Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matajiri Saudia kumrudisha Klopp kazini

KLOPPA Pict

Muktasari:

  • Klopp alitangaza kuachana na Liverpool, mwisho wa msimu wa  2023/24, katika taarifa ambayo ilishtua mashabiki wengi wa soka na akasisitiza hawezi tena kufanya kazi hiyo kwa sasa.

LIVERPOOL, HISPANIA: KOCHA wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp anadaiwa kuwa katika mazungumzo na Al-Ittihad ya Saudi Arabia ambayo inatafuta kocha kwa sasa.

Klopp alitangaza kuachana na Liverpool, mwisho wa msimu wa  2023/24, katika taarifa ambayo ilishtua mashabiki wengi wa soka na akasisitiza hawezi tena kufanya kazi hiyo kwa sasa.

Akiwa katika viunga vya Anfield, Klopp aliiongoza Liverpool kushinda mataji makubwa kama Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa ya Ulaya na Kombe la Klabu bingwa  Dunia la FIFA.

Baada ya kuondoka Liverpool, Klopp alijiunga na kampuni  Red Bull kama Mkuu wa masuala ya  Soka Ulimwenguni (Head of Global Soccer).

Tangu wakati huo amekuwa akihusishwa na timu mbalimbali na sasa, Klopp, 58, anahusishwa na  Al Ittihad ambayo inataka akachukue nafasi ya  Laurent Blanc aliyefutwa kazi, baada ya kipigo cha 2-0 dhidi ya Al Nassr ya Cristiano Ronaldo.

KLO 01
KLO 01

Mbali ya Klopp, inaelezwa timu hii pia ilihitaji huduma ya Xavi Hernandez lakini alikataa kwani bado anahitaji kufundisha timu za Ulaya na kujenga zaidi CV yake.

Aprili mwaka huu baada ya Klopp kuhusishwa sana na ajira ya kwenda kuifundisha timu ya taifa ya Brazil, wakala wake, Mark Kosicke, alitangaza Mjerumani huyo anafurahia sana kazi yake katika kampuni ya Red Bull.

Mwandishi wa Sky Sports Germany, Florian Plettenburg aliandika: “Kuna uvumi mpya unaomhusisha Jurgen Klopp na Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya Brazil. Ukweli ni wakala wake, Marc Kosicke, aliniambia Jurgen ana furaha sana na nafasi yake  kama Mkuu wa Soka Ulimwenguni katika kampuni ya Red Bull.”

KLO 02

“Klopp bado hana mpango wa kuchukua nafasi ya kocha mkuu msimu ujao hata zikija timu nyingine tofauti ya Real Madrid au Brazil.”

 Mei mwaka huu, Klopp pia alihusishwa na kuhamia AS Roma, taarifa ambazo zilikanushwa na wakala wake.

Akiwa Qatar, Kosicke aliviambia vyombo vya habari nchini humo kwamba: “Ripoti kuhusu Klopp kuwa kocha mpya wa AS Roma si kweli.”