Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City kicheko, Man U inazama

Muktasari:

  • Mchezo ambao ulivutia mashabiki wengi zaidi ulikuwa ule wa Manchester United na Manchester City ambao ulimalizika kwa Mashetani Wekundu kupoteza kwa mabao 3-0.

LONDON, ENGLAND: LIGI Kuu England iliendelea wikiendi ambapo mchezo wa mapema ulikuwa kati ya Burnely na Liverpool uliomalizika kwa Majogoo kushinda bao 1-0 lililopatikana katika dakika za jiooni kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa na Mohamed Salah.

Mchezo ambao ulivutia mashabiki wengi zaidi ulikuwa ule wa Manchester United na Manchester City ambao ulimalizika kwa Mashetani Wekundu kupoteza kwa mabao 3-0.

Katika mechi hiyo iliyopigwa katika Uwanja wa Etihad, Man City ilijipatia mabao yake kupitia kwa Phil Foden na Erling Haaland aliyefunga mawili.

Huo ulikuwa ni mchezo wa 47 katika michuano yote kwa kocha Ruben Amorim tangu achukue usukani wa kuiongoza Man United na kati ya hiyo ameshinda 18, sare tisa na kupoteza 20.

Hali hiyo imemfanya kuwa kocha mwenye takwimu mbovu zaidi kuliko kocha yeyote aliyewahi kuifundisha timu hiyo baada ya kuondoka kwa Sir Alex Ferguson.

Ushindi huo uliiwezesha Man City kurudi katika mstari ukiwa ni wa pili wa ligi kushinda baada ya mchezo uliopita iliopoteza mbele ya Brighton kwa mabao 2-1.

Kwa sasa Man City inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi sita wakati Man United ikizidi kushuka chini hadi nafasi ya 14 ikiwa na pointi nne ilizokusanya baada ya kushinda mechi moja na sare moja.

Baada ya ushindi Liverpool imepanda hadi kileleni ikiwa na alama 12 baada ya kushinda mechi zote nne za mwanzo wa msimu huu.

Kabla ya kupanda kileleni, Arsenal ndio ilikuwa ikiongoza msimamo kwa pointi tisa ilizofikisha Jumamosi baada ya kuichapa Nottingham Forest kwa mabao 3-0.