Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majogoo watenga Pauni 250 milioni, Alvarez atajwa

TETESI Pict

Muktasari:

  • Katika orodha hii miongoni mwa mastaa ambao wanaonekana kuwa huenda wakawagharimu kiasi kikubwa cha pesa ni pamoja na Alvarez ambaye mkataba wake na Atletico unamalizika mwaka 2030 na msimu huu amecheza mechi 44 za michuano yote na kufunga mabao 23.

LIVERPOOL imepanga kutumia zaidi ya Pauni 250 milioni dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ajili ya kuboresha kikosi chao NA ina mpango wa kusajili mastaa kadhaa ikiwemo straika wa Atletico Madrid na Argentina, Julian Alvarez, 25, kiungo wa RB Leipzig na Uholanzi, Xavi Simons, 21, na beki wa Inter Milan na Italia, Alessandro Bastoni, 25.

Katika orodha hii miongoni mwa mastaa ambao wanaonekana kuwa huenda wakawagharimu kiasi kikubwa cha pesa ni pamoja na Alvarez ambaye mkataba wake na Atletico unamalizika mwaka 2030 na msimu huu amecheza mechi 44 za michuano yote na kufunga mabao 23.

Vigogo wa Liverpool wametenga kiasi hicho cha pesa kwa sababu baadhi ya wachezaji wao wengi muhimu ikiwemo Mohamed Salah, Trent Alexander Arnold na Virgil van Dijk watakuwa wanamaliza mikataba mwisho wa msimu huu na hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote yanayoashiria kwamba wamefikia mwafaka wa kubakia.


Alexander Isak

LIVERPOOL wamefanya mawasiliano na watu walioko karibu na mshambuliaji wa Newcastle na Sweden, Alexander Isak,  25, ili kuona ikiwa inaweza kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Isak ambaye msimu huu amecheza mechi 33 za michuano yote na kufunga mabao 23, Mkataba wake na Newcastle unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Hata hivyo, mabosi wa Newcastle wana uhakika nyota huyo hatoondoka mwisho wa msimu.


Marcus Rashford

INAELEZWA Manchester United imeongeza bei ya mshambuliaji wao na timu ya taifa ya England, Marcus Rashford, 27 dirisha lijalo la majira ya kiangazi baada ya kiwango bora alichoonyesha akiwa na Aston Villa kiasi cha kusababisha aitwe kwenye kikosi cha timu ya taifa. Rashford ambaye alijiunga na Villa kwa mkopo wa nusu msimu, anaweza kuuzwa kwa zaidi ya Pauni 70 milioni na kuna uwezekano mkubwa akanunuliwa jumla na Villa.


Diogo Jota

WOLVES wanaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wao wa zamani raia wa Ureno, Diogo Jota ambaye hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Liverpool. Mabosi wa Wolves wana matumaini makubwa ya kumsajili Jota kwa sababu haonekani kuwa kwenye mipango ya kocha wa majogoo. Msimu huu Jota amecheza mechi 29 za michuano yote na hajawa na kiwango kizuri Anfield.


Kyle Walker

AC Milan inataka kumsainisha mkataba wa kudumu beki wa Manchester City na timu ya taifa ya England, Kyle Walker, 34, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika kikosi chao. Milan imevutiwa sana na kiwango cha Walker lakini mbali ya kutaka kumbakisha Walker, wababe hawa pia wanataka kumsainisha mkataba wa kudumu Joao Felix ambaye anawatumikia kwa mkopo akitokea Chelsea.


Jeremie Frimpong

BEKI wa Bayer Leverkusen na Uholanzi, Jeremie Frimpong ni mmoja wa mabeki wanaopewa kipaumbele zaidi na kocha wa Liverpool, Arne Slot kwenda kuchukua nafasi ya Trent Alexander Arnold ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho wa msimu huu. Trent anadaiwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kuachana na Liverpool kutokana na ofa kubwa aliyowekewa mezani na Real Madrid.


Antonio Cordero

NEWCASTLE United inapewa nafasi kubwa ya kuzipiku Real Madrid na Barcelona dili la kuiwania saini ya mshambuliaji wa Malaga na Hispania, Antonio Cordero, 18, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Cordero amepanga kujiunga Newcastle badala ya Barca na Madrid kwa sababu anaamini atapata nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.


Marc Guehi

LIVERPOOL inadaiwa kufikia makubaliano na wawakilishi wa beki wa Crystal Palace, Marc Guehi kwa ajili ya kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Kabla ya kufikia makubaliano ya kumsajili fundi huyu, Liverpool imeshinda vita dhidi ya timu nyingine kama Newcastle, Tottenham na Chelsea. Mkataba wake unamalizika mwaka 2026.