Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yazidi kutumbukia kwenye mgogoro, mustakabali wa Carrick watikisika

Muktasari:

  • Kabla ya mchezo huo, Atletico iliweka bango lenye ujumbe “Linda kile tunachokipenda”, lakini United ilishindwa kuzuia mashambulizi ya wenyeji na kuendeleza mwenendo wake mbaya katika msimu huu.

MADRID, HISPANIA: MANCHESTER United imeendelea kuyumba baada ya kukumbana na kipigo dhidi ya Atletico Madrid, matokeo yanayozidi kuweka mashakani mustakabali wa kocha Michael Carrick, ambaye kikosi chake sasa kimetimiza mechi tano mfululizo bila ushindi.

Kabla ya mchezo huo, Atletico iliweka bango lenye ujumbe “Linda kile tunachokipenda”, lakini United ilishindwa kuzuia mashambulizi ya wenyeji na kuendeleza mwenendo wake mbaya katika msimu huu.

Hata hivyo, haikuwa mechi ambayo United ilicheza vibaya kila idara, kama ambavyo mashabiki wake 3,750 waliokuwa katika sehemu ya juu ya Uwanja wa Wanda Metropolitano walivyoweza kutarajia. Timu hiyo ilipata nafasi za kusawazisha na kugonga mwamba, lakini ilishindwa kuzitumia.

United pia ililazimika kucheza ikiwa na wachezaji 10 katika dakika 15 za mwisho baada ya mwamuzi, kwa msaada wa teknolojia ya VAR, kuamua kuwa Leny Yoro alimwangusha Jonathan David kwa makusudi alipokuwa na nafasi ya kufunga.

Licha ya kupambana hadi mwisho, kipigo hicho kimeongeza presha kwa Carrick, ambaye ana kibarua kigumu cha kuendelea kuinoa timu hiyo baada ya mwezi huu.

Huo ulikuwa mchezo wa nne kupoteza kati ya tisa iliyocheza msimu huu, huku Sir Jim Ratcliffe, mmoja wa wamiliki wa klabu hiyo, akiwa uwanjani kushuhudia matokeo hayo.

Ratcliffe amehudhuria michezo mitatu ya ugenini ya United katika mashindano ya Ulaya, lakini timu hiyo haijaibuka na ushindi katika mchezo wowote kati ya hiyo.

Uwanja wa Wanda Metropolitano unatarajiwa kuandaa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi Juni, lakini mashabiki wa United waliokuwa na matumaini ya kuiona timu yao ikifika hatua hiyo huenda sasa wakaanza kuyapima upya matarajio yao.

Katika kujaribu kuizuia timu isizidi kuporomoka, Carrick alifanya mabadiliko makubwa ya kiufundi. Bruno Fernandes, ambaye amekuwa akionyesha kiwango kisichoridhisha katika wiki za hivi karibuni, alihamishiwa upande wa kulia, huku Youri Tielemans akisogezwa mbele na Carlos Baleba kuunganishwa na Andrey Santos kwa mara ya kwanza.

Mpango huo ulilenga kuifanya United icheze kwa mshikamano zaidi na kuziba mianya iliyokuwa imefichuliwa na Tottenham katika mchezo uliopita. Hata hivyo, Atletico ilianza kwa kasi zaidi.

Ingawa Atletico ni timu yenye ubora unaostahili kuheshimiwa, kumhamishia Fernandes upande wa kulia kulizua maswali kuhusu nafasi yake katika mfumo wa timu. Ilikuwa mara yake ya kwanza kucheza upande huo tangu Oktoba 2023.

Mabadiliko hayo yameibua mjadala kuhusu kama uwepo wa Fernandes unaathiri namna United inavyocheza, pamoja na hatma ya mkataba wake mpya.

Katika tukio moja, Fernandes aliposhindwa kuudhibiti mpira vizuri, alisimama kwa muda badala ya kuendelea kukimbia. Mchezaji huyo pia alionekana kutoridhishwa na nafasi yake mpya, huku lugha ya mwili ikionyesha kukata tamaa.

Ayden Heaven, ambaye mechi zake mbili za mwanzo alizoanza msimu huu ziliishia kwa vipigo, alipewa nafasi ya kucheza beki wa kushoto kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka la ushindani wa kiwango cha juu. Udhaifu wake katika nafasi hiyo ulionekana katika sehemu mbalimbali za mchezo.


Mabadiliko hayo ya kikosi hayakudumu hata dakika moja kabla ya United kuruhusu bao. Diogo Dalot na Yoro waliacha nafasi kubwa katika safu ya ulinzi, iliyotumiwa na Alex Baena kupokea mpira, kugeuka na kumpasia Pablo Barrios.

Barrios alipiga shuti la ndani ya mguu lililogonga Heaven aliyekuwa akiteleza kujaribu kuzuia mpira, kabla ya kuingia wavuni na kuipa Atletico bao la kuongoza.

Carrick alionekana kukata tamaa, akainamisha kichwa na kurejea benchi la ufundi huku akitazama marudio ya bao hilo.

Hata hivyo, mashabiki wa United waliokuwa ugenini waliendelea kuishangilia timu yao, huku wachezaji nao wakipambana badala ya kukata tamaa kama ilivyokuwa kwa Tottenham ilipocheza katika uwanja huo msimu uliopita.

United ilikaribia kusawazisha dakika ya 14 kupitia Tielemans, ambaye alikuwa akicheza nafasi ya kiungo mshambuliaji. Baada ya kupokea pasi kutoka kwa Yoro, alimpatia Bryan Mbeumo, aliyemzidi ujanja David Hancko na kupiga shuti lililookolewa na kipa Jan Oblak.

Dakika moja baadaye, United ilipata nafasi nyingine baada ya Lisandro Martinez kupiga pasi ya juu iliyomfikia Marcus Rashford, ambaye alipaswa kuudhibiti mpira vizuri ili kupata nafasi ya kukabiliana na kipa akiwa peke yake.