Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mainoo akumbuka magumu United

Muktasari:

  • Mainoo ambaye alionekana kuwa moja ya vipaji vinavyong’aa baada ya kupandishwa kikosi cha kwanza chini ya Erik ten Hag, alisema maendeleo yake yalikwama ghafla baada ya mabadiliko ya benchi la ufundi.

MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO wa Manchester United, Kobbie Mainoo, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu changamoto alizopitia baada ya kupoteza nafasi kikosini chini ya kocha wa zamani Ruben Amorim kabla ya kurejea kwenye kiwango bora chini ya kocha wa muda Michael Carrick.

Mainoo ambaye alionekana kuwa moja ya vipaji vinavyong’aa baada ya kupandishwa kikosi cha kwanza chini ya Erik ten Hag, alisema maendeleo yake yalikwama ghafla baada ya mabadiliko ya benchi la ufundi.

Kiungo huyo alikiri kuwa kipindi hicho kilikuwa kigumu sana, kiasi cha kufikiria kuondoka Old Trafford kwa mkopo, ombi ambalo lilizuiwa.

Katika mahojiano na Sky Sports, Mainoo alisema kupungua kwa muda wa kucheza kulimfundisha uvumilivu na nidhamu mpya katika maisha ya soka.

“Kutoka kucheza karibu kila mechi hadi kutopata nafasi mara kwa mara ilikuwa ngumu sana. Lakini nilijifunza mambo mengi kuhusu subira, nidhamu na namna ya kuishi kama mchezaji wa kulipwa,” alisema Mainoo.

Aliongeza kuwa kipindi hicho kilimsaidia kujifunza kutoka kwa wachezaji wenye uzoefu kama Casemiro, Bruno Fernandes na Joshua Zirkzee ambao walimpa moyo wa kuendelea kupambana licha ya kukosa nafasi.

Mainoo pia alikiri kuwa wakati fulani alikosa kabisa kuingia hata kama mchezaji wa akiba, jambo lililomuumiza kutokana na mapenzi yake makubwa kwa soka.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa familia na marafiki zake walimsaidia kubaki imara na kuona mwanga wa mafanikio mbele.

Kuhusu uvumi wa kuondoka klabuni, Mainoo alisema alifikiria mambo yote, lakini ndoto yake kuu imekuwa kuichezea Manchester United tangu akiwa akademi na bado anashikilia msimamo huo.

Tangu kuja kwa Michael Carrick kama kocha wa muda, Mainoo ameonekana kurejea katika kiwango chake bora, akiwa ameanza katika mechi 14 kati ya 15. Uongozi wa Manchester United pia umempa mkataba mpya wa muda mrefu unaomweka Old Trafford hadi mwaka 2031, hatua inayoonesha imani kubwa kwa kiungo huyo.