City waliobeba ubingwa wa Championship kwenye Uwanja wa Emirates. Itakumbukwa kwamba Coventry wamekuwa nje ya ligi hiyo kwa miaka 25, na huenda wakakutana na wakati mgumu kuikabili safu imara ya ushambuliaji na ile ya ulinzi ya Arsenal.

Arsenal waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wa ufunguzi wa msimu wa 2025-26 kabla ya kutwaa ubingwa baada ya miaka 22. Hiyo inaonyesha kuwa ni timu moja kati ya mabingwa 13 wa mwisho wa Ligi Kuu England waliopoteza mchezo wa kwanza wa msimu sawa na Man City 2021-22 walipofungwa 1-0 na Tottenham Hotspur.

Kuanza vizuri ni muhimu kuwa na msimu mzuri. Kwa timu zinazotarajiwa kupigania nafasi za chini, mwanzo mzuri au mbaya unaweza kuamua hatima ya msimu wao. Kwa ujumla timu 103 zimeshinda mechi mbili za kwanza za msimu wa ligi hiyo, lakini ni tatu tu kati yao ndizo zilizoshuka daraja msimu husika ambazo ni Wolves (2011-12), Hull (2016-17) na West Brom (2017-18).

Miongoni mwa mechi zinazovutia zaidi za wiki ya kwanza msimu ujao ni Hull City dhidi ya Manchester United itakayopigwa Jumamosi, Agosti 22, kabla ya mchezo wa mwisho wa Jumapili ambapo Newcastle United watakuwa wenyeji wa Liverpool katika mchezo utakaokuwa wa kwanza rasmi kwa Andoni Iraola akiwa kocha mkuu wa Liverpool.

Kwa kutumia mfumo wa Opta inawezekana kupima ugumu wa ratiba za kila timu, ambapo mfumo huo hupima takribani timu 10,000 duniani, ukitoa alama kuanzia 100 kwa timu bora hadi 0 kwa dhaifu zaidi. Timu za EPL zimepangwa kulingana na wastani wa nguvu za wapinzani wao nahii inaanzia Arsenal (namba 1 duniani ikiwa na alama 100 na ndiyo timu ngumu zaidi kucheza nayo) hadi Hull City (nafasi ya 164 duniani kwa alama 82.2 ikiwa ni rahisi zaidi kucheza nayo).


TANO ZA MWANZO

Timu yenye ratiba nafuu zaidi katika mechi tano za mwanzo ni Manchester United (ikiwa na wastani wa alama za ubora wa wapinzani wa 89.3). Kwa mara ya kwanza tangu 2016/17, Mashetani Wekundu wataanza msimu kwa mchezo wa ugenini, lakini angalau ni dhidi ya Hull City, timu iliyoorodheshwa chini zaidi katika ligi. Kikosi hicho cha Michael Carrick kisha kitaikaribisha Ipswich Town, timu nyingine iliyopanda daraja, kabla ya kusafiri kwenda Everton.

Baada ya hapo kutakuwa na dabi ya Manchester, kisha safari ya kwenda Fulham. Hivyo basi, siyo mwanzo ambao unaweza kuitwa rahisi kabisa, lakini Carrick amepewa nafasi nzuri ya kuendeleza kasi ambayo United walimalizia nayo msimu wa 2025/26 baada ya kuthibitishwa rasmi kuwa kocha mkuu wa kudumu.

Newcastle United na Liverpool zitakutana katika Uwanja wa St. James’ Park mwishoni mwa wiki ya ufunguzi wa msimu, ambapo Alexander Isak na mchezaji mpya wa Liverpool, Victor Munoz ambaye awali alionekana kuelekea Newcastle United wanaweza kupata mapokezi ya kipekee kutoka kwa mashabiki. Hata hivyo, baada ya mchezo huo, timu zote mbili zinaonekana kuwa na ratiba nafuu zaidi kuliko nyingi nyinginezo.

Kikosi cha Eddie Howe pia kitacheza nyumbani dhidi ya Bournemouth na Hull katika mechi zake tano za kwanza, huku kikisafiri kucheza dhidi ya Tottenham Hotspur na Leeds United.

Nao mchezo wa kwanza wa nyumbani wa Andoni Iraola akiwa kocha wa Liverpool utakuwa dhidi ya Nottingham Forest, kabla ya kukutana na Ipswich (ugenini), Fulham (nyumbani) na Bournemouth (ugenini).

Kwa upande wa ugumu wa ratiba, Arsenal na Manchester City zinaonekana kuwa na mwanzo unaofanana katika mechi tano za kwanza, kila moja ikikabiliana na wapinzani wenye wastani wa alama 90.9. Mabingwa watetezi Arsenal wataanza kwa kuikaribisha Coventry, kisha kusafiri kucheza na Aston Villa katika mchezo mgumu, kabla ya kukutana na Chelsea (nyumbani), Sunderland (ugenini) na Brighton (ugenini).

Mrithi wa Pep Guardiola, Enzo Maresca, ataanza maisha yake Manchester City kwa mchezo wa nyumbani dhidi ya Bournemouth ya Marco Rose, kabla ya kukutana na Crystal Palace (ugenini), Coventry (nyumbani), Manchester United (ugenini) na Sunderland (nyumbani).

Kuhusu ratiba ngumu zaidi katika mechi tano za kwanza inaonekana kuisubiri Bournemouth, ingawa mechi tatu kati ya tano za kwanza zitachezwa nyumbani. Kama ilivyotajwa, itaanza kwa kuifuata Manchester City kabla ya kucheza dhidi ya Everton (nyumbani), Newcastle (ugenini), Brentford (nyumbani) na hatimaye Liverpool katika Uwanja wa Vitality.

Sunderland pia wana mwanzo mgumu, wakikabiliana na Arsenal na Manchester City, huku Coventry wakionekana kurejea Ligi Kuu England wakianzia ugenini dhidi ya Arsenal, timu iliyo juu zaidi kwenye viwango vya ubora wa ligi kabla ya kuikaribisha Hull, timu ya mwisho kwenye viwango hivyo, na kisha kusafiri kwenda Manchester City, timu ya pili kwa ubora.

Hull (92.1) na Ipswich (91.7) hawana ratiba ngumu sana kama Coventry katika mechi tano za kwanza, lakini bado wanakabiliwa na ratiba iliyo katika nusu ngumu ya ligi. Hali hiyo pia inawakabili Tottenham (92.2).

Xabi Alonso amepewa ratiba ambayo inaweza kuitwa ya wastani, huku Chelsea wakionekana kuwa na ratiba ya 10 kwa ugumu katika mechi tano za kwanza. Wataanza kwa dabi ya Magharibi mwa London dhidi ya Fulham. Chelsea pia watasafiri kwenda Arsenal katika mchezo wa tatu wa msimu, ambao utakuwa mtihani mgumu.

Nao Aston Villa watakutana na Arsenal kabla ya hapo katika wiki ya pili ya msimu, na wao pia wana ratiba mchanganyiko katika mechi tano za mwanzo, huku wakianza kwa kuifuata Brighton, kisha Hull City na Tottenham.