Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Acha inyeshe tuone panapovuja

CHAMPIONSHIP Pict

Muktasari:

  • Mechi za jana ilikuwa kati ya Songea United iliyotoka kuchapwa mabao 2-0, dhidi ya Bandari Tanzania ikicheza na Transit Camp kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini, Morogoro, huku ikitoka pia kufungwa na maafande wenzao wa Tanzania Prisons mabao 2-1.

UTAMU wa Ligi ya Championship unaendelea kushika kasi na baada ya jana Ijumaa kuchezwa mechi tatu za raundi ya nane, ila nyingine tatu pia zitapigwa leo Jumamosi, huku zingine mbili kali zikichezwa kesho Jumapili, kwenye viwanja mbalimbali.

Mechi za jana ilikuwa kati ya Songea United iliyotoka kuchapwa mabao 2-0, dhidi ya Bandari Tanzania ikicheza na Transit Camp kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini, Morogoro, huku ikitoka pia kufungwa na maafande wenzao wa Tanzania Prisons mabao 2-1.

Vinara wa Ligi hiyo KMC yenye pointi 15, baada ya wiki iliyopita kulazimishwa suluhu (0-0), dhidi ya IAA SC ya jijini, Arusha, iliikaribisha Stand United ‘Chama la Wana’ kutoka Shinyanga, iliyotoka kuchapwa na Bigman FC ya Tanga mabao 3-2.

Rhino Rangers iliyotoka kuichapa Mbuni FC ya Arusha bao 1-0, ilikuwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini, Tabora kucheza na Gunners FC ya jijini, Dodoma, ikiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu (0-0), dhidi ya TMA FC ya mkoani Iringa.

CHAMP 01

Leo Jumamosi, Mbuni FC iliyochapwa bao 1-0, dhidi ya Rhino Rangers itakuwa kwenye Uwanja wa Aga Khan, jijini, Arusha, kucheza na KenGold FC kutoka jijini, Mbeya, ambayo mechi ya mwisho ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar.

Katika mechi saba iliyocheza Mbuni FC hadi sasa msimu huu, imeshinda moja, sare mbili na kupoteza minne, ikiwa nafasi ya 13 na pointi tano, huku KenGold inayoshika nafasi ya 10 na pointi nane, ikishinda miwili, sare mbili na kupoteza mitatu.

Mbuni FC haina balansi nzuri katika eneo la kujilinda na ushambuliaji, kwani hadi sasa imefunga mabao sita na kuruhusu 12, huku kwa upande wa timu ya KenGold, safu ya kushambulia imefunga mabao manane na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 10.

CHAMP 02

Kwenye Uwanja wa Manungu Complex, mjini, Morogoro, wenyeji Mtibwa Sugar iliyotoka sare ya kufungana bao 1-1, dhidi ya KenGold FC ya jijini, Mbeya, itakuwa na kibarua kigumu cha kupambana na Bandari Tanzania iliyoichapa Songea United 2-0.

Mtibwa iliyoshuka daraja msimu uliopita, katika mechi saba ilizocheza hadi sasa imeshinda mitatu, sare tatu na kupoteza mmoja, ikiwa nafasi ya saba na pointi 12, huku kwa upande wa Bandari ikishinda minne, sare mbili na kuchapwa mmoja pia.

Mechi kati ya timu hizo inategemewa kuongeza ushindani zaidi kutokana na nafasi zao, ambapo Mtibwa inayoshika nafasi ya saba ina pointi 12, huku kwa upande wa Bandari ikishika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi ikiwa na pointi zake 14.

CHAMP 03

Katika mechi hiyo, Mtibwa Sugar itaingia ikiwa inawategemea Juma Liuzio na Ezekia Mwashilindi kutokana na viwango vyao tangu msimu umeanza, huku Bandari ikiwategemea John Mbise na Anderson Chawaka ambao kila mmoja amefunga mabao mawili.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Awadh Juma ‘Maniche’, amesema anatarajia mechi ngumu kutokana na uimara wa wapinzani wao, japo, wamejiandaa kuutumia vyema uwanja wao nyumbani, baada ya wiki iliyopita kushindwa kubakia na pointi tatu muhimu.

“Mahitaji ya kila timu yamezidisha msimu huu uwe mgumu zaidi, tunaiheshimu Bandari kutokana na aina ya wachezaji bora na benchi la ufundi walilonalo, japo tutahakikisha tunapambana kwa lengo moja la kubakia na pointi tatu,” amesema Maniche.

CHAMP 04

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Bandari Tanzania, Habibu Kondo aliyewahi kuifundisha Mtibwa Sugar, amesema ni furaha kwake kurejea tena sehemu aliyowahi kufanya kazi, huku akisifu kiwango cha wapinzani wao kwa sasa kutokana na uzoefu walionao.

Mechi ya mwisho leo, itapigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini, Dar es Salaam, ambapo Kigamboni United iliyochapwa mabao 2-1, dhidi ya Mbeya Kwanza, itaikaribisha IAA SC ya jijini, Arusha iliyotoka kuilazimisha suluhu (0-0), kikosi cha KMC.

Katika mechi nane ilizocheza Kigamboni United, imeshinda tatu, sare mbili na kupoteza pia mbili, ikiwa nafasi ya nane na pointi 11, huku IAA SC, ikishinda mbili, sare tatu na kupoteza mbili, ikishika nafasi ya tisa na pointi zake pia tisa.

CHAMP 05

Kigamboni inamtegemea mshambuliaji nyota wa kikosi hicho, Abdulkarim Segeja aliyefunga mabao matano akiwa nafasi ya pili ya wafungaji bora, nyuma ya Ramadhan Hashim Kalanje wa KMC FC na Hamdan Sarhani wa Transit Camp wenye saba kila mmoja.

Kwa upande wa IAA SC inayoshiriki Championship kwa mara ya kwanza msimu wa 2026-2027, anayeongoza ni Ombeni Sefue mwenye mabao mawili, huku Shaban Seif, January Lyandungwe, Frank Selemani na Goodluck Tapioh wakifunga bao moja kila mmoja wao.

Raundi ya nane itahitimishwa kesho Jumapili kwa mechi mbili kuchezwa, ambapo Tanzania Prisons iliyotoka kuichapa Transit Camp mabao 2-1, itakuwa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini, Mbeya kucheza na TMA FC iliyotoka suluhu (0-0) na Gunners FC.

CHAMP 06

Katika mechi saba ilizocheza Prisons imeshinda nne, sare moja na kupoteza mbili, ikiwa nafasi ya nne na pointi 13, huku kwa upande wa TMA FC inayoburuza mkiani mwa nafasi ya 16 na pointi mbili, ikishinda moja, sare mbili na kupoteza minne.

Kwenye Uwanja wa Mkwakwani, mjini, Tanga, Bigman FC iliyotoka kushinda mechi yake ya kwanza msimu huu wiki iliyopita kwa kuifunga Stand United ‘Chama la Wana’, mabao 3-2, itaikaribisha Mbeya Kwanza iliyoichapa Kigamboni United kwa mabao 2-0.

Ushindi huo wa Bigman FC ni wa kwanza msimu huu, ikitoka sare moja na kuchapwa mitano, ikishika nafasi ya 14 na pointi nne, huku kwa upande wa Mbeya Kwanza ikishinda mbili, sare moja na kupoteza minne, ikiwa nafasi ya 12 na pointi saba.