Mabosi Man United wakiri kuna shida
Muktasari:
- Dirisha lililopita, Man United ilimpa kocha wake Ruben Amorim kiasi hicho cha pesa ili kusajili wachezaji wapya na alifanikiwa kumpata Benjamin Sesko kwa Pauni 74 milioni pamoja na Matheus Cunha na Bryan Mbeumo kwa Pauni 120 milioni pamoja na kipa Senne Lammens ambaye alisajiliwa baada ya msimu kuanza.
MANCHESTER, ENGLAND: MABOSI wa Manchester United wamekubali kikosi cha timu hiyo bado kina upungufu licha ya kusajili wachezaji kadhaa kwa Pauni 200 milioni dirisha lililopita la majira ya kiangazi.
Dirisha lililopita, Man United ilimpa kocha wake Ruben Amorim kiasi hicho cha pesa ili kusajili wachezaji wapya na alifanikiwa kumpata Benjamin Sesko kwa Pauni 74 milioni pamoja na Matheus Cunha na Bryan Mbeumo kwa Pauni 120 milioni pamoja na kipa Senne Lammens ambaye alisajiliwa baada ya msimu kuanza.
Hata hivyo, licha ya usajili huo, viongozi wa Man United hawana matumaini makubwa ya timu hiyo kufanya vizuri wakiamini kikosi alichonacho na badala yake kinahitaji kufanyiwa maboresho ili kupata matokeo zaidi.
Mapema wiki hii, Man United iliharibu rekodi yao ya kutopoteza mechi tano mfululizo mfululizo baada ya kufungwa na Everton ambayo ilikuwa pungufu baada ya staa wao Idrissa Gana Gueye kuonyeshwa kadi nyekundu dakika za mwanzo za kipindi cha kwanza.
Licha ya mpango wa kutaka kufanya maboresho katika kikosi chao, ripoti kutoka tovuti ya ESPN zinaeleza hawana mpango wa kufanya usajili dirisha lijalo la majira ya baridi badala yake watasubiri hadi dirisha la majira ya kiangazi ingawa inaweza kufikiria kuingiza wachezaji wapya ikiwa itatokea dharula kama majeruhi.
Moja ya sababu zinazowafanya mashetani hawa wekundu kutotaka kusajili Januari ni wanaamini wachezaji wengi huuzwa bei kwa wakati huo, pia wanataka kusubiri mwisho wa msimu ili kuuza kwanza wachezaji wao kama Marcus Rashford na Jadon Sancho na kupata pesa zaidi.
Moja kati ya eneo wanalohitaji zaidi kulifanyia usajili ni lile la kiungo na mastaa kama Elliot Anderson, Adam Wharton na Carlos Baleba wanatajwa kuwa katika rada zao.