Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kapera; Straika aliyepishana na mamilioni Msimbazi

KAPERA Pict

Muktasari:

  • Kapera ambaye aliibukia Majimaji FC ya mjini Songea wakati huo ikiwa daraja la kwanza (Championship), kwa mara ya kwanza msimu wa 2014/15, alikuwa na uwezo mkubwa kuzitoa mate timu nyingi. 

IKIWA imepita zaidi ya misimu mitano tangu kuondoka Kagera Sugar, Ramadhan Kapera anasema bado haamini kilichotokea kwenye dili lake la kujiunga na Simba dakika ya mwisho, akieleza kuwa anahisi ‘mkono’ wa mtu ulihusika.

Kapera ambaye aliibukia Majimaji FC ya mjini Songea wakati huo ikiwa daraja la kwanza (Championship), kwa mara ya kwanza msimu wa 2014/15, alikuwa na uwezo mkubwa kuzitoa mate timu nyingi. Hata hivyo msimu wa 2020/21 akiwa katika kiwango bora akiitumikia Kagera Sugar, alipokea ofa kutoka kwa Wekundu lakini katika hali isiyo ya kawaida na sintofahamu, dili hilo liliyeyuka kimyakimya.

Katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti, Kapera anayekipiga Songea United kwa sasa amefunguka mazito aliyopitia kwenye mpira na namna anavyojitafuta upya kuhakikisha kabla ya msimu huu 2026/27 kuisha arejee tena Ligi Kuu.


KAPE 01

AKWEPA KIFO

Katika msimu uliopita, straika huyo hakuonekana uwanjani hali iliyowapa maswali mengi wadau na mashabiki wa soka juu ya nyota huyo kukosekana katika majukumu yake tofauti na ilivyokuwa imezoeleka. Hata hivyo mchezaji huyo mwenye nguvu na akili ya mpira anaeleza kuwa kupotea kwake kutokana na ajali ya gari aliyoipata na kumpunguzia kasi.

Anasema baada ya kumaliza kusaini mkataba kuitumikia Polisi Tanzania mapema msimu uliopita, wakati anakwenda kujiandaa na majukumu yake, alipata ajali akienda nyumbani kwao mjini Songea.

“Ilikuwa kabla ya kuanza msimu wakati wa dirisha kubwa la usajili, baada ya kumaliza kusaini nikaona nirudi nyumbani kujipanga, nilikuwa na wenzangu ambapo tukiwa tunakaribia Songea mjini tukapata ajali,” anasema mchezaji huyo.

“Katika ajali ile haikujulikana sababu, kwakuwa ilikuwa usiku hivi sasa sikujua ni uchovu wa dereva au vinginevyo, ambapo mmoja alivunjika miguu na mwingine kufariki, mimi nikapata shida ya goti na kifua.”

Anaeleza kuwa kutokana na ajali hiyo, ilimfanya kuwa nje ya uwanja akiuguza maumivu hayo yaliyodumu kwa takribani mwaka mmoja lakini kwa sasa anashukuru Mungu afya imeimarika.


KAPE 02

UZOEFU MWINGI

Kapera anasema moja ya kitu anachojivunia kwenye kazi yake ya soka ni pamoja na uzoefu, uwezo na ushindani alionao kwenye mpira kutokana na kukutana na timu nyingi na wachezaji kibao.

Anasema tangu alipoanza mpira akitokea timu ya mtaani kwao, City Center ya mjini Songea alitambulishwa na Majimaji, kisha Polisi Moro, Kagera Sugar, KMC, Ihefu, Polisi Tanzania, Kitayosce, Ndanda, Mbeya Kwanza, Geita Gold, TMA na sasa Songea United.

“Maeneo yote nilicheza kwa mafanikio japokuwa yapo mengine matokeo ya jumla hayakuwa mazuri, lakini sina tatizo na uzoefu, kiwango na ubora wangu kwenye soka la ushindani,” anasema Kapera.


KAPE 03

KUSHUSHA TIMU

Penye mafanikio hayakosi changamoto, kwani licha ya makubwa aliyofanya Kapera katika timu alizotoka ikiwamo mchezaji bora, mfungaji bora na kuziokoa timu kadhaa kushuka daraja, vivyo hivyo zipo zilizoshuka akiwa nazo.

