Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yabaniwa kwa Semenyo, lakini haijaisha

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa Semenyo, 25, ni miongoni mwa wachezaji ambao Liverpool ilikuwa inataka sana kuwasajili dirisha lijalo la majira ya baridi kwa ajili ya kuboresha safu yao ya ushambuliaji.

MPANGO wa Liverpool kutaka kimsajili mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana Antoine Semenyo, unakaribia kufa baada ya klabu yake kuendelea kushikilia msimamo wa kutohitaji kumuuza staa huyo.

Inaelezwa Semenyo, 25, ni miongoni mwa wachezaji ambao Liverpool ilikuwa inataka sana kuwasajili dirisha lijalo la majira ya baridi kwa ajili ya kuboresha safu yao ya ushambuliaji.

Mbali ya kuboresha safu ya ushambuliaji, Liverpool ilikuwa inamwangalia Semenyo kama mbadala sahihi wa Mohamed Salah ambaye atakisekana kuanzia mwezi ujao kutokana na majukumu yake ya timu ya taifa ya Misri ambayo itashiriki michuano ya AFCON.

Liverpool ilikuwa imepanga kuwasilisha zaidi ya Pauni 70 milioni kama ada ya uhamisho ili kumsajili Semenyo lakini kwa sasa shida kubwa haionekani kuwa ni pesa kwani Bournemouth imegoma tu na inataka kuendelea kuipata huduma ya Staa huyo hadi mwisho wa msimu ambapo ndio itamuuza.

Mbali ya kumbakisha ili kusaidia timu Bournemouth inaamini Semenyo atapanda zaidi thamani baada ya kumalizika kwa msimu huu na wanaweza kumuuza kwa bei kubwa zaidi.


Said El Mala

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amevutiwa sana na kiwango cha winga wa Cologne,  Said El Mala, 19,  ambaye anataka kuipata saini yake dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Maskauti wa Man City wamekuwa  wakimfuatilia kwa karibu fundi huyu na ripoti yao inaonekana kumvutia sana Guardiola kiasi cha kusisitiza yaanzishwe mazungumzo na wawakilishi wake haraka ili kumsajili.


Elliot Anderson

Nottingham Forest haina mpango wa kumuuza kiungo wao wa kimataifa wa England, Elliot Anderson katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi licha ya vigogo mbalimbali kutamani kumsainisha. Ripoti zinaeleza, licha ya kwamba Forest haina mpango wa kumuuza fundi huyu, inaweza kufikiria kufanya hivyo ikiwa itapokea ofa inayoanzia Pauni 100 milioni kama ada yake ya uhamisho.Elliot mwenye umri wa miaka 23, anawinda na Newcastle United na Manchester United.


Joao Gomes

KIUNGO wa Wolves, Joao Gomes yupo tayari kujiunga na Manchester United dirisha lijalo la majira ya baridi na ripoti zinadai anaweza akanunuliwa kwa Pauni 44 milioni. Staa huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 24, amevutiwa sana na mipango ya Kocha Ruben Amorim ambaye amekuwa akizungumza naye kwa muda sasa akimshawishi ajiunge na timu hiyo. Mkataba wa sasa wa staa huyu anatarajiwa kumalizika 2028.


Kenan Yildiz

Arsenal, Chelsea na Real Madrid zinatarajiwa kuingia vitani dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kumsajili mshambuliaji wa Juventus na timu ya taifa ya Uturuki mwenye umri wa miaka 20. Yildiz ambaye nj miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Juventus, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Mabosi wa Juventus wamekuwa wakipambana kumsainisha mkataba mpya lakini staa huyu anadaiwa kukataa.


Niclas Fullkrug

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani, Niclas Fullkrug, 32, anatarajiwa kuondoka West Ham mwezi Januari na tayari yupo katika mazungumzo na timu za Bundesliga. Kabla ya kujiunga na West Han staa huyu alikuwa akiichezea Borussia Dortmund ambayo pia inahitaji huduma yake kwa sasa. Fullkrug amekuwa akipambana kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha West Ham lakini inaonekana kushindikana.


Ivan Toney

Mshambuliaji wa Al-Ahli ya Saudi Arabia, Ivan Toney, 29, anatarajiwa kuendelea kubaki katika klabu yake licha ya kuhitajika na klabu nyingjne kama  Tottenham, Everton na West Ham. Toney alijiunga na Al-Ahli 2024 kwa usajili huru baada ya mkataba wake kumalizika. Tottenham inamwangalia kama mbadala wa Harry Kane. West Ham pia inahitaji huduma ya staa huyu.


Conor Gallagher

KIUNGO wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya England, Conor Gallagher amekanusha uwezekano wa kuondoka dirisha lijalo akisisitiza bado ataendelea kuitumikia timu hiyo kwani ana furaha sana na maisha ya Jiji la Madrid. Fundi huyo anahusishwa sana na Manchester United ambayo ilikuwa na mpango wa kumsajili dirisha lijalo la majira ya baridi.