Manchester United hali tete huko Ulaya
Muktasari:
- Atletico Madrid iliandika bao la kuongoza katika dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kiungo Pablo Barrios kisha mshambuliaji Ademola Lookman akamaliza mchezo kwa kufunga bao la pili katika dakika ya 79.
Madrid, Hispania. Manchester United imepoteza mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Atletico Madrid ya Hispania, katika mchezo uliochezwa jana, Oktoba 13, 2026.
Atletico Madrid iliandika bao la kuongoza katika dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kiungo Pablo Barrios kisha mshambuliaji Ademola Lookman akamaliza mchezo kwa kufunga bao la pili katika dakika ya 79.
Katika dakika ya 74 Man United ilipata pigo baada ya beki wake, Leny Yoro, kuonyeshwa kadi nyekundu na kulazimika kucheza wakiwa pungufu.
Huu unakuwa ni mchezo wa tano mfululizo Man United inaondoka bila ushindi katika mashindano yote iliyocheza kwani imetoka sare mechi mbili na kupoteza mechi tatu huku mara ya mwisho ilipata ushindi katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sabah Baku, Septemba 10, 2026.
Matokeo ya mechi nyingine
Arsenal 3-0 Lille
Leins 0-2 Sporting CP
Sabah Baku 2-0 Slavia Prague
Galatasaray 1-4 Barcelona
Inter Milan 3-4 Club Brugge
RB Leipzig 1-0 PSV
Viking 3-3 Bayern Munich
Villarreal 3-1 Napoli