Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki walia paa kuvuja Old Trafford

MARTIN 03

Muktasari:

  • Mvua kubwa ilinyesha wakati Man United ilipokuwa ikiichakaza Ipswich Town kwa mabao 5-2 katika mchezo wa Ligi Kuu England, huku maji yakianza kuingia ndani ya uwanja kupitia paa.

MANCHESTER, ENGLAND: SHABIKI wa Manchester United wamebaki vinywa wazi baada ya kugundua kuwa klabu hiyo bado haijatatua tatizo la paa linalovuja kwenye Uwanja wa Old Trafford.


Mvua kubwa ilinyesha wakati Man United ilipokuwa ikiichakaza Ipswich Town kwa mabao 5-2 katika mchezo wa Ligi Kuu England, huku maji yakianza kuingia ndani ya uwanja kupitia paa.

Licha ya United kutumia zaidi ya Pauni150milioni katika usajili wa wachezaji wapya msimu huu, inaonekana hakuna fedha za kutosha zilizotengwa kukarabati paa la uwanja huo wenye umri wa miaka 116.

United ilitumia Pauni70 milioni kumsajili Carlos Baleba, Pauni50 milioni kwa Andrey Santos na Pauni53 milioni kwa Youri Tielemans.

KUVU 01

Tatizo hilo lilionekana wazi baada ya maji kuanza kumwagika kama maporomoko kutoka kwenye paa upande wa Stretford End wakati wa ushindi dhidi ya Ipswich.

Maji yalionekana yakitoka kwenye paa na kutiririka kuelekea chini ya uwanja, huku video nyingine zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha maeneo mengine ya Old Trafford yakivuja na maji kudondokea sehemu za kukaa mashabiki.

Mashabiki walishangazwa kuona tatizo hilo likiendelea licha ya klabu kupata muda wa kulifanyia kazi wakati wa mapumziko ya msimu.

Shabiki mmoja aliandika: "Paa la Old Trafford bado linavuja mwaka 2026. Kocha wapya, usajili wapya, lakini maporomoko ya maji ni yale yale."

Mwingine amesema: "Manchester United imetumia Pauni milioni 150 msimu huu, lakini paa la Old Trafford bado linavuja."

KUVU 02

Shabiki mwingine aliandika kwa kifupi: "Maporomoko ya maji ya Old Trafford yameonekana tena."

Mwingine amesema: "Ni mwaka 2026 na Old Trafford bado inavuja kila mvua inaponyesha."

Shabiki mwingine akaongeza: "Sasa mmeona kwa nini tunataka kujenga uwanja mwingine."

Tatizo la paa limejitokeza wakati United pia imekuwa ikitumia fedha kuboresha maeneo mengine ya Old Trafford, ikiwemo kupanua eneo la huduma maalumu kwa wageni na kubadilisha nyasi za uwanja huo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 14.