Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hapa Neves na Madalena, kule Ronaldo na Georgina!

Muktasari:

  • Neves na Madalena waliweka wazi uhusiano wao Septemba 19, 2024, baada ya kila mmoja kuposti picha akiwa na mwenzake kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. Wakati huo, wote wawili walikuwa na umri wa miaka 19.

Staa wa Paris Saint-Germain (PSG) na timu ya taifa ya Ureno, Joao Neves, kwa miaka zaidi ya miwili amekuwa katika uhusiano na mwigizaji wa nyumbani kwao, Madalena Aragao ambaye walifahamiana kabla kwenda Ufaransa kucheza soka.

Neves na Madalena waliweka wazi uhusiano wao Septemba 19, 2024, baada ya kila mmoja kuposti picha akiwa na mwenzake kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii. Wakati huo, wote wawili walikuwa na umri wa miaka 19.

Tetesi kuhusu uhusiano wao zilianza Julai 2024 baada ya wawili hao kuonekana pamoja huko mjini Tavira, eneo ambalo anatokea Neves, na baadaye walionekana wakitazama mechi ya Benfica.

Utakumbuka Neves alianza kujijengea jina kupitia akademi ya Benfica kabla ya kupata nafasi katika kikosi cha kwanza. Uwezo wake ulizivutia baadhi ya klabu kubwa Ulaya na hatimaye Agosti 2024, PSG ilimsajili.

Tangu wakati huo, Madalena amekuwa akisafiri mara kwa mara kwenda jijini Paris kumshuhudia mpenzi wake huyo akiichezea PSG. Aliwahi kueleza kuwa umbali uliopo kati yao haujawahi kuwa kikwazo katika uhusiano wao.

Baada ya PSG kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mnamo Mei 2026, Madalena aliposti ujumbe maalumu wa kumpongeza Neves kwa mafanikio hayo makubwa ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwa klabu hiyo kutwa taji hilo.

Kuanzia kukutana kwao kwa mara ya kwanza jijini Lisbon hadi kuonekana pamoja kwenye matukio mbalimbali ya michezo, Neves na Madalena wameendelea kuvutia hisia za mashabiki wa soka.

Madalena ni mwigizaji na mwongozaji wa filamu kutokea Ureno, alianza kujihusisha na tasnia ya filamu tangu akiwa mtoto, ambapo alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka 10 na kujijengea jina katika filamu na vipindi vya televisheni nchini humo.

Ameshiriki katika tamthilia za TVI zikiwemo Para Sempre na Quer o Destino, pamoja na kupata nafasi ya kuongoza tamthilia ya vijana ya Morangos com Acucar ya TVI, ambayo ilianza kurekodiwa Aprili 2023.

Mwaka huohuo, Jarida la Forbes Portugal lilimtaja Madalena katika orodha ya vijana waliofanikiwa wakiwa chini ya umri wa miaka 30. Hivyo wakati Neves akiendelea kujenga jina lake katika soka akiwa PSG, Madalena naye anaendelea na shughuli zake katika tasnia ya burudani.

Hata hivyo, katika hali isiyotarajiwa Neves na Madalena walijikuta wakiwa kitimoto mtandaoni na mashabiki wa Cristiano Ronaldo, ambaye ni nahodha wa kikosi cha Ureno.

Baada ya mchezo wa Kombe la Dunia 2026 kati ya Ureno na DR Congo kumalizika kwa sare ya magoli 1-1, ambapo Neves alifunga goli pekee la Ureno, maelezo yake kuhusu Ronaldo baada ya mchezo huo hayakuwafurahisha mashabiki wa staa huyo.


Ingawa Neves alisifia mchango na historia ya Ronaldo katika soka, pia alisema kuwa mshambuliaji huyo mkongwe kwa sasa ni mchezaji mwingine kabisa ndani ya kikosi cha timu hiyo, akimaanisha uwezo wake wa sasa ni tofauti na mwanzo.

Baadhi ya mashabiki wa Ronaldo walitafsiri kauli hiyo kama dharau dhidi ya gwiji huyo ambaye anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Ureno.

Kufuatia kauli hiyo, Neves na Madalena walijikuta wakipewa vidonge vichungu na mashabiki wa Ronaldo kupitia mitandao ya kijamii. Mashabiki hao walionyesha hasira kutokana na kile walichokiona kuwa ni kumkosea heshima Ronaldo.

Hali hiyo ilipelekea wawili hao kufunga sehemu ya mashabiki kutoa maoni yao ili kujilinda dhidi ya usumbufu huo, huku post za Neves ambazo alikuwa hajafanya hivyo zikipokea comments zaidi ya 180,000.

Mvutano huo ulizidi kushika kasi baada ya screenshot moja kuanza kusambazwa mitandaoni, ikidaiwa kuonyesha Madalena akimtukana Ronaldo na kumtaka astaafu soka.

Ujumbe huo uliokuwa na maneno makali dhidi ya Ronaldo baadaye ulibainika kuwa wa uongo kabisa na ulikuwa umetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde (AI).

Licha ya screenshot hiyo kuwa feki, bado ujumbe huo ulisambaa kwa kasi kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii, hali iliyozidisha hasira za mashabiki na kuugeuza mzozo huo kuwa gumzo kubwa. Mzozo huo ulizidi kuwa mkubwa zaidi baada ya mke wa Ronaldo, Georgina Rodriguez kutoa maoni yake kuhusu picha hiyo feki. Wakati huo, Georgina aliandika ujumbe mtandaoni uliyoashiria kuwa aliamini picha hiyo.   “Wow! Kizazi hiki kimekuja kwa kasi sana!”€  aliandika Georgina huku akiambatanisha na alama (emoji) za kucheka. Hata hivyo, inadaiwa kuwa viongozi wa timu ya taifa ya Ureno waliona tukio hilo kama mzozo usiokuwa na maana hivyo hawakuchukua hatua zozote zaidi ya kuandelea kuiandaa timu na michuano hiyo.