Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manchester United sasa yatua kwa Aurelien Tchouameni

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa Man United imekuwa ikimnyatia kiungo huyu kwa muda mrefu na ilishawasilisha hadi ofa ya Pauni 79.4 milioni, lakini Madrid ilikataa.

MANCHESTER United imepanga kumsajili kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Aurelien Tchouameni, 25, katika dirisha lijalo la majira ya baridi au kiangazi.

Inaelezwa Man United imekuwa ikimnyatia kiungo huyu kwa muda mrefu na ilishawasilisha hadi ofa ya Pauni 79.4 milioni, lakini Madrid ilikataa.

Tchouameni amekuwa mchezaji tegemeo kwa Madrid kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi kiwanjani kiasi cha kutumika mara kwa mara kama kiraka.

Mkataba wa sasa wa fundi huyu ambaye kwa sasa yupo nje kwa majeraha yanayotarajiwa kupona Desemba 1, unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 21 za michuano yote.

Awali, mashetani hawa wekundu walihusishwa sana na kiungo wa Brighton, Carlos Baleba, lakini changamoto kubwa inaonekana ni kiasi cha pesa ambacho timu yake inakihitaji ili kumuuza kuwa ni kikubwa.

Inaelezwa Brighton ipo tayari kumuuza Baleba, lakini inahitaji takribani Pauni 90 milioni kama ada ya uhamisho ambayo inaweza kufikia Pauni 100 milioni pamoja na gharama za ziada.


Marc Guehi

CRYSTAL Palace inaamini kuwa Liverpool ndiyo timu pekee itakayojaribu kumsajili beki wao Marc Guehi Januari mwakani. Guehi mwenye umri wa miaka 25, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Crystal Palace ipo tayari kumuuza Januari ili kupata fedha walau kiduchu badala ya kukosa chochote mwisho wa msimu kwani fundi huyu amekataa kusaini mkataba mpya.

Guehi ni miongoni mwa mabeki visiki kwa sasa katika Ligi Kuu England.



Karim Adeyemi

INTER Milan na Manchester United zinafanya mazungumzo na wakala wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Karim Adeyemi, mwenye umri wa miaka 23, ambaye yuko tayari kuondoka Dortmund.

Adeyemi anatafuta timu itakayompa nafasi ya kushinda mataji zaidi tofauti na ilivyo sasa. Manchester United inaamini fundi huyu ataenda kuongeza kasi katika safu yao ya ushambuliaji. Ada yake ya uhamisho inadaiwa kufikia Euro 40 milioni.


Ivan Toney

MSHAMBULIAJI wa Al-Ahli ya Saudi Arabia, Ivan Toney, mwenye umri wa miaka 29, yuko tayari kukubali kupunguza mshahara wake ili kurejea Ligi Kuu ya England Januari mwakani ambako Tottenham na Everton zinavutiwa naye.

Inadaiwa kuwa Toney hafurahii maisha ya Saudi Arabia na anataka kurudi England ili kurudisha nafasi yake ya kuitwa kwenye timu ya taifa.

Everton wanahitaji mfungaji wa uhakika kutokana na ukame wa mabao unaowakumba msimu huu. Ahli wako tayari kumuuza kwa kiasi kinachokadiriwa kufika Pauni 30 milioni.


Kobbie Mainoo

NAPOLI imeanza kuangalia uwezekano wa kusajili kiungo mwingine tofauti na Kobbie Mainoo katika dirisha lijalo la majira ya baridi, lakini staa huyo wa Manchester Unitee bado ameendelea kuwa chaguo lao la kwanza.

Mabosi wa Napoli wameanza kuangalia mbadala kwa sababu wana wasiwasi kwamba huenda Man United ikagoma kumwachia staa huyo.

Mainoo mwenyewe amekuwa akiomba kuondoka tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi.


Tiago Gabriel

JUVENTUES imeanza mazungumzo na wawakilishi wa beki kisiki wa Lecce na timu ya taifa ya Ureno kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21, Tiago Gabriel, 20. Juventus inataka kumsajili staa huyu katika dirisha lijalo la majira ya baridi lakini inakutana na upinzani mkali kutoka kwa Brentford ambayo pia inahitaji saini yake. Kwa mujibu wa ripoti, Lecce inahitaji zaidi ya Pauni 45 milioni ili kumuuza Tiago.


Marc Cucurella

ATLETICO Madrid inamfuatilia kwa karibu beki wa kushoto wa Chelsea na timu ya taifa ya Hispania, Marc Cucurella ambaye inataka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Inaelezwa staa huyu ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza Chelsea, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.

Mabosi wa Atletico wanahitaji kiasi kisichopungua Pauni 35 milioni ili kumnunua lakini pesa hiyo inaonekana kuwa ni kiduchu.


Marc-Andre ter Stegen

BESIKTAS imepanga kumsajili kipa wa Barcelona na timu ya taifa ya Ujerumani, Marc-Andre ter Stegen, 33, kwa mkopo wa nusu msimu utakaokuwa na kipengele cha kumnunua mazima.

Staa huyu ambaye amekuwa hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha Barca amekuwa akiandamwa sana na majeraha ya mara kwa mara.

Mbali ya wababe hao kutoka Uturuki, Tottenham Hotspur pia inahitaji saini yake.