Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yajitosa jumla jumla kwa Sesko

SESKO Pict

Muktasari:

  • Straika huyo wa kimataifa wa Slovenia, Sesko na yule wa Aston Villa, Ollie Watkins wametajwa kuwa washambuliaji wawili waliowekwa kwenye rada za Man United, ambapo kocha Ruben Amorim anataka huduma ya mmoja akaongoze safu yake ya ushambuliaji kwa ajili ya msimu ujao.

MANCHESTER, ENGLAND: MAMBO ni moto. Manchester United imeamua kwenda miguu yote kwenye ofa yao ya kumchukua straika wa RB Leipzig, Benjamin Sesko.

Straika huyo wa kimataifa wa Slovenia, Sesko na yule wa Aston Villa, Ollie Watkins wametajwa kuwa washambuliaji wawili waliowekwa kwenye rada za Man United, ambapo kocha Ruben Amorim anataka huduma ya mmoja akaongoze safu yake ya ushambuliaji kwa ajili ya msimu ujao.

Na kwenye ishu ya Sesko, ili kunasa saini yake, Man United italazimika kutumia Pauni 70 milioni kwa mujibu wa bei ambayo imeelezwa kutajwa na Leipzig.

Sesko sasa anatajwa kuwa chaguo la kwanza la kocha Amorim kwenye msako wake wa kutafuta Namba 9 kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi.

Na hilo limekuja baada ya Aston Villa kudai kwamba haifikirii kabisa kumuuza Watkins, hivyo sasa Man United nguvu zote zimeelekezwa kwa Sesko, ambaye atagharimu Pauni 70 milioni na bonasi kadhaa.

Mkurugenzi wa usajili wa Man United, Christopher Vivell na bosi wa kusimamia dili hizo kufikia makubaliano, Matt Hargreaves walisafiri kwenda Ujerumani kuweka mchakato huo kwenye hatua nzuri, huku mabosi hao wa Old Trafford watapambana kuhakikisha Leipzig inashusha bei.

Vivell alikuwa mfanyakazi kwenye kampuni ya Red Bull inayozimiliki klabu za Leipzig na timu ya zamani wa Sesko, Salzburg kwa miaka saba, hivyo anamfahamu vizuri straika huyo mwenye umri wa miaka 22 na kimo cha futi 6 inchi 5.

Alipohojiwa hivi karibuni huko Ujerumani, Vivell alisema: “Benjamin Sesko ni mmoja wa vijana wenye vipaji vikubwa sana na wenye nafasi ya kuja kuwa wachezaji wa daraja la juu. Ana viwango vyote vya kufikia huko.

“Ni mwepesi, ana uwezo mkubwa wa kuruka na ni hodari hewani. Benjamin ni mfungaji mahiri, ambaye hakai sehemu moja na ni fundi pia. Uwezo wake umemfanya kuwa mchezaji spesho na mwenye rekodi spesho.”

Ripoti zinafichua kwamba Sesko, ambaye pia alikuwa kwenye rada za Arsenal katika dirisha hili, atachagua uhamisho wa kwenda Old Trafford. Licha ya kwamba Newcastle inayomtaka pia inaweza kumpa ofa ya kucheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, staa huyo anatazamiwa kuchagua kutua Man United, ambayo haitakuwapo kwenye michuano yoyote ya Ulaya msimu huu.

Kocha wa Newcastle, Eddie Howe ameanza kuwa na wasiwasi juu ya kumpata Sesko, ambaye alifunga mabao 39 kwa misimu miwili huko kwenye Bundesliga, baada ya Man United kuingia mbele kutaka huduma yake.

Leipzig haitajivunga kuipa Man United mchezaji Sesko kama mkwanja wanaotaka utawekwa mezani, ambapo Pauni 70 milioni, zilidaiwa ndizo zilizoikimbiza Arsenal kwenda kumchukua Viktor Gyokeres kwa ada ya Pauni 63 milioni. Sesko alijiunga na RB Salzburg mwaka 2023 na ameichezea timu hiyo mechi 87 ikiwamo za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Man United imeshafanya uwekezaji mkubwa kwenye safu yake ya ushambuliaji baada ya kuwanasa Matheus Cunha na Bryan Mbeumo kwa ada ya pamoja ya Pauni 133.5 milioni.


MECHI 10 ZA KWANZA ZA MAN UNITED EPL 2025-2026

-Agosti 17 vs Arsenal (nyumbani)

-Agosti 24 vs Fulham (ugenini)

-Agosti 30 vs Burnley (nyumbani)

-Septemba 14 vs Man City (ugenini)

-Septemba 20 vs Chelsea (nyumbani)

-Septemba 27 vs Brentford (ugenini)

-Oktoba 4 vs Sunderland (nyumbani)

-Oktoba 18 vs Liverpool (ugenini)

-Oktoba 25 vs Brighton (nyumbani)

-Novemba 1 vs Nottm Forest (ugenini)