Real Madrid yampigia hesabu Enzo Fernandez
Muktasari:
- Fernandez ni miongoni mwa wachezaji ghali wa Chelsea tangu Februari 2023, alipojiunga na klabu hiyo akitokea Benfica kwa ada ya Pauni 106 milioni.
CHELSEA imeiambia Real Madrid ipo tayari kumuuza kiungo wao wa kimataifa wa Argentina, Enzo Fernandez mwenye umri wa miaka 25, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.
Fernandez ni miongoni mwa wachezaji ghali wa Chelsea tangu Februari 2023, alipojiunga na klabu hiyo akitokea Benfica kwa ada ya Pauni 106 milioni.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Argentina, ambaye alishinda Kombe la Dunia 2022 na Copa America 2024, tangu wakati huo amekuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Chelsea.
Hata hivyo, inaelezwa Chelsea wako tayari kuachana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye alitwaa taji la UEFA Conference League msimu uliopita na Kombe la Dunia la Klabu 2025.
Chelsea inataka kumuuza staa huyo kwa sababu inaamini itapata kiasi kikibwa cha pesa ambacho kitawasaidia kufanya usajili na kurekebisha mahesabu katika vitabu vyao ili kuepukana na shida za kanuni za masuaka ya kifedha.
Vyanzo kutoka Real Madrid vimesema Chelsea imeonyesha dalili zote za kuwa tayari kumuuza Fernandez, lakini kwa bei kubwa inayodaia kufikia Pauni 120 milioni.
Staa huyu amekuwa akiwindwa na Madrid tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi na mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2032.
Joao Gomes
MANCHESTER United imepanga kufanya kila linalowezekana kuhakikisha inamsajili kiungo wa Wolves, Joao Gomes dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Napoli na Atletico Madrid ni miongoni mwa timu zinazohitaji huduma ya staa huyu ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030. Mabosi wa Wolves wanaamini ni ngumu kumbakisha Gomes mwenye umri wa miaka 24, lakini inataka hata akiuzwa auzwe kwa pesa nyingi.
Elliot Anderson
VIUNGO wawili raia wa England, Elliot Anderson, 23, kutoka Nottingham Forest na Adam Wharton, 21 wa Crystal Palace ni miongoni mwa mastaa ambao Manchester United inafikiria kuwasajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi.
Man United inaamini mastaa hawa vijana watakuwa sehemu ya mipango ya muda mrefu ya kujenga kikosi chao hivyo ikiwapata watakuwa na mchango mkubwa.
Jean-Philippe Mateta
CRYSTAL Palace imekataa ofa ya kwanza ya Juventus iliyoiwasilishwa kwa ajili ya kumsajili straika wao wa kimataifa wa Ufaransa, Jean-Philippe Mateta mwenye umri wa miaka 28.
Mateta ni miongoni mwa washambuliaji ambao Juventus inatamani sana kuwasajili kwa ajili ya kuziba pengo la staa wao Dusan Vlahovic ambaye kuna asilimia kubwa akaondoka dirisha lijalo la majira ya kiangazi na vigogo wengi Ulaya wanaonekana kuhitaji huduma yake.
Tangu kuanza kwa msimu huu Mateta amecheza mechi 33 za michuano yote na kufunga mabao 10. Barcelona wamwangalia Arteta na Luis Enrique
Pablo Garcia
BOURNEMOUTH na West Ham zimeingia vitani kuiwania saini ya winga chipukizi wa Real Betis na timu ya taifa ya Hispania, Pablo Garcia, 19.
Klabu hizo mbili za EPL zipo tayari kulipa kipengele cha kuvunja mkataba cha Pauni 26 milioni ili kumnunua mchezaji huyo ambaye ameonyesha pia kutaka kuondoka baada ya timu hizo za England akiamini ataenda kupata soka la kiushindani zaidi pia kucheza katika ligi hiyo ni moja kati ya ndoto zake. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2029.
Patrick Wimmer
EVERTON na Fulham zinadaiwa zinaongoza katika mbio za kumsajili winga wa Wolfsburg na timu ya taifa ya Austria, Patrick Wimmer, 24.
Wolfsburg wapo tayari kusikiliza ofa kutoka kwa timu yoyote inayohitaji huduma ya fundi huyo lakini itamuuza kwa dau nono pekee.
Ushindani huu kati ya Everton na Fulham unatarajiwa kuifanya bei ya Wimmer kupanda zaidi na anaweza akauzwa kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Jeremy Monga
CHELSEA na Manchester City zimeingia vitani kutaka kumsajili winga chipukizi wa Leicester City, Jeremy Monga, 16, dirisha hili.
Monga ambaye ni miongoni mwa wachezaji vijana walioibuka katika kikosi cha Leicester kuanzia mwaka jana, amekuwa akifuatilia pia na maskauti wa timu za nje ya England ambazo zinaonekana kutaka kumsajili ingawa Chelsea na Man City ndio zinapewa nafasi kubwa ya kuipata huduma yake kwa sababu tayari zimeshaanza hadi mazungumzo na familia yake ambayo ndio inamsimamia kwa sasa.
Nathan Patterson
SEVILLA imeingia rasmi katika mbio za kumsajili beki wa kulia wa Everton na timu ya taifa ya Scotland, Nathan Patterson, 24, katika dirisha hili.
Patterson ameomba kuondoka Everton katika dirisha hili ili kupata timu itakayompa nafasi kubwa zaidi ya kucheza tofauti na ilivyo sasa.
Sevilla inamwona kama chaguo bora la kuimarisha safu yao ya ulinzi, hasa kutokana na uwezo wake wa kupandisha mashambulizi mbali ya kukaba.