Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamelodi, Kaizer Chiefs zikitupwa nje CAF

Muktasari:

  • Mshambuliaji wa Wiliete, Mabululu ndiye aliyefunga bao la kusawazisha na kuifanya Mamelodi ishindwe kuingia hatua ya makundi baada ya miaka 11 kupita tangu ilipoondolewa na TP Mazembe mwaka 2015. 

Raundi ya pili ya awali ya mashindano ya Klabu Afrika imekuwa chungu nchini Afrika Kusini kufuatia klabu mbili kubwa za huko, Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs zote kujikuta zikitolewa jana Ijumaa, Oktoba 23, 2026 tena zikiwa ardhi ya nyumbani.

Mamelodi Sundowns imetupwa nje baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Wiliete ya Angola kwenye Uwanja wa Masterpiece Moripe, Pretoria.

Matokeo hayo yamefanya Mamelodi kuondolewa kwa faida ya bao la ugenini walilopata Wiliete baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa suluhu nchini Angola.

Katika mchezo huo wenyeji Mamelodi ndiyo walikuwa wa kwanza kuandika bao la uongozi mapema katika dakika ya 11 kupitia kwa mshambuliaji Tashreeq Matthews.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Mamelodi iliondoka kifua mbele kwenda kwenye vyumba vya kubadilisha nguo kwa bao hilo moja.

Hata hivyo, mwanzoni mwa kipindi cha pili katika dakika ya 49, Wiliete ilipata bao la kusawazisha lililofungwa na mshambuliaji hatari Agostinho Cristóvão Paciência  'Mabululu'.

Bao la mshambuliaji huyo ndiyo lililoitupa nje Mamelodi ambayo hadi dakika 90 zinamalizika haikuweza kuongeza bao la uongozi na kuwafanya Wiliete kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Mara ya mwisho Mamelodi kushindwa kuingia  hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa msimu wa 2014/2015 ambapo iliondolewa na TP Mazembe kwa jumla ya mabao 3-1.

Kwenye Uwanja wa FNB jijini Johannesburg, wenyeji Kaizer Chiefs walitupwa nje ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupoteza kwa mikwaju ya penalti 3-2 dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Dakika 90 zilimalizika kwa Kaizer Chiefs kupata ushindi wa bao 1-0.

Kwa vile mechi ya kwanza nchini Zambia ilimalizika kwa Red Arrows kushinda kwa bao 1-0, ililazimu mikwaju ya penalti kutumika ili kutafuta mshindi.

Mikwaju hiyo ya penalti iligeuka shubiri kwa Kaizer Chiefs ambapo ilifunga mbili na kukosa tatu huku wapinzani wao wakifunga penalti tatu na kukosa mbili hivyo kusonga mbele.