Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki wa Ronaldo wavamia harusi

RONAL 03

Muktasari:

  • Tukio hilo lilitokea jana baada ya uvumi kusambaa kwa kasi kwamba Ronaldo, 41, na Georgina, 32, walikuwa wamepanga kufunga ndoa katika kanisa hilo la kihistoria.

LISBON, URENO: WATU takribani 2,000 walijazana nje ya Kanisa Kuu la Funchal, Madeira, wakiamini kuwa nyota wa soka Cristiano Ronaldo alikuwa akifunga ndoa na mchumba wake Georgina Rodríguez, lakini wakajikuta wamekosea baada ya kugundua kuwa harusi hiyo ilikuwa ya wanandoa wengine.

Tukio hilo lilitokea jana baada ya uvumi kusambaa kwa kasi kwamba Ronaldo, 41, na Georgina, 32, walikuwa wamepanga kufunga ndoa katika kanisa hilo la kihistoria.

Badala yake, harusi hiyo ilikuwa ya raia wa Ureno, Fabio Ramos na Fatima Nicole Cunha Teixeira, ambao wote wanatokea Madeira, lakini wanaishi nchini Ufaransa.

Licha ya ukweli huo, mashabiki waliendelea kuamini kuwa Ronaldo alikuwa ameficha utambulisho wake na kwamba kanisa hilo la karne ya 15 lilikuwa limehifadhiwa kwa ajili ya harusi yake na Georgina.

Fatima alijikuta akipita kwa tabu katikati ya umati wa watu waliokuwa wakimkodolea macho na kumpiga picha, huku baadhi yao wakiwa wamevaa jezi maarufu namba saba ya Ronaldo.

RONALDO Pict

Wakati bibi harusi akielekea ndani ya kanisa, baadhi ya wageni walilazimika kuwaambia mashabiki waliokuwa nje: "Huyu si Georgina!"

Video za vurugu hizo zilisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na hata kufika kwenye akaunti ya Ronaldo, ambaye alijibu kwa kuweka emoji kadhaa za kucheka.

Mmoja wa wageni amesema hali hiyo ilikuwa ya kushangaza huku akieleza kuwa bibi harusi alianza kuwa na hofu kwamba vurugu hizo zingeharibu siku yake muhimu.

RONAL 04

Dada Ronaldo aongeza sintofahamu

Wakati uvumi wa harusi ukionekana kufifia, dada yake Ronaldo, Katia Aveiro, ameongeza sintofahamu baada ya kuweka video akionyesha akitua Madeira kwa kile alichokiita "sherehe".

Katika picha na video hizo alionekana pia akisalimiana na mama yao, Maria Dolores, katika chumba kilichoonekana kuwa cha hoteli.

Hali hiyo iliwafanya mashabiki kuamini huenda Ronaldo na Georgina bado walikuwa na mpango wa kufunga ndoa katika kisiwa hicho.

Zaidi ya hapo, wafanyakazi wa hoteli ya kifahari ya Savoy Palace walidai kuwa walipewa taarifa kwamba Ronaldo alikuwa amehifadhi ghorofa mbili za juu katika eneo maalumu la hoteli hiyo linalojulikana kama "The Reserve".

RONAL 02

Padri avunja uvumi

Hata hivyo, Padre Marcos Goncalves, anayesimamia Kanisa Kuu la Funchal, alikanusha taarifa hizo na kuweka wazi kuwa harusi iliyofanyika siku hiyo haikuwa ya Ronaldo.

"Hii ndiyo harusi pekee inayofanyika hapa leo. Sina nafasi iliyowekwa kwa ajili ya Cristiano Ronaldo," amesema padre huyo.

Ameongeza kuwa hakuamini Ronaldo alikuwa amepanga kufunga ndoa katika kanisa hilo hivi karibuni.

Mashabiki kadhaa waliokuwa wamevaa jezi namba saba walijaza eneo la nje ya kanisa hilo, wakiwa na matumaini ya kumuona staa huyo akifunga ndoa na Georgina.

RONAL 01

Uvumi wa harusi wavurugwa

Ronaldo na Georgina walichumbiana Agosti mwaka jana, huku Ronaldo akiwa amewahi kusema kuwa angefunga ndoa "baada ya Kombe la Dunia."

Hata hivyo, taarifa zilizokuwa zikidai kuwa wawili hao wangefunga ndoa Agosti 1 katika jumba la kihistoria la Quinta da Regaleira mjini Sintra, Ureno, zilikanushwa.

Uvumi huo ulianza baada ya mwaliko bandia wa harusi kusambaa kwenye televisheni za Ureno.

Jarida la HOLA! lilikuwa miongoni mwa vyombo vilivyopinga taarifa hizo, likieleza kuwa eneo hilo liliendelea kuwa wazi kwa watalii katika tarehe iliyodaiwa kuwa ya harusi.

Ronaldo na Georgina walikutana wakati Georgina alipokuwa akifanya kazi kama muuzaji katika duka la Gucci mjini Madrid, kabla ya uhusiano wao kukua na kufikia hatua ya uchumba.

Kwa sasa Ronaldo anajiandaa kurejea Saudi Arabia kujiunga na kikosi cha Al-Nassr kwa maandalizi ya msimu mpya, huku hatma ya tarehe halisi ya harusi yake na Georgina ikiendelea kuwa siri.