Mashabiki England wamvuruga Thomas Tuchel
Muktasari:
- Three Lions ilipata mabao matatu ndani ya dakika 20 dhidi ya Wales ambayo inajiandaa na mechi muhimu ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Ubelgiji, nyumbani.
Kocha Thomas Tuchel alionekana kuwa mwenye hasira licha ya England kupata ushindi mzuri dhidi ya Wales katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyofanyika nyumbani kwao jana Alhamisi, Oktoba 09, 2025.
Three Lions ilipata mabao matatu ndani ya dakika 20 dhidi ya Wales ambayo inajiandaa na mechi muhimu ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Ubelgiji, nyumbani.
Ulikuwa ni wakati wa kushangaza kwa kocha wa Wales, Craig Bellamy kuchagua mpinzani mkali dhidi ya kikosi chake, na England ilionyesha kutoa upinzani kweli. Kikosi cha Wales kilijitahidi kuimarisha ulinzi na kuepuka kupokea mabao zaidi baada ya la tatu, lakini kilionekana hakikuwa katika kiwango chao bora.
Morgan Rogers, Ollie Watkins na Bukayo Saka walifunga mabao, na baada ya mechi, Tuchel ameongea kuhusu kuchanganyikiwa kwake kwamba mashabiki wa England waliokuwepo Wembley hawakumuunga mkono, hasa baada ya nyota wa Arsenal, Saka, kufunga bao la tatu.
“Uwanja ulikuwa kimya,” amesema.
“Hatujawahi kupata nguvu yoyote kutoka kwa mashabiki. Ndiyo, nilikuwa natarajia zaidi kutoka Wembley jana usiku. Ukisikiliza tu mashabiki wa Wales… ni huzuni kidogo. Timu ilikuwa inastahili sapoti kubwa.”
Kocha huyo Mjerumani ameulizwa kama alitarajia ushirikiano zaidi wa mashabiki kutoka Wembley, amejibu: “Ndiyo. Unaweza kutoa nini zaidi ndani ya dakika 20? Hatukutia nafasi yoyote ya kuikimbia timu. Ukisikiliza tu mashabiki wa Wales kwa nusu saa, ni huzuni kwa sababu timu ilistahili sapoti zaidi.
“Ninasimama nyuma ya kauli hii. Hatuwezi kufanya zaidi kuliko kuwa na mabao 3-0 katika mchezo wa dabi. Ningeomba sapoti zaidi katika vipindi ambapo ilikuwa vigumu. Katika nusu ya pili kutuunga mkono, kulikuwa na sapoti kutoka kwa mashabiki wa Wales. Ingekuwa msaada kwetu kupata nguvu tena, lakini ni jinsi ilivyo.”
Mashabiki wa Wales walikuwa na sauti kubwa hata baada ya mechi licha ya kuona timu yao ikicheza vibaya.