Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City yaingilia dili la Simons kwenda Chelsea

TETESI Pict

Muktasari:

  • Simons, ambaye alisaini mkataba wa kudumu na Leipzig dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana baada ya kuonyesha kiwango bora akiwa kwa mkopo kwenye klabu hiyo, amekuwa rada za Chelsea tangu kuanza kwa dirisha hili lakini dili linakwamishwa na masuala ya masilahi baina ya timu.

MANCHESTER City inadaiwa kuingilia kati dili la Chelsea la kumsajili winga wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Uholanzi, Xavi Simons, 22.

Simons, ambaye alisaini mkataba wa kudumu na Leipzig dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana baada ya kuonyesha kiwango bora akiwa kwa mkopo kwenye klabu hiyo, amekuwa rada za Chelsea tangu kuanza kwa dirisha hili lakini dili linakwamishwa na masuala ya masilahi baina ya timu.

Chelsea haitaki kutoa pesa ili kuipata huduma ya fundi huyu na badala yake inataka kufanya mabadilishano ya wachezaji suala ambalo Leipzig inalipinga.

Leipzig inahitaji zaidi ya Pauni 50 milioni ili kumuuza Simons wakati Chelsea wakihitaji kufanya mabadilishano ya staa huyo na Christopher Nkuku.

Man City inaonekana huenda ikaipiku Chelsea na kufanikisha mchakato wa kumsajili kwa haraka kwa sababu ipo tayari kutoa pesa ili kumnunua.

Simons ambaye msimu uliopita akiwa na Leipzig, alifunga mabao 10 na kutoa asisti 13 katika michuano yote  amekuwa akifuatiliwa kwa muda mrefu na Man City na Pep Guardiola anaamini ataenda kuongeza nguvu zaidi katika eneo la kiungo ambalo limeondokewa na mastaa zaidi ya wawili dirisha hili.

Mbali ya  kucheza kiungo mchezeshaji, pia ana uwezo wa kucheza kama namba 10 au winga, jambo linalofanya timu nyingi zivutiwe naye.


Carlos Baleba

BRIGHTON inahitaji Pauni 100 milioni ili kumuuza  kiungo wao wa  kati wa kimataifa wa Ujerumani,  Carlos Baleba, 21, baada ya Manchester United kuonyesha nia ya kumsajili. Baleba, aliyesajiliwa kutoka Lille mwaka 2023, amekuwa mhimili muhimu wa safu ya kiungo ya Brighton msimu uliopita akicheza mechi 33, pia alishinda  tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa klabu hiyo. Hata hivyo, Man United haina mpango wa kutoa kiasi hicho ingawa ofa yao ya kwanza inaweza kufikia Pauni 60 milioni.


Rasmus Hojlund

MSHAMBULIAJI wa Manchester United na timu ya taifa ya Denmark, Rasmus Hojlund yupo tayari kuondoka  Old Trafford katika majira haya ya kiangazi kujiunga na AC Milan ambayo inataka  kumchukua kwa mkopo wenye kipengele cha kumnunua kabisa ifikapo mwisho wa msimu ujao. Hojlund, aliyesajiliwa na Man United kwa Pauni 72 milioni akitokea Atalanta msimu uliopita, alifunga mabao 14 katika mashindano yote msimu kwa msimu uliopita.


Maghnes Akliouche

MANCHESTER City imeongeza jina la kiungo mshambuliaji wa Monaco, Maghnes Akliouche, 23, kwenye orodha ya mastaa inayohitaji kuwasajili dirisha hili. Hata hivyo, ili kumpata itatakiwa kushinda vita dhidi ya Bayer Leverkusen ambayo pia inahitaji saini yake. Akliouche aling’ara Ligue 1 msimu uliopita akifunga mabao nane na asisti tisa. Ripoti zinadai mchezaji mwenyewe anatamani zaidi kujiunga na Man City.


Leon Bailey

AS Roma iko kwenye mazungumzo na Aston Villa kuhusu uwezekano wa kumsajili winga wa Jamaica, Leon Bailey 28, dirisha hili, lakini  bado haijatoa ofa rasmi. Bailey ambaye aliwahi kucheza timu moja na Mbwana Samatta ya KRC Genk, pia anawindwa  na  Besiktas ya Uturuki na timu kadhaa za Saudi Arabia. Msimu uliopita staa huyu alionyesha kiwango bora  wenye akifunga mabao tisa na kutoa asisti saba katika Ligi Kuu England.


Kevin

FULHAM iko tayari kuvunja rekodi yao ya usajili ya Pauni 34 milioni ili kumsajili winga raia wa Brazili Kevin, 22, kutoka Shakhtar Donetsk dirisha hili. Kevin aling’ara kwenye Ligi Kuu ya Ukraine msimu uliopita ambapo alifunga mabao 12 na kutoa asisti 10 za michuano yote. Ripoti zinaeleza kuna uwezekano Fulham ikalipa takriban Pauni 36 milioni kwa ajili ya kuipata saini yake.


Alejandro Garnacho

MANCHESTER United inasubiria ofa rasmi kutoka Chelsea inayohitaji huduma ya winga wake, Alejandro Garnacho, 21, dirisha hili. Ripoti zinaeleza kinachokwamisha dili hilo kwa sasa ni Chelsea inahitaji kulipa chini ya Pauni 50 milioni ambayo inahitajika na Man United.  Garnacho ni miongoni mwa wachezaji waliopewa ruhusa ya kuondoka katika dirisha hili.


Nick Woltemade

BAYERN Munich imewasilisha ofa ya Pauni 52 milioni Stuttgart ili kumsajili  mshambuliaji wa timu hiyo, Nick Woltemade, 23, dirisha hili lakini ofa hiyo inadaiwa kukataliwa na mabosi wa Stuttgart wanaohitaji Pauni 65 milioni ili kumuuza staa huyo tegemeo katika timu yao. Woltemade ambaye alijiunga na Stuttgart akitokea Werder Bremen, alifunga mabao 18 ya michuano yote kwa msimu uliopita.