Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mainoo atakiwa kwa mkopo wa miezi sita

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • West Ham United inataka kukamilisha dili hilo la usajili kwenye dirisha la Januari litakapofunguliwa.

WEST Ham United imeripotiwa kuwa na mpango wa kumpa kiungo wa Manchester United, Kobbie Mainoo kichaka cha kukimbilia ikimhitaji kwa mkopo wa miezi sita baada ya kuwa na wakati mgumu huko Old Trafford.

West Ham United inataka kukamilisha dili hilo la usajili kwenye dirisha la Januari litakapofunguliwa.

Kiungo huyo wa England ameweka wazi juu ya mpango wa kuondoka Man United mwishoni mwa msimu huu kutokana na kocha Ruben Amorim kushindwa kumpa muda wa kutosha uwanjani.

Lakini, sasa West Ham inataka kumwokoa mapema kutoka kwenye benchi, ikihitaji huduma yake kwenye dirisha la Januari, ili akacheze kwenye timu yao kwa mkopo wa miezi sita hadi mwisho wa msimu.

Bado Man United haijaonyesha dhamira ya kumwaachia Mainoo, licha ya kudaiwa kuwa na mpango wa kuingia sokoni Januari ili kwenda kunasa viungo wengine.

Kocha Amorim, amekuwa akiwapa muda wa kutosha viungo Bruno Fernandes na Casemiro na kumweka benchini Mainoo, huku akiwa chaguo la nne nyuma ya Manuel Ugarte.


Elliot Anderson

MANCHESTER United imeripotiwa kuweka kipaumbele chao kwenye usajili ujao wa dirisha la Januari kwamba itavamia Nottingham Forest kwenda kunasa huduma ya kiungo, Elliot Anderson. Staa huyo wa England mwenye umri wa miaka 23, anatazamwa na Man United kama mchezaji muhimu katika mipango yao ya kuimarisha eneo la kiungo ili kuweza kushindana kwenye michuano mbalimbali ikiwamo Ligi Kuu England.


Ivan Toney

MKURUGENZI wa michezo wa klabu ya Al-Ahli ya Saudi Arabia, Rui Pedro Braz, amesema kwamba mshambuliaji wa England, Ivan Toney, hataruhusiwa kuhama timu hiyo kwenye dirisha lijalo la Januari. Kwa muda sasa, Toney, 29, amekuwa akihusishwa na mpango wa kuachana na timu hiyo ya Saudia wakati dirisha la Januari litakapofungulia, lakini kwa mujibu wa bosi huyo wa Al-Ahli, dili hilo haliwezi kufanyika.


Robert Lewandowski

STRAIKA wa Poland, Robert Lewandowski amesema hana muda mrefu atafanya uamuzi wa kutambua hatima ya maisha yake baada ya kuachana na Barcelona. Mkataba wa fowadi huyo wa zamani wa Borussia Dortmund na Bayern Munich huko Barcelona utafika tamati majira ya kiangazi ya mwaka, hivyo atahitaji kufanya uamuzi mapema kufahamu atafanya kitu gani atakapong’oka Nou Camp.



Takefusa Kubo

TOTTENHAM Hotspur imeripotiwa kuwa na mpango wa kumsajili winga wa Kijapani, Takefusa Kubo kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa Januari. Spurs inamtazama mkali huyo wa Real Sociedad kuwa mwafaka kwenye mipango yao, wakiamini atakwenda kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji ili kutimiza mipango yao ya kuhakikisha inamaliza nafasi za juu kwenye ligi msimu huu.


Niclas Fullkrug

WEST Ham United imeripotiwa kufungua milango ya kumpiga bei straika wa Kijerumani, Niclas Fullkrug kwenye dirisha la Januari. West Ham, haitaki kuweka ngumu kwa fowadi huyo mwenye umri wa miaka 31, endapo kama kutakuwa na timu itakayohitaji saini yake kwenye dirisha la Januari, huku yenyewe ikiweka mpango wa kumpiga bei ili kutua nafasi ya kuleta fowadi mwingine kwenye kikosi hicho cha London.


Ibrahima Konate

BEKI wa kati wa Liverpool, Ibrahima Konate ameripotiwa kufunguka bado hajapokea ofa yoyote ya kuhusu mkataba mpya kutoka kwa klabu yake hiyo. Kauli hiyo ya Konate inakuja siku chache tangu ilipoibuka taarifa Real Madrid inahitaji huduma yake ili akakipige Bernabeu. Mkataba wa Konate Anfield utafika tamati mwishowa msimu huu, huku Bayern Munich pia ikidaiwa kumhitaji.


Antoine Semenyo

MANCHESTER City imeripotiwa kumfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo ili kunasa saini yake kwenye dirisha la Januari. Hata hivyo, huduma yake haitakuwa nyepesi kwa Man City kuipata kutokana na kuwapo na klabu nyingine za Ligi Kuu England ikiwamo Liverpool na Tottenham zikihitaji huduma ya mchezaji huyo, 25.