Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama Ronaldo acharuka

MAMA Pict

Muktasari:

  • Aveiro ameonesha kutoridhishwa na namna Ronaldo alivyoshughulikiwa ndani ya kikosi cha Ureno, huku akitoa kauli kali baada ya timu hiyo kufungwa mabao 4-1 na Denmark katika mchezo wa kimataifa uliochezwa bila uwepo wa nahodha huyo wa zamani.

LISBON, URENO: MAMA wa supastaa Cristiano Ronaldo, Maria Dolores dos Santos Aveiro, amezua mjadala mzito baada ya kumshambulia kocha wa timu ya taifa ya Ureno, Jorge Jesus, kufuatia kile alichodai kuwa mwanawe hakutendewa haki kabla ya kuamua kustaafu soka la kimataifa.

Aveiro ameonesha kutoridhishwa na namna Ronaldo alivyoshughulikiwa ndani ya kikosi cha Ureno, huku akitoa kauli kali baada ya timu hiyo kufungwa mabao 4-1 na Denmark katika mchezo wa kimataifa uliochezwa bila uwepo wa nahodha huyo wa zamani.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sporting, mama huyo amesema mwanawe aliumizwa na namna mambo yalivyokwenda, akidai hakuheshimiwa na hata baadhi ya wachezaji wenzake.

MAM 01

"Ni wazi kwamba alihuzunika. Walimdanganya. Na mimi pia nina huzuni. Walistahili kufungwa. Nilifurahi kuona matokeo hayo," amesema Aveiro.

Aliendelea kwa kusema: "Katika timu ya taifa, hakuheshimiwa, hata na wachezaji wenzake."

Kauli hizo zimekuja baada ya mgogoro kati ya Ronaldo na kocha Jorge Jesus, ambao ulianza kufuatia namna mshambuliaji huyo alivyotumiwa katika mchezo dhidi ya Norway mwezi Septemba.

Ronaldo alikerwa baada ya kuachwa benchi licha ya kufanya mazoezi ya kujipasha moto, jambo ambalo lilikuwa la kwanza kwake katika kipindi cha miaka 23 ya kuitumikia timu ya taifa.

Baada ya tukio hilo, nyota huyo aliripotiwa kukosa mazoezi matatu na kuondoka kambini kabla ya michezo miwili iliyofuata ya mapumziko ya kimataifa.

MAM 02

Inadaiwa aliondoka kwa ndege binafsi kuelekea Hispania akiwa na familia yake, bila hata kutazama mchezo uliofuata wa Ureno.

Akijibu kauli za mama huyo kabla ya mchezo dhidi ya Wales, Jesus amesema anamheshimu Aveiro na kuelewa hisia zake kama mzazi.

"Sasa ninapaswa kumjibu mama wa Cristiano Ronaldo? Ni mwanamke ninayemheshimu sana. Mama ni mama, na ninaelewa kauli zake," amesema Jesus.

Ameongeza: "Mama humtetea mtoto wake hata kwa gharama yoyote. Huyo ni mama mwenye thamani kubwa ambaye ameteseka sana kuwalea watoto wake."

Hata hivyo, Jesus alisisitiza kuwa hajioni kuwa na hatia kuhusu uamuzi wa Ronaldo kuachana na timu ya taifa.

"Sijisikii kuwa na hatia yoyote kuhusu kuondoka kwake. Ninaheshimu uamuzi wake na historia yake haiwezi kupuuzwa. Daima atabaki kuwa alama muhimu katika historia ya soka," amesema.

MAM 03

Mgogoro huo ulitokana na madai ya Ronaldo kwamba kocha huyo alivunja ahadi ya kumpa dakika 30 za kucheza dhidi ya Norway, baada ya awali kumshawishi asiache kuichezea timu ya taifa baada ya Kombe la Dunia.

Ronaldo alidai pia Jesus alipaswa kuomba radhi kwa mashabiki wa Ureno na wachezaji wenzake kwa kumwacha benchi.

Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or alitoa tamko kali la maneno 1,996 akimshutumu kocha huyo kwa kuvunja ahadi.

Kwa upande wake, Jesus alikiri kuwa kumtaka Ronaldo apashe moto misuli huku akimuacha benchi lilikuwa kosa, lakini alisisitiza kuwa mchezaji huyo alielewa uwezekano wa kutumiwa katika mchezo huo.

Ronaldo anamaliza safari yake ya kimataifa akiwa amecheza mechi 234 na kufunga mabao 146, rekodi inayomfanya kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo.