Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Martinez: Kidole hakitarudi kama zamani!

MARTINEZ Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 alivunjika na kuteguka kidole wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa fainali ya Europa League, ambapo Aston Villa iliibuka na ushindi dhidi ya Freiburg mwezi Mei.

LONDON, ENGLAND: KIPA wa Argentina na Aston Villa, Emiliano Martinez amefichua kuwa kidole chake kilichovunjika na kutoka sehemu yake ya kawaida hakitawahi kurejea katika hali yake ya awali, licha ya kuendelea kucheza soka akiwa na maumivu makali.

Martinez, ambaye alijitolea kucheza akiwa majeruhi ili kuisaidia Argentina katika harakati za kutetea ubingwa wa Kombe la Dunia, amesema alikumbana na wakati mgumu baada ya kupata taarifa za vipimo vilivyoonyesha ukubwa wa jeraha hilo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 alivunjika na kuteguka kidole wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa fainali ya Europa League, ambapo Aston Villa iliibuka na ushindi dhidi ya Freiburg mwezi Mei.

MAR 01

Akizungumza kupitia chaneli ya YouTube ya mwandishi wa habari wa Argentina, Gaston Edul, Martinez amesema alitokwa na machozi baada ya kuona majibu ya vipimo vya X-ray, akihofia jeraha hilo lingemfanya akose nafasi ya kuichezea Argentina katika mashindano hayo makubwa.

Hata hivyo, baada ya kupata msaada na ushauri kutoka kwa kocha wa Argentina, Lionel Scaloni, iliamuliwa kuepuka upasuaji ambao ungeweza kumuweka nje ya michuano hiyo.

Badala yake, Martinez alipewa glavu maalumu zilizotengenezwa na kampuni ya Adidas kwa ajili ya kulinda kidole chake kilichoumia. Hata hivyo, alikiri kuwa glavu hizo zilimfanya ashindwe kuushika mpira kwa ufanisi kama kawaida.

MAR 02

“Kidole changu hakitarudi tena katika hali yake ya zamani. Hadi sasa bado nacheza nikiwa na maumivu,” amesema Martinez.

Ameongeza: “Siku moja kabla ya mchezo dhidi ya Algeria nilikuwa najirusha kuokoa mipira kwa kutumia mkono mmoja, nilikuwa naruka kama zombie.

“Kila nilipoweka mkono chini niliona kama nyota zinacheza mbele ya macho yangu. Ilikuwa hali mbaya sana. Kila usiku nilikuwa nikilia kwa sababu kidole changu kilikuwa kimevimba kama soseji.

“Lakini hizo ndizo hatari unazokubali unapoitumikia timu ya taifa. Ningeamua hivyo tena bila kusita.”

Martinez pia amefichua kuwa jeraha hilo lilichangia kuvunjika kwa mpango wake wa kuhamia Italia katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi, huku Juventus ikitajwa kuwa miongoni mwa klabu zilizokuwa zikimuwania.

Amesema baada ya kufanyiwa vipimo vingine vya X-ray, ilibainika kuwa kidole hicho kilikuwa kimevunjika tena, hali iliyosababisha klabu iliyokuwa ikimhitaji kubadili msimamo wake kuhusu usajili wake.

MAR 03

“Nilipofanyiwa X-ray, ilionyesha kuwa kidole kilikuwa kimevunjika tena. Hapo ndipo dili la kujiunga na klabu moja lilipokwama kutokana na tatizo hilo,” amesema.

Alifafanua kuwa alielezwa angeweza kuendelea kucheza katika hali hiyo, lakini angehitaji kufanyiwa upasuaji wakati fulani.

Kwa sasa, Martinez anaendelea na matibabu baada ya kupata jeraha jingine la kuvunjika taya katika ushindi wa Chelsea dhidi ya Everton mapema mwezi huu.