Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabosi Chelsea waendelea kupambania dili la Garnacho

TETESI Pict

Muktasari:

  • Matajiri hao wanaamini kuwa watampata nyota huyo kwa Pauni 35 milioni.

CHELSEA inaendelea na juhudi za kumsajili winga  wa kimataifa wa Argentina, Alejandro Garnacho kutoka Manchester United katika dirisha hili la usajili.

Matajiri hao wanaamini kuwa watampata nyota huyo kwa Pauni 35 milioni.

Man United inadaiwa kuhitaji kiasi kisichopungua Pauni 50 milioni ili kumuuza staa huyo, lakini Chelsea imekataa na inajaribu kutoa Pauni 35 milioni.

 Garnacho ambaye mkataba wake unamalizika 2028, alitoa asisti 10 na kufunga mabao 11 katika michuano yote msimu uliopita, lakini Man United inataka kumuuza   kwa sababu kocha Ruben Amorim haoni kama anaendana na mifumo yake.

Mchezaji huyo tayari amefikia hadi makubaliano binafsi na Chelsea juu ya masuala ya mishahara na bonasi nyingine na kitu pekee kinachokwamisha dili hilo ni ada ya uhamisho.

Staa huyo alikuwa akihitajiwa na timu nyingi Ulaya pamoja na Saudi Arabia, lakini aliwaambia wawakilishi wake kwamba timu pekee anayotaka kujiunga nayo katika dirisha hili ni Chelsea na si vinginevyo.


Morten Hjulmand

MANCHESTER United imepanga kutoa dau la Pauni 50 milioni kwa ajili ya kumsajili kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Denmark, Morten Hjulmand katika dirisha hili ikiwa itashindwa kuipata huduma ya Carlos Baleba, 21, anayeichezea Brighton na timu ya taifa ya Cameroon.  Hjulmand ambaye alijiunga na Sporting Agosti 2023 akitokea Lecce kwa Euro 18 milioni, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028.



Eberechi Eze

TOTTENHAM Hotspur ina imani kuwa ofa ambayo imepanga kuiwasilisha kwa ajili ya kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa England, Eberechi Eze, 27, itaishawishi Crystal Palace kukubali kumuuza. Inaelezwa Spurs ipo tayari kutoa takriban Pauni 68 milioni. Eze ni mmoja kati ya wachezaji muhimu wa Palace akifunga mabao 11 na kutoa asisti sita msimu uliopita. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2027.


Yoane Wissa

NEWCASTLE United iko karibu kukamisha usajili wa winga wa Brentford na timu ya taifa ya DR Congo, Yoane Wissa, 28. Mabosi wa Newcastle imelazimika kuangukia kwa staa huyo baada ya wachezaji wengi waliokuwa ikiwataka dirisha hili kujiunga na timu nyingine. Brentford tayari imeshapata mbadala wa Wissa ambapo itamsajili staa wa Bournemouth, Dango Ouattara, 23.


Rasmus Hojlund

FULHAM imeonyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa kimataifa wa Denmark anayeichezea Man United, Rasmus Hojlund ambaye pia anawindwa na AC Milan. Hojlund alisajiliwa na Man United Agosti 2023 akitokea Atalanta kwa Euro 75 milioni na msimu wa kwanza EPL alifunga mabao 16 kwenye michuano yote. Mkataba wake na Man United unaisha 2028.


Ademola Lookman

INTER Milan imepanga kutumia wiki moja zaidi kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Atalanta na timu ya taifa ya Nigeria, Ademola Lookman katika dirisha hili. Lookman ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo Atalanta msimu uliopita alifunga mabao 17 katika michuano yote.Atalanta inataka kumuuza kwa sababu mkataba wake utaisha mwisho wa msimu ujao.


Facundo Buonanotte

BORUSSIA Dortmund imeingia katika vita na Bayer Leverkusen kutaka kumsajili kwa mkopo winga wa Brighton, Facundo Buonanotte, 20, katika dirisha hili. Buonanotte aliyesajiliwa na Brighton Desemba 2022 kutoka Rosario Central, mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2028. Facundo msimu uliopita alicheza kwa mkopo Leicester mechi 31 kiwango chake pia kinazivutia timu kibao.


Oleksandr Zinchenko

ARSENAL ipo tayari kusikiliza ofa kutoka timu zinazotaka kumnunua beki wa kushoto, Oleksandr Zinchenko katika dirisha hili. Taarifa zinadai staa huyu mwenye umri wa miaka 28, anahitajika na timu mbalimbali ikiwemo FC Porto, Fenerbahçe, na Real Betis. Zinchenko ambaye alijiunga na Arsenal Julai 2022 akitokea Man City kwa Euro 35 milioni, mkataba wake unamalizika 2026.