Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City yaandika mwanzo bora, historia yatoa onyo la ubingwa

Muktasari:

  • Mapumziko ya kwanza ya mechi za kimataifa msimu huu daima hutoa muda wa kutafakari na kujaribu kuelewa kilichotokea katika mechi za mwanzo za msimu.

LONDON, ENGLAND: MANCHESTER City imeanza msimu kwa kushinda mechi zote tano, lakini kama ambavyo Ligi Kuu England imethibitisha mara nyingi huko nyuma, mashindano hayo ni kama mbio za masafa marefu, siyo za kasi.

Mapumziko ya kwanza ya mechi za kimataifa msimu huu daima hutoa muda wa kutafakari na kujaribu kuelewa kilichotokea katika mechi za mwanzo za msimu.

Bila shaka, msimu wa 2026-27 hautofautiani sana na mingine, lakini safari hii klabu zimepata muda mrefu zaidi wa kutafakari iwapo zimeanza vizuri au zimekwama kutokana na mapumziko marefu ya Septemba mpaka Oktoba.

Ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England, Manchester City ndiyo timu pekee iliyoshinda mechi zote tano katika msimu wa 2026-27, huku klabu hiyo ikianza maisha baada ya Pep Guardiola kwa njia bora kabisa uwanjani. Tayari imefungua pengo la pointi tatu dhidi ya Arsenal, ambayo ni mpinzani wake mkubwa katika mbio za ubingwa, lakini je, mwanzo huo wa kasi unamaanisha moja kwa moja kwamba City inatarajiwa kutwaa taji la Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu?

Bila shaka, kuna suala dogo la City kuripotiwa kupatikana na hatia katika makosa 114 kati ya 115 ya ukiukaji wa kanuni za kifedha iliyoshtakiwa, ambayo imekanusha, lakini kwa madhumuni ya makala hii, tutajaribu kupuuza madhara yote yanayoweza kutokea kutokana na suala hilo.


MWANZO WA USHINDI

Kikosi hicho cha Enzo Maresca kimekuwa timu ya 15 tofauti kushinda mechi zake tano za kwanza katika msimu wa Ligi Kuu England, na hii ni mara ya nne kwa City kufanya hivyo. Hata hivyo, City imeshinda taji katika msimu mmoja tu kati ya misimu mitatu iliyopita ambayo ilianza kwa ushindi wa asilimia 100 katika mechi tano za kwanza. Walitwaa ubingwa 2023-24, lakini walishindwa kutumia vyema ushindi wa mechi tano mfululizo mwanzoni mwa msimu katika misimu ya 2015-16 na 2016-17.

Hilo linafuata mwenendo mpana zaidi katika ligi unapozitazama timu zilizoshinda mechi zao tano za kwanza za msimu. Ni timu nne tu kati ya 14 zilizoshinda mechi tano za kwanza katika msimu wa Ligi Kuu England ambazo zimeendelea kutwaa ubingwa msimu huo (asilimia 29); Man City 2023-24, Liverpool 2019-20 na Chelsea 2009-10 na 2005-06.

Pengine jambo muhimu zaidi ni kwamba timu zote nne ziliendelea kuongeza ushindi katika mfululizo wao wa mwanzo. Chelsea msimu wa 2009-10 na Man City 2023-24 ziliongeza ushindi mmoja zaidi (ushindi mara sita), wakati Liverpool (ushindi mara nane 2019-20) na Chelsea (mara tisa 2005-06) ziliweka mifululizo miwili mirefu zaidi ya ushindi wa klabu katika kuanza msimu wa Ligi Kuu England.

Tottenham Hotspur inashikilia rekodi ya ushindi mwingi zaidi mfululizo mwanzoni mwa msimu wa ligi ya daraja la juu, baada ya kushinda mechi zake 11 za kwanza 1960-61. Kwa kawaida, walitwaa ubingwa msimu huo.

Lakini, kuanza kwa ushindi hakuhakikishii mafanikio, kama Manchester United ilivyokuwa 1985-86. Licha ya kushinda mechi 10 za kwanza msimu huo (na kubaki bila kufungwa katika mechi 15 za mwanzo) chini ya kocha Ron Atkinson, Mashetani Wekundu waliporomoka na kumaliza msimu katika nafasi ya nne.


TANO KATI YA TANO

Mwanzo bora wa City msimu huu umesaidiwa na kuwa na ratiba mojawapo nyepesi katika mechi zake tano za kwanza za msimu wa 2026-27.

Kwa mujibu wa Opta, City ilikuwa na mwanzo wa pili kwa urahisi msimu huu, huku wapinzani wao wakiwa na wastani bora wa 91.2 kwa mujibu wa vipimo vya taasisi hiyo. Ni Liverpool pekee (91.1) ndiyo ilipewa mwanzo rahisi zaidi wa msimu na mfumo wa kompyuta wa upangaji ratiba wa Ligi Kuu England. Hata hivyo, kama wengi wanavyosema, hakuna mechi rahisi katika Ligi Kuu England, hivyo huenda mwanzo wa City haupaswi kupuuzwa.

Takwimu mojawapo ambayo huenda ikaipa City wasiwasi ni kwamba hakuna klabu kati ya saba zilizopita kuanza msimu wa Ligi Kuu England kwa ushindi wa mechi tano mfululizo ambazo ziliendelea hadi kutwaa ubingwa katika msimu huo. Ya hivi karibuni zaidi ilikuwa Liverpool msimu uliopita.

Mabingwa hao watetezi chini ya kocha Arne Slot waliishinda Bournemouth, Newcastle United, Arsenal, Burnley na Everton katika kuanza kampeni ya Ligi Kuu England 2025-26 kwa ushindi wa mechi tano mfululizo kabla ya kupoteza mechi nne mfululizo.

Ukweli kwamba Liverpool ilishinda nne kati ya mechi zake tano za kwanza kwa kufunga mabao baada ya dakika ya 83 au baadaye ulionyesha kuwa huenda mfululizo huo wa ushindi haukuwa endelevu kwa muda mrefu, na ndivyo ilivyothibitika.

Maswali kuhusu ubora wa ulinzi wa City katika mechi zake tano za kwanza msimu huu yameashiria uwezekano kwamba huo unaweza kuwa mfano mwingine wa mfululizo wa ushindi usioweza kudumu. Uwezo wao utajaribiwa mara Ligi Kuu England itakaporejea katika mechi ya sita ya msimu, ambapo watasafiri kwenda Anfield kucheza dhidi ya Liverpool, ambayo bado haijafungwa chini ya kocha mpya Andoni Iraola.

Nafasi ya chini zaidi ambayo timu imewahi kumaliza baada ya kushinda mechi zake tano za kwanza za msimu wa Ligi Kuu England ni ya sita (Newcastle United 1994-95), ingawa hilo lilitokea katika msimu uliokuwa na mechi 42.

Ukiangalia historia yote ya ligi ya daraja la juu England, mfululizo wa sasa wa City ni tukio la 40 la timu kushinda mechi zake tano za kwanza za msimu. Ni timu 14 tu kati ya 39 zilizotangulia ambazo ziliendelea hadi kutwaa ubingwa wa ligi (asilimia 36).


MABINGWA WA MWISHO WA EPL

Wastani wa pointi walizokusanya mabingwa wa Ligi Kuu England katika mechi zao tano za kwanza katika misimu 34 iliyopita ni 11.3, ambao ni zaidi ya pointi ambazo Arsenal ilikusanya ilipokuwa njiani kutwaa taji lake la kwanza baada ya miaka 22 msimu uliopita.

The Gunners ilikusanya pointi 10 katika mechi tano za kwanza msimu wa 2025-26, ikipoteza pointi tatu baada ya kufungwa na Liverpool huko Anfield katika mechi ya nne kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 nyumbani dhidi ya Man City katika mechi ya tano.

Kikosi cha kocha Mikel Arteta kimeanza msimu huu vizuri zaidi, kikikusanya pointi 12 kati ya 15, huku dosari pekee ikiwa ni kipigo cha kushangaza cha mabao 3-0 dhidi ya Brighton katika mechi ya tano. Idadi ndogo zaidi ya pointi ambazo mabingwa wa mwisho wa Ligi Kuu England wamewahi kukusanya katika mechi tano za kwanza ilikuwa katika msimu wa kwanza wa ligi hiyo, 1992-93.

Man United ilikusanya pointi saba pekee (ushindi mara mbili, sare moja na kupoteza mara mbili) katika mechi zake tano za kwanza, lakini kutokana na kuwepo kwa mechi nne za ziada za kucheza kwa sababu ya ligi hiyo kuwa na timu 22, kikosi cha Alex Ferguson kilikuwa na muda wa kurejea na kutwaa ubingwa.

Hakuna timu iliyowahi kutwaa taji la Ligi Kuu England katika msimu wa mechi 38 baada ya kukusanya chini ya pointi nane katika mechi zake tano za kwanza. United imetwaa ubingwa wa ligi mara nne baada ya kukusanya pointi nane kamili katika mechi zake tano za mwanzo za msimu (1998-99, 2002-03, 2007-08 na 2008-09), huku City ikifikisha rekodi hiyo pia msimu wa 2020-21. Tunachojaribu kusema ni kwamba, kwa mashabiki wa Hull City na Newcastle united bado inawezekana!

Hata hivyo, mabadiliko ya kushangaza zaidi kuwahi kufanywa na mabingwa katika historia ya ligi ya daraja la juu England huenda yakawa yale ya Sunderland msimu wa 1912-13, ambapo The Black Cats walishindwa kushinda mchezo wowote kati ya saba ya kwanza wakitoka sare mbili na kupoteza mitano, lakini waliendelea kutwaa taji la iliyokuwa Ligi Daraja la Kwanza (First Division) sawa na Ligi Kuu kwa sasa.

Kwa kuwa wakati huo ushindi ulikuwa ukitoa pointi mbili pekee (kwa mshindi), ilikuwa rahisi zaidi kwa timu kurejea baada ya mfululizo wa matokeo mabaya; hata hivyo, bado ulikuwa ujio mkubwa wa mafanikio baada ya mwanzo huo.