Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yampigia hesabu kali Kolo Muani

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa  Juventus ambayo aliichezea kwa mkopo msimu uliopita, bado inataka kuendelea kuwa naye kwa mkataba wa mkopo kwa msimu mwingine jambo ambalo mabosi wa PSG hawataki.

MANCHESTER United imeingia katika mchakato wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa, Randal Kolo Muani, mwenye umri wa miaka 26, ambaye anawindwa na timu nyingine kubwa barani Ulaya.

Inaelezwa  Juventus ambayo aliichezea kwa mkopo msimu uliopita, bado inataka kuendelea kuwa naye kwa mkataba wa mkopo kwa msimu mwingine jambo ambalo mabosi wa PSG hawataki.

Matajiri hao wa Jiji la Paris wanadaiwa kuwaambia Juventus kwamba aidha wamnunue jumla au kama wanamtaka kwa mkopo basi kiwepo kipengele kitakachowalazimisha kumnunua jumla mwisho wa msimu huu.

Juventus ndio inaonekana kuwa mpinzani halisi wa Man United katika dirisha hili na inatamani sana kumsajili kutokana na kiwango bora alichoonyesha  alipokuwa akicheza kwa mkopo katika kikosi chao.

Katika msimu uliopita akiwa na Juventus katika michuano ya Kombe la Dunia la Klabu, Muani alicheza mechi tatu na kufunga mabao mawili.

Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

Kocha wa Man United, Ruben Amorim bado anahitaji kuboresha eneo lake la ushambuliaji na miongoni mwa wachezaji anaodaiwa kuwapendekeza ni huyu Kolo Muani, ambaye pia ni staa wa timu ya taifa ya Ufaransa, ambaye tayari amecheza fainali moja za Kombe la Dunia walipolala dhidi ya Argentina.


Dominic Calvert-Lewin

ASTON Villa inajiandaa kuingia katika vita dhidi ya AC Milan na Newcastle ili kuipata saini ya aliyekuwa mshambuliaji wa Everton na England, Dominic Calvert-Lewin, mwenye umri wa miaka 28, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na Everton kumalizika mwisho wa msimu uliopita. Awali, Lewin aliripotiwa kuwa katika rada za Manchester United lakini mashetani hao wanaonekana kurudi nyuma katika dili la kumsajili kwa sasa.


Alexander Isak

NEWCASTLE United inatarajia kupokea ofa rasmi kutoka Liverpool wiki hii kwa ajili ya mshambuliaji wao wa kimataifa wa Sweden mwenye umri wa miaka 25, Alexander Isak. Isak amekuwa katika rada za Liverpool kwa muda sasa na tayari ameshawaambia vigogo wa Newcastle kwamba hahitaji kuendelea kubakia katika kikosi hicho kwa msimu ujao. Newcastle inataka Pauni 150 milioni kama ada yake ya uhamisho. Mkataba wake unaisha mwaka 2029.

Msimu uliopita alicheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao 27.


Igor Paixao

LEEDS United imetuma ofa ya pili ya Euro 32 milioni kwenda Feyenoord kwa ajili ya kuipata huduma ya winga wa Feyenoord, Igor Paixao, katika dirisha hili. Staa huyu wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 25, anawindwa na timu nyingi barani Ulaya kutokana na kiwango alichoonyesha msimu uliopita. Paixao ambaye pia anawindwa na West Ham, msimu uliopita alicheza mechi 47 za michuano yote.


Michael Cooper

WEST Ham imeanza mazungumzo na wawakilishi wa kipa wa Sheffield United, Michael Cooper, mwenye umri wa miaka 25 na kuna uwezekano ikawasilisha ofa rasmi kwenda kwa timu yake ili kumsajili. Akiwa na Sheffield katika mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza England msimu uliopita, Cooper alicheza mechi 46 za michuano yote na kuruhusu mabao 35 na amecheza mechi 23 bila ya kuruhusu hata bao moja.


Sam Johnstone

BURNLEY inataka kumsajili kipa wa Wolves ambaye ni raia wa England, Sam Johnstone, mwenye unri wa miaka 32 akawe mbadala wa James Trafford, aliyejiunga na Manchester City katika dirisha hili. Johnstone mwenyewe anadaiwa kuwa ameshafikia makubaliano binafsi na mabosi wa Burnely na amevutiwa sana na mpango uliowekwa mezani na Burnley. Mkataba wa Trafford unaisha mwaka 2028.


Malick Yalcouye

MABOSI wa Toulouse wamefungua mazungumzo rasmi na Brighton kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa timu hiyo na Mali mwenye umri wa  miaka 19, Malick Yalcouye.

Hapo awali ilidaiwa kuwa Malick angeuzwa kwenda timu mojawapo ya Championship ya England lakini ofa ya Toulouse inaonekana kumvutia zaidi.


Amine Adli

WOLVES inapambana kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Morocco, Amine Adli, 25, klabu yake inaonekana kuwa kikwazo kutokana na kiasi kikubwa cha pesa  inachohitaji. Tovuti ya Bild imefichua kwamba, Leverkusen inahitaji takribani Euro 30 milioni ili kumuuza. Mkataba wake unaisha 2028.