Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanachokifanya Haji Mnoga na wenzake

UGHAIBUNI Pict

Muktasari:

  • Baada ya kumaliza msimu uliopita wakiwa na mchango katika timu zao, nyota hao wam eendelea kuo nyesha dalili nzuri, mwanzo wa msimu mpya, jambo linaloweza kuwapa nafasi zaidi ya kuendelea kuwa sehemu ya mipango ya Taifa Stars.

HAWA ni baadhi ya wachezaji wenye asili ya Tanzania ambao wamekuwa wakiitwa mara kwa mara kwenye kikosi cha Taifa Stars, na wameanza msimu wa 2026/27 vizuri katika klabu zao mpya.

Baada ya kumaliza msimu uliopita wakiwa na mchango katika timu zao, nyota hao wam eendelea kuo nyesha dalili nzuri, mwanzo wa msimu mpya, jambo linaloweza kuwapa nafasi zaidi ya kuendelea kuwa sehemu ya mipango ya Taifa Stars.

UGHA 03

HAJI MNOGA – PATRO EISDEN

Beki wa kulia, Haji Mnoga ameanza maisha mpya wa maisha ya Patro Eisden ya Ubelgiji baada ya kuachana na Salford City.

Msimu uliopita akiwa Salford City, Mnoga alicheza mechi 32 katika mashindano yote, kwa dakika 2,268 akiwa sehemu ya kikosi kilichoipeleka timu hiyo hatua ya play-off za kupanda daraja. Sasa akiwa Patro Eisden, Mnoga ameanza msimu wa 2026/27 akiwa tayari ameingia kwenye kikosi cha kwanza. Alianza dhidi ya Anderlecht U-23, mechi ambayo Patro Eisden ilishinda 2-1, kabla ya kucheza dakika zote 90 dhidi ya Lierse kwenye mchezo uliofuata.

Katika mchezo huo wa Lierse, Patro Eisden ilipoteza 2-1, lakini Mnoga alimaliza dakika zote 90. Rekodi hizo zinaonyesha kuwa bado yupo kwenye mipango ya kocha na anaendelea kupata muda wa kucheza tangu kuhamia Ubelgiji.

UGHA 02

TARRYN ALLARAKHIA – BOREHAM WOOD

Winga huyo ambaye msimu uliopita alikuwa na kikosi cha Rochdale ya ligi daraja la nne England, aliisaidia chama hilo kuipandisha daraja hadi ligi daraja la tatu. Msimu uliopita akiwa Rochdale, Allarakhia alicheza mechi 55 za ligi na kufunga mabao sita, licha ya kucheza zaidi kama kiungo wa pembeni, ana uwezo wa pia kuhusika katika kutengeneza na kufunga mabao.

Mwanzo wake wa 2026/27 unaonyesha bado anapewa nafasi na kocha Luke Garrard. Katika Ligi ya National League amecheza dhidi ya Tamworth, Halifax Town, Forest Green na Boston United.

Mchango wake mkubwa umeonekana pia kwenye National League Cup ambako alifunga bao katika ushindi wa 5-2 dhidi ya Leeds United U-21 Agosti 18.


UGHA 01

CHARLES M’MOMBWA – ZABBAR

Usajili wa M’Mombwa kwenda Zabbar msimu huu ulikuwa na changamoto baada ya chama lake la zamani Floriana inayoshiriki Ligi Kuu ya Malta kudai kuwa bado ni mchezaji wao halali.

Msimu uliopita ulikuwa muhimu kwake kwani alikuwa sehemu ya kikosi cha Floriana kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Malta. Takwimu zinaonyesha M’Mombwa alicheza mechi 27 za ligi, kwa dakika 2,022 na kufunga mabao mawili. Pia alicheza mechi nne za UEFA Conference League na kufunga bao moja.

Licha ya changamoto hiyo msimu huu akiwa Zabbar, M’Mombwa ameanza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza. Amecheza dakika 90 dhidi ya Valletta, dakika 79 dhidi ya Birzebbuga na dakika 76 dhidi ya Hibernians. Katika mchezo wa mwisho dhidi ya Hibernians, uliomalizika kwa sare ya 1-1, alicheza zaidi ya saa moja na kuendelea kuonyesha umuhimu wake katika eneo la kiungo.