Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea yaandaa mkwanja wa maana ili kumnasa Alvarez

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Alvarez mwenye umri wa miaka 25, ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Atletico Madrid na amekuwa akihusishwa na timu za England tangu dirisha lililopita la usajili.

CHELSEA inajiandaa kuwasilisha ofa ya takriban Euro 150 milioni kwa ajili ya kumsajili straika wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Argentina, Julian Alvarez, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Alvarez mwenye umri wa miaka 25, ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Atletico Madrid na amekuwa akihusishwa na timu za England tangu dirisha lililopita la usajili.

Kiasi hicho cha Euro 150 milioni kinadaiwa ndicho kimewekwa katika mkataba wake ikiwa kuna timu inahitaji kuuvunja.

Alvrez aliyejiunga na Atletic Madrid 2024 baada ya kuchoka kutumika akiwa mbadala wa Erling Haaland, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2030 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 18 za michuano yote na kufunga mabao tisa. Katika mabao hayo tisa, saba amefunga La Liga ambapo amecheza mechi 12 msimu huu.


Karim Adeyemi

MANCHESTER United inapanga kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Ujerumani, Karim Adeyemi, 23, katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Taarifa zinaeleza Man United inataka kumtumia Sancho na pesa kiduchu kama sehemu ya ofa baada ya kuona hivi karibuni Dortmund imeonyesha nia ya kuhitaji huduma yake. Hata hivyo, Dortmund haitaki kufanya mabadilishano badala yake inataka pesa..


Joao Gomes

KATIKA kuhakikisha inaboresha zaidi eneo la kiungo, Manchester United imepiga hodi  Wolves na kuulizia uwezewekano wa kuipata huduma ya kiungo wa timu hiyo, Joao Gomes mwenye umri wa miaka 24. Staa huyo wa kimataifa wa Brazil anaonekana kuvutiwa na mpango wa kujiunga na Mashetani Wekundu na kinachosubiriwa ni timu kufikia makubaliano ya ada za uhamisho, na ikiwa hilo litafanikiwa Gomes anaweza kutua Old Trafford Januari, mwakani.


Antoine Semenyo

LIVERPOOL na Tottenham Hotspur zinapigana vita vya chinichini kuwania saini ya mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo, 25, kwa ajili ya kuboresha safu ya ushambuliaji. Taarifa zinadai Semenyo aliomba kuondoka dirisha lililopita la usajili, lakini Bournemouth ilikataa na kumtaka acheze msimu huu kisha itamruhusu. Mkataba wa Semenyo unatarajiwa kumalizika 2030.


Kees Smit

NEWCASTLE United inaripotiwa kuwa katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa AZ Alkmaar, Kees Smit, 19, dirisha lijalo la majira ya baridi. Katika mchakato wa kuiwania saini yake Newcastle United inakumbana na upinzani mkali kutoka Barcelona, Bayern Munich, Borussia Dortmund na Real Madrid ambazo zinaitaka saini ya staa huyo. Hata hivyo, Newcastle inaonekana kuwasilisha ofa nono.


Daizen Maeda

BRENTFORD, Everton na Leeds zinapambana kuwania saini ya mshambuliaji wa Celtic na timu ya taifa ya Japan, Daizen Maeda, 28, ambaye zinatamani kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Maeda ni miongoni mwa washambuliaji bora katika Ligi Kuu Scotland ba Celtic inatajwa kutaka zaidi ya Pauni 40 milioni ili kimuuza. Timu tajwa za England zinahitaji saini ya mshambuliaji huyo ili kuboresha safu ya ushambuliaji.


Joshua Zirkzee

ROMA inapambana kutaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya Uholanzi, Joshua Zirkzee kwa mkopo katika dirisha lijalo la majira ya baridi, lakini inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Everton, West Ham United, Juventus na PSV  ambazo pia zinamtaka. Zirkzee hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Man United.


Endrick

KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Carlo Ancelotti amekanusha kumshawishi staa wa taifa hilo, Endrick, 19, kuondoka Real Madrid ili atue Lyon katika dirisha lijalo la majira ya baridi ili apate nafasi ya kucheza na hatimaye amjumuishe katika kikosi cha Brazil kitachoshiriki Kombe la Dunia mwakani. Endrick anatajwa kujiunga na Lyon kwa mkopo wa nusu msimu.