Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AC Milan VS Inter Milan; Dabi Madonnina ni hisia kotekote

MILAN Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, wakati Lazio, Roma na Inter zote zilipata pointi tatu, ingawa ushindi wa Inter haukuambatana na kiwango cha kuridhisha, Milan ilipoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kwa mabao 4-2 nyumbani dhidi ya Bologna.

MILAN, ITALIA: WAPINZANI wa wa jadi wa Dabi ya Italia maarufu Derby della Madonnina, AC Milan na Inter Milan waliingia katika michezo ya katikati ya wiki ya Ligi Kuu Italia (Serie A) wakiwa miongoni mwa timu nne ambazo hazikuwa zimepoteza mchezo wowote katika ligi hiyo msimu huu.

Hata hivyo, wakati Lazio, Roma na Inter zote zilipata pointi tatu, ingawa ushindi wa Inter haukuambatana na kiwango cha kuridhisha, Milan ilipoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kwa mabao 4-2 nyumbani dhidi ya Bologna.

Hat-trick ya Samuel Mbangula iliihukumu Rossoneri kupata kipigo, huku akiwa mchezaji wa pili pekee kufunga hat-trick ya ugenini dhidi ya Milan katika Serie A baada ya Gabriel Batistuta kufanya hivyo akiwa Fiorentina, Septemba 1998. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Milan kufungwa mabao manne katika mchezo wa Serie A nyumbani tangu Januari 2023, ilipofungwa mabao 5-2 na Sassuolo.

Kocha Ruben Amorim alisema baada ya mchezo huo kuwa timu yake “ilionekana kuchoka tangu dakika ya kwanza”, huku mfululizo wa majeruhi, hasa katika eneo la kiungo ukipunguza machaguo ya wachezaji. Hata hivyo, AC MIlan maarufu pia kama Rossoneri italazimika kutafuta mbinu mpya, leo Jumamosi, inapokutana na wapinzani wake wa jadi Inter Milan ikiwa mwenyeji wa mchezo huo.


MILA 06

SHIDA ILIANZIA HAPA

Kipigo cha Jumatano kilikuwa cha tano kwa AC Milan katika michezo ya nyumbani ya Serie A tangu kuanza kwa mwaka 2026. Ni mara ya tano pekee katika miaka 50 iliyopita kwa Milan kufikia idadi hiyo ya vipigo vya nyumbani ndani ya mwaka mmoja wa kalenda, baada ya kufanya hivyo  1997 (vipigo vitano), 2012 (sita), 2017 (saba) na 2021 (saba). Timu zote mbili zitakuwa zikicheza katika uwanja wao wa nyumbani, San Siro.

Taarifa zinaeleza kuwa Milan inatarajia kuwapata Mario Gila na Diego Moreira kutoka katika majeraha kabla ya mchezo huo. Hata hivyo, Adrien Rabiot, Ruben Loftus-Cheek, Samuel Chukwueze, Matteo Gabbia na Alexis Saelemaekers hawatarajiwi kurejea.

Kwa AC Milan imeendelea kupungukiwa na wachezaji itamhitaji Alphadjo Cisse kuendeleza kiwango chake bora baada ya kufunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza dhidi ya Bologna.

MILA 02

Akiwa na umri wa miaka 20 na siku sita, mabao yake mawili yaliyomfikisha kwenye jumla ya mabao manne ya Serie A msimu huu yalimfanya kuwa mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Milan kufunga zaidi ya mabao mawili katika mashindano hayo tangu 1994-95.

Ni Alexandre Pato (akiwa na miaka 18 na siku 147 Januari 27, 2008) na Stephan El Shaarawy (akiwa na miaka 19 na siku 332 Septemba 23, 2012) pekee waliofanya hivyo wakiwa na umri mdogo zaidi.

MILA 04

Cisse pia ni mmoja wa wachezaji watatu pekee waliofunga angalau mabao mawili katika mchezo mmoja wa Serie A na mashindano makubwa ya UEFA msimu huu, pamoja na Donyell Malen na Lautaro Martínez.

Inter Milan nayo kwa upande wake ilihitaji mabao ya kujifunga ya dakika za mwisho kutoka kwa wachezaji wa Venezia, Matias Moreno na Redouane Halhal, ili kupata ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa Stadio Pier Luigi Penzo.

Kocha Cristian Chivu hakufurahishwa na kiwango cha timu yake, akisema baada ya mchezo kuwa alitamani angeweza kuwabadilisha wachezaji wote. Hata hivyo, pointi 25 za Inter baada ya michezo tisa ni rekodi mpya ya klabu hiyo katika hatua hii ya msimu tangu 1994-95. Huu ni mwanzo bora wa msimu wa Serie A kwa Inter, ikilinganishwa na misimu ya 1966-67 na 1988-89.

MILA 03

Hakan Calhanoglu, Manuel Akanji, Nicolo Barella, Francesco Pio Esposito na Henrikh Mkhitaryan wote walianza mchezo huo wakiwa benchi.

Wachezaji watatu walio majeruhi, Curtis Jones, John Stones na Benjamin Pavard, wanaendelea kupata nafuu. Hata hivyo, Inter huenda ikakosa tena huduma ya mshambuliaji wake muhimu, Lautaro Martinez, baada ya kupata tatizo la misuli ya nyuma ya paja wakati wa mchezo wa hivi karibuni wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Club Brugge.

Mshambuliaji huyo wa Argentina amefunga mabao tisa katika michezo 21 ya Derby della Madonnina, huku pia akitoa asisti tatu. Amecheza dhidi ya Milan mara nyingi zaidi kuliko klabu nyingine yoyote akiwa mchezaji wa Inter, huku akiwa amehusika katika mabao mengi zaidi dhidi ya Cagliari (13, mabao 12 na pasi moja ya bao).

Kutokuwepo kwake ni pigo kubwa kwa Nerazzurri, lakini wana mshambuliaji mwingine aliye katika kiwango kizuri sana, Marcus Thuram aliyehusika katika angalau bao moja katika michezo 12 kati ya 14 ya Serie A aliyocheza tangu ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Roma Aprili 5, akifunga mabao 11 na asisti tano. Ni Donyel Malen wa Roma pekee aliyefanya vizuri zaidi katika kipindi hicho akiwa na mabao 14 na asisti tatu.


MILA 05

HISTORIA YA KUKUTANA

Licha ya Inter kuwa na mafanikio makubwa zaidi katika Serie A, baada ya kumaliza juu ya Milan katika misimu minane kati ya tisa iliyopita, isipokuwa 2021-22 ambao Rossoneri ilitwaa ubingwa wa Scudetto, rekodi yao ya hivi karibuni katika dabi haijawa nzuri.

Inter haijashinda mchezo wowote kati ya saba iliyopita dhidi ya Milan katika mashindano yote, ikiwa na sare mbili na vipigo vitano. Hiyo ni rekodi mbaya zaidi dhidi ya wapinzani wao tangu kupoteza michezo 10 mfululizo bila ushindi katika mashindano yote kati ya Novemba 2002 na Aprili 2005.

Mbali na vipigo vitatu katika michezo minne ya mwisho ya Serie A dhidi ya Milan, huku mchezo mmoja ukiisha kwa sare, mfululizo huo mbaya wa Inter unajumuisha pia kipigo katika fainali ya Supercopa Italiana Januari 2025 na kuondolewa kwa jumla ya mabao katika nusu fainali ya Coppa Italia msimu huohuo.

Milan ilishinda kwa bao 1-0 katika michezo yote miwili ya ligi dhidi ya Inter msimu wa 2025-26.

Hilo lilimfanya Chivu kuwa kocha wa tatu wa Inter kupoteza michezo yake miwili ya kwanza dhidi ya Milan katika mashindano yote, baada ya Giuseppe Meazza 1947 na Giuseppe Chiappella kati ya 1975 na 1976.


MILA 01

SA’ ITAKUWAJE?

Pamoja na hayo yote Inter, kimsingi, inapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo kwa asilimia 46.9, huku Milan ikiwa na 28.2 ilhali asilimia 24.9 utaisha kwa sare. Vilevile Inter inapewa nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wa Serie A msimu wa 2026-27 kwa asilimia 54.4, ilhali Milan ina 3.3, Roma (15.6), Como (12.8) na Lazio (11.8) zinaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuwa wapinzani wa Inter katika mbio za ubingwa.