Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yashusha bili ya mishahara

MAN Utd Pict

Muktasari:

  • Man United imevuna Pauni 47 milioni kwenye dili zake za kibiashara, licha ya kwamba mapato hayo ya matangazo yameshuka kwa karibu Pauni 5 milioni.

MANCHESTER, ENGLAND: BILI ya mishahara ya Manchester United imeshuka kwa hesabu za robo ya kwanza ya mwaka wa fedha.

Baada ya kupunguza wafanyakazi mara mbili tofauti na kulipa bonasi chache bili ya mishahara ya Man United imeshuka hadi Pauni 73.6 milioni licha ya kufanya usajili wa Pauni 232.7 milioni kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Barcelona inalipa mshahara wa Marcus Rashford wa Pauni 325,000 kwa wiki baada ya kumchukua kwa mkopo wa msimu mmoja, jambo ambalo limekuwa na faida kubwa kwa Man United katika bili yake ya mishahara.

Barca ina kipengele cha kumbeba jumla Rashford huku kiungo Casemiro anayelipwa mshahara mkubwa atalazimika kushusha ili abaki kwenye kikosi hicho cha Old Trafford. Jadon Sancho kwenye mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki, naye anajiandaa kuondoka kwenye timu hiyo wakati mkataba wake utakapofika tamati Juni mwakani.

Kutokana na hilo, Man United sasa itakuwa na uwezo wa kufanya usajili wa viungo inaowasaka kwenye dirisha lijalo la kiangazi akiwamo Elliot Anderson, Adam Wharton na Carlos Baleba.

Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Man United, Omar Berrada anaamini hesabu mpya za kifedha za klabu hiyo zinaonyesha jinsi timu ilivyo kwenye utaratibu mzuri wa kujiendeesha.

Kwenye hesabu hizo, Man United imepata faida ya Pauni 13 milioni katika robo fainali huku hilo likitokana na mauzo ya tiketi ya mechi zao licha ya kwamba haipo kwenye michuano ya Ulaya.
 

Man United imevuna Pauni 47 milioni kwenye dili zake za kibiashara, licha ya kwamba mapato hayo ya matangazo yameshuka kwa karibu Pauni 5 milioni.