Tukio la kwanza ni kuinusuru Kagera Sugar kutoshuka daraja msimu wa 2020/21 kupitia mchujo (play off), alipoiongoza kushinda jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Pamba Jiji na kubaki salama Ligi Kuu.

Ikumbukwe msimu huu, mchezo wa kwanza ulishindwa kufanyika baada ya kutokea sintofahamu katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, kwa kile kilichodaiwa wenyeji kukataa matangazo mubashara.

KAPE 07

Hata hivyo mamlaka za soka ziliamua mchezo huo kupangiwa tarehe nyingine, ambapo matokeo ya awali jijini Mwanza ilikuwa suluhu ya bila kufungana kabla ya mechi ya pili Kagera Sugar akiwa mwenyeji mjini Bukoba kushinda 2-0.

Hata hivyo, tukio lingine ni msimu wa 202/23 ambapo KMC ikiwa katika presha ya kushuka daraja, bao pekee la Kapera huko Tuliani mkoani Morogoro lilitosha kuinusuru timu hiyo kutoshuka dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ukiachana na historia hiyo, Kapera anaingia kwenye rekodi pia ya kushuka na timu, akianza na Ndanda FC, Geita Gold, Polisi Tanzania na Majimaji FC huku akiwa anasaka rekodi mpya ya kupandisha timu daraja.


KAPE 04

ALIZWA SIMBA

Katika mazungumzo na Mwanaspoti, Kapera anasema hawezi kusahau tukio la dili lake kuyeyuka dakika za mwisho alipokuwa amalizane na Simba, lakini katika hali ambayo hakuielewa ishu haikufikia mwisho mzuri.

Anafafanua kuwa wakati anamalizia msimu Kagera Sugar mchezo wa mwisho wa play off dhidi ya Pamba Jiji, alikuwa na tiketi ya ndege, ambapo baada ya mchezo alisafiri kwenda Dar es Salaam.

Anabainisha kuwa wakati wa dili lote, alikuwa akiwasiliana mara chache na mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ ambaye walikuwa na mazungumzo mazuri kuanzia ofa hadi maslahi mengine.

“Tulikuwa tukiwasiliana na Mo kupitia WhatsApp, akaniambia atanipa Sh40 milioni na pikipiki nne, ila akawa anasema afya yake haiko sawa, hivyo nikifika Dar es Salaam nitakutana na watendaji wake tumalize kazi,” anasema mchezaji huyo na kuongeza:

KAPE 06

“Sasa katika hali ya sintofahamu baada ya kufika niliowakuta wakaniambia wanipe Sh20 milioni, lakini watatanguliza Sh10 milioni nisaini, nikajiuliza kimyakimya sikupata majibu.

“Nilichogundua ni aidha haikuwa bahati na riziki yangu au kuna mkono wa mtu ambaye aliamua kivyake kuharibu mchongo, kiujumla hadi sasa nikikumbuka mazingira yale inaniumiza sana.”

Anasema kama ilivyo wachezaji wengi ndoto zao kucheza timu kubwa ili kuonekana na kufika mbali hata yeye alitamani kufanya hivyo ila haikuwezekana kwa uamuzi wa ‘mtu kati’ kwa maslahi binafsi.


KAPE 05

LIBASE, ABUYA WAMKUNA

Kapera anasema amekutana na mastaa wengi kwenye soka walioonesha ubora mkubwa, wakiwamo Juma Nyoso, Abdalah Shaibu ‘Ninja’ na Kelvin Yondani lakini kwa sasa wapo wawili anawakubali.

Anasema wachezaji Neo Maema na Libase Gueye (Simba) na Duke Abuya ni moja na nyota wanaomvutia kutokana na ubora na uwezo wao wa soka uwanjani pamoja na Kenny Ally na Charles Ilanfya.

“Sikutamani kukutana na Ninja kipindi akiwa Yanga, jamaa alikuwa anazima haswa, lakini kwa sasa kuna Gueye, Maema na Abuya wanafanya kazi nzuri mno, miaka ya nyuma Nyoso na Yondani walitesa mno,” anasema Kapera.