Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afrika Kusini na hesabu za vidole

BANYANA Pict

Muktasari:

  • Banyana Banyana ilianza kampeni kwa kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa  Tanzania, matokeo ambayo Kocha Desiree Ellis alikiri yalisababishwa zaidi na kushindwa kutumia nafasi walizopata.

NI hesabu za vidole tu, Afrika Kusini imejikuta ikipigana na hesabu ngumu za kusaka robo fainali ya WAFCON 2026 baada ya kuanza vibaya mashindano hayo, huku mechi yake ya mwisho dhidi ya Burkina Faso ikiwa imebeba matumaini.

Banyana Banyana ilianza kampeni kwa kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa  Tanzania, matokeo ambayo Kocha Desiree Ellis alikiri yalisababishwa zaidi na kushindwa kutumia nafasi walizopata.

“Walipata nafasi mbili na wakafunga zote na kushinda. Tulijua kabla mechi ingekuwa mgumu, pia tulijifanyia maisha kuwa magumu,” alisema Ellis baada ya mechi hiyo na kusisitiza kila mchezo uliokuwa mbele yao ungekuwa mgumu na hawakuwa na nafasi ya kupoteza pointi nyingine.

Hata hivyo, katika mechi iliyofuata dhidi ya Ivory Coast Banyana Banyana ilitoka sare ya mabao 2-2, yaliyofungwa na Thembi Kgatlana na Hildah Magaia.

Kocha alisema makosa ya kutotumia nafasi vizuri yamekuwa yakijirudia kwenye kikosi chake na kwa muda uliobaki wanapambana kurekebisha ili angalau kupunguza tatizo hilo.

"Tumekuwa na changamoto ya kutumia nafasi hii mechi ya pili mfululizo sasa, tutakaa kuangalia kwa muda uliobaki wapi tunaweza kusaidia iliangalau tupunguze tatizo hilo."

Sare hiyo imeifanya Afrika Kusini kuwa na pointi moja mkiani mwa kundi B, baada ya mechi mbili, huku Ivory Coast ikiwa kileleni na pointi nne, Tanzania ikiwa na pointi tatu na Burkina Faso ikiwa na pointi tatu.

Ikiwa Afrika Kusini itaifunga Burkina Faso mechi ya mwisho itafikisha pointi nne hivyo ina nafasi ya kumaliza nafasi ya pili kama Tanzania itapoteza mechi ya mwisho.

Burkina Faso nayo inaingia kwenye pambano hilo ikiwa na pointi tatu baada ya kuifunga Tanzania 2-1, hivyo haitakuwa mechi rahisi kwa mabingwa hao watetezi.