Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yamtaka Antoine Semenyo akamrithi Salah

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Semenyo, ambaye hatoshiriki katika michuano hiyo kwa sababu Ghana haijafuzu, anaonekana kuwa mbadala sahihi kutokana na kiwango bora alichoonyesha akiwa na Bournemouth.

LIVERPOOL imeendelea kupambana ili kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth, Antoine Semenyo, 25, katika dirisha lijalo la usajili wa Januari ili akazibe pengo la staa wao raia wa Misri, Mohamed Salah anayetarajiwa kujiunga na timu ya taifa ya Misri katika michuano ya AFCON inayoanza mwezi ujao.

Semenyo, ambaye hatoshiriki katika michuano hiyo kwa sababu Ghana haijafuzu, anaonekana kuwa mbadala sahihi kutokana na kiwango bora alichoonyesha akiwa na Bournemouth.

Mkataba wake wa sasa wa Semenyo unatarajiwa kumalizika mwaka 2030 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 12 za michuano yote, amefunga mabao sita na kutoa asisti tatu.

Mara kadhaa imewahi kuripotiwa kwamba Bournemouth haitaki kumuuza staa huyo Januari lakini Liverpool huenda ikaweka ofa nono ili kuishawishi ikubali kuwaachia.


Joshua Zirkzee

AS Roma ipo kwenye mazungumzo na Manchester United kuhusu uwezekano wa kumsajili kwa mkopo wa nusu msimu mshambuliaji wa timu hiyo, Joshua Zirkzee mwenye umri wa miaka 24, katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Katika mkataba huo wa mkopo, Roma inataka kuwapo kwa kipengele kitakachowawezesha kumnunua mazima kwa Euro 35 milioni ikiwa itaridhishwa na kiwango chake baada ya msimu kumalizika.


Nicolas Jackson

MSHAMBULIAJI wa Chelsea na timu ya taifa ya Senegal, Nicolas Jackson, 24, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo wa msimu mmoja Bayern Munich, hana nia ya kuvunja mkataba huo Januari na kurudi Chelsea.

Jackson anataka kupigania nafasi yake Bayern licha ya ushindani mkali uliopo.

Vilevile Bayern inamwona kama mbadala sahihi wa Harry Kane katika eneo la ushambuliaji kwa sababu huenda staa huyo akaondoka mwakani.


Gonzalo Garcia

INAELEZWA Real Madrid ipo tayari kusikiliza ofa ya kuanzia Euro 20 milioni kutoka kwa timu inayohitaji mshambuliaji wake chipukizi Gonzalo Garcia, 21, ambaye anawindwa na timu nyingi za England ikiwa pamoja na Sunderland, Aston Villa na Wolves. Garcia amekuwa miongoni mwa vijana waliowahi kutabiriwa kuwa hazina kwa hapo baadaye lakini amekuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Madrid.


David Alaba

REAL Madrid haina haraka ya kuanza mazungumzo ya mkataba mpya na beki wao wa kati David Alaba 33, ambaye yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake wa sasa na anaweza kuondoka bure Juni mwakani.

Alaba amekuwa hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza tangu apate jeraha baya la goti Desemba 2023 na kufanyiwa upasuaji.

Msimu uliopita alicheza mechi 10 za michuano yote.


Carlos Baleba

KATIKA jitihada za kocha Ruben Amorim kuimarisha safu yake ya kiungo cha kati kwenye kikosi cha Manchester United, amekuwa akipiga hodi kila mara kwa viongozi wake wa juu akitaka kusajiliwa kwa kiungo raia wa Cameroon, Carlos Baleba, 21, anayeichezea Brighton.

Baleba amekuwa mmoja wa viungo bora vijana katika Ligi Kuu England tangu msimu uliopita na Brighton inahitaji takribani Pauni 90 milioni ili kumuuza.


Ademola Lookman

KUNA uwezekano mkubwa Tottenham ikafeli katika mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Atalanta, Ademola Lookman, 28, baada ya timu hiyo kubadilisha kocha.

Lookman alikuwa na uhusiano mbaya na kocha aliyepita, Ivan Juric kiasi cha kuomba kuondoka lakini kufukuzwa kwake kunaweza kusababisha akabadilisha mawazo.

Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu huu amecheza mechi 10 za michuano yote na kufunga bao moja tu.


Christian Pulisic

KIUNGO mshambuliaji wa AC Milan na timu ya taifa ya Marekani, Christian Pulisic, 27, anataka kusubiri hadi AC Milan iwe na uhakika wa kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao kabla ya kusaini mkataba mpya na miamba hiyo ya Serie A.

Pulisic amekuwa mchezaji muhimu tangu ajiunge na Milan kutoka Chelsea 2023, na klabu hiyo inataka kumuongeza mkataba